CCM na ahadi kwa miaka 60

CCM na ahadi kwa miaka 60

Fwimbo

Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
82
Reaction score
214
Wadau leo ninapenda niliweke hili suala uwanjani kwa kuwa naamini humu kuna wana CCM, wana Chadema, nk. Kwa ujumla ccm ni zao la TANU na ASP na kwa mantiki hiyo tokea mwaka 1961 ccm iko madarakani. Ni kuanzia huo mwaka walichukua majukumu ya kusimamia maendeleo ya nchi kama vile kujenga Barabara, reli, kuwekeza kwenye umeme,Huduma za usafirishaji( majini ,nchi kavu na angani). Pia ilipewa majukumu ya kusimamia uwepo na ubora wa Huduma za kijamii kama vile Huduma za Afya, elimu na upatikanaji wa Maji.

Jambo la kushangaza kila mwaka wa uchaguzi Hiki chama cha CCM kinakuja na ajenda zilezile kuwa wachaguliwe wajenge miundombinu, barabara , reli , hospitali,shule, nk. Hata mwaka 2015 walikuja na hizo ajenda na mwaka huu hakuna kilichobadirika katika ahadi zao kwa wapiga kura. Sasa jambo la kujiuliza je hawa CCM ni kweli kuna uwezekano wa kupata suluhu ya changamoto ambazo kwa miaka 60 wameshindwa kuzitatua?

Je CCM mmekosa ahadi nyingine kiasi kwamba kila mwaka wa uchaguzi mnarudi na hizo ahadi kana kwamba hamkuwa kwenye madaraka? Je hamuoni ni muda sahihi wa kukaa pembeni kupisha mawazo na njia mbadala wa kutatua kero za wananchi? Please njooni na hoja na siyo vioja, karibuni.
 
Wadau leo ninapenda niliweke hili suala uwanjani kwa kuwa naamini humu kuna wana CCM, wana Chadema, nk. Kwa ujumla ccm ni zao la TANU na ASP na kwa mantiki hiyo tokea mwaka 1961 ccm iko madarakani. Ni kuanzia huo mwaka walichukua majukumu ya kusimamia maendeleo ya nchi kama vile kujenga Barabara, reli, kuwekeza kwenye umeme,Huduma za usafirishaji( majini ,nchi kavu na angani). Pia ilipewa majukumu ya kusimamia uwepo na ubora wa Huduma za kijamii kama vile Huduma za Afya, elimu na upatikanaji wa Maji.
Jambo la kushangaza kila mwaka wa uchaguzi Hiki chama cha CCM kinakuja na ajenda zilezile kuwa wachaguliwe wajenge miundombinu, barabara , reli , hospitali,shule, nk. Hata mwaka 2015 walikuja na hizo ajenda na mwaka huu hakuna kilichobadirika katika ahadi zao kwa wapiga kura. Sasa jambo la kujiuliza je hawa CCM ni kweli kuna uwezekano wa kupata suluhu ya changamoto ambazo kwa miaka 60 wameshindwa kuzitatua? Je CCM mmekosa ahadi nyingine kiasi kwamba kila mwaka wa uchaguzi mnarudi na hizo ahadi kana kwamba hamkuwa kwenye madaraka? Je hamuoni ni muda sahihi wa kukaa pembeni kupisha mawazo na njia mbadala wa kutatua kero za wananchi? Please njooni na hoja na siyo vioja, karibuni.
Wadau karibu kwenye mjadala..
 
Kama Rais Magufuli kwa miaka mitano tu ametupeleka uchumi wa kati

Je tukimuongezea miaka mitano?

Je tukimuongea tena miaka mitano?
 
Kama Rais Magufuli kwa miaka mitano tu ametupeleka uchumi wa kati

Je tukimuongezea miaka mitano?

Je tukimuongea tena miaka mitano?
Safari ya uchumi wa kati hakuanzia kwa Magufuli bali ni kwa Mkapa, ikaja kwa Kikwete ndo ikapokelewa na Magufuli. Pia huwezi kunishawishi kuwa tuko uchumi wa kati na wakati nchi haima uwezo wa kulipa madeni.
 
Kama Rais Magufuli kwa miaka mitano tu ametupeleka uchumi wa kati

Je tukimuongezea miaka mitano?

Je tukimuongea tena miaka mitano?
Hoja hapa mmetawala miaka 60 KILA baada ya miaka mitano mnatuambia porojo zilezile....mnawadanganya mburula wenzenu eti uchumi wakati uchumi wa kati,wakti KILA saa inayopita mtu anadondoka kwa njaa..we nenda kachukua buku Saba yako...MAANA NDIO INAYOKUPOFUSHA MACHO

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Moderators mmeondoa post yangu ya Nani kati ya Mh. Lissu na Mh. Magufuli anayetetea ushoga? Sasa nauweka ushahidi wa Mh. Magufuli kuunga mkono ushoga ambao ni kauli ya serikali
 
Attachments

  • FB_IMG_16020625808011409.jpg
    FB_IMG_16020625808011409.jpg
    24.9 KB · Views: 5
Back
Top Bottom