CCM na CHADEMA mnafanya siasa kweli!


VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,988
Likes
7,898
Points
280
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,988 7,898 280
Sasa siasa zinafanyika kweli. Siasa ni hoja,mbinu na mikakati.Maneno yakutosha;sera za ‘kumwaga';wagombea wenye 'sifa', nia kweli na vyama vyenye ushawishi mkubwa. Hii sasa ndiyo siasa. Ingawa sote tunalenga kuijenga nchi yetu ya Tanzania, tofauti lazima ziwepo. Bila ya tofauti hakutakuwa na kujirekebisha wala kusonga mbele.Hatutaendelea. Tutabaki tulipo.

CCM na CHADEMA sasa ni ‘hatua kwa hatua',bega kwa bega. Halali mtu;ukilala hauamshwi. Upinzani umeenea karibu nchi nzima. Kuanzia Mashariki hadi Magharibi;Kaskazini hadi Kusini. Siasa za vyama vingi si tu kama zipo lakini pia zinaonekana kuwepo.

Hapa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake;pale Freeman Aikaeli Mbowe na makamanda wake. Siasa zinafanywa Bungeni,runingani,majukwaani,mitaani,kwenye kampeni na kwingineko. Mchuano huu sasa umefika patamu. Sasa ni hama huku-njoo huku. Yaani mbaya huku,mzuri kule.

Siasa za CCM na CHADEMA zinafanywa kidijitali sana. Watu wanapondana na baadaye wanakutana. Wanasemana baadaye wanachekeana. Ndizo siasa za kisasa. Matusi na kejeli zisizo na mpango hazina nafasi. Tuanataka sera na si hela.

Jumapili kutafanyika Uchaguzi Mdogo wa nafasi za Udiwani katika mikoa mbalimbali nchini. Kila mkoa,CCM na CHADEMA mpambano ni moto. Kila upande unatarajia ushindi.Ni kama enzi za mpambano wa ndondi kati ya Mohammad Alli na George Foreman. Jumatatu, watanzania wataanza kupokea matokeo. Washindi watatangazwa.Watakuwa watumishi wetu.

Upinzani wa dhati uliopo nchini kwasasa unasaidia mambo mengi. Viongozi hawajisahau tena. Ufisadi unapungua. Uhakika wa kushinda kwakuwa uko chama fulani haupo tena. Hakuna urahisi wa kupita bila kupingwa.Miradi ya maendeleo inakodolewa macho na kulindwa. Tunapata maendeleo.

CCM na CHADEMA, endeleeni hivyo hivyo hadi kieleweke!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Messages
3,304
Likes
48
Points
145
mdeki

mdeki

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2011
3,304 48 145
Sawasaw ndugu kitaeleweka lini sasa?
 
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Messages
2,364
Likes
21
Points
135
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2011
2,364 21 135
Kama nia ni moja ya kujenga Taifa ambalo ni Tanzania,kwa nini ccm inateka makada na wanachama wa cdm na hata kuwakata mashoka na wengine kutishiwa bastola na hata kuwawa? au wanaofanyiwa hayo hawana uraia wa nchi hii? "hubiri mazuri na pia kemea mabaya"
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,914
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,914 2,483 280
mkuu VUTA-NKUVUTE wakati fulani unaongea mambo ya msingi sana.Hata hivyo sasa naanza kupata picha kwamba wewe ni mtu wa namna gani.
 
Last edited by a moderator:
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
16,965
Likes
9,970
Points
280
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
16,965 9,970 280
hueleweki, nini kieleweke
 
N

ngoshas

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
707
Likes
10
Points
0
N

ngoshas

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
707 10 0
Cku ikifikia kampeni ckatawaliwa na bendera za taifa, hapo kitakuwa kimeeleweka, hy ya bendera za vyama Ni kwa manufaa ya vyama
 
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
5,988
Likes
7,898
Points
280
VUTA-NKUVUTE

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
5,988 7,898 280
mkuu VUTA-NKUVUTE wakati fulani unaongea mambo ya msingi sana.Hata hivyo sasa naanza kupata picha kwamba wewe ni mtu wa namna gani.
Mkuu betlehem, mimi ni kati ya watu wachache wa nchi hii wapenda siasa za kweli na za ushindani.Kwa umri wangu huu, sina cha kupoteza kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Wakuvanga

Wakuvanga

Member
Joined
Jun 2, 2011
Messages
25
Likes
0
Points
3
Wakuvanga

Wakuvanga

Member
Joined Jun 2, 2011
25 0 3
Mzee Tupa tupa Arusha utaenda wewe>>>???!! Chezea Lema wewe, kaamua kuachia posho zote bungeni halafu wanaLumumba wote wamehamia Arusha kwa mategemeo ya kupata walau kata moja. Waambie jamaa zako kuwa hata hao wananchi wanaofika kuwasikiliza kwenye mikutano yao wanawaenjoy mwisho wa siku wanapiga kura CDM. Pamoja na kumleta mtu mliyemwagia tindikali nyie wenyewe mkitegemea huruma ya wapiga, Wambie kina Mwigulu na Nape wategemee kichapo kikali. Vp umebaki wewe mwenyewe ndo unalinda ofisi hapo Lumumba?
 

Forum statistics

Threads 1,274,335
Members 490,676
Posts 30,508,696