saitama_kein
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 981
- 100
MWENYEKITI wa UVCCM, Hamad Masauni Yussuf, anadaiwa kughushi cheti cha kuzaliwa kwa lengo la kudanganya umri ili aweze kupata nafasi ya uongozi.
Anamiliki cheti cha kuzaliwa bandia chenye namba E. 00023509 kilichotolewa Juni 15, 2007 na kuonyesha kwamba amezaliwa Oktoba 3, 1979.
KUMBE
Detail toka Pasi ya kusafiria ya Januari 28, 2005 zina maelezo kwamba alizaliwa Oktoba, 1973.
KATIBA YA CCM: Nitasema ukweli daima, fitina kwangu ni mwiko!!
🙂::KICHEKESHO::🙂
Source: Tanzania daima
Asante Sonara...kweli Zanzibar ni zaidi ya tuijuavyo.....Hilo lisikustajabisheni kwani Baba yake aliyemzaa ndie aliyekuwa Mtoa Pass hapa Zanzibar akishirikiana na mama mmoja kwa jina Bi Asia nasikia yupo mbele ya haki kwa sasa.
Bila ya Mzee Masauni ilikuwa Ng'oo kuipata pass hapa zanzibar na wahindi wengi pamoja na watu wa mataifa ya karibu waliondokea kwa pass za Tz kwenda Ng'ambo miaka ile.
Kwa taarifa yako mzee Masauni ndie aliyeifanya Batili na kuwa halali ule mwaka ?? palipo bakia utajaza
Tanzania yenye neema inawezekana bila ya CCM jamani eeeh.......THE WAY FORWARD: Hawa CCM wameshajiaminisha kwamba hakuna Tanzania bila CCM, na mbaya zaidi wamashaamini kwamba watanzania ni 'hamna kitu' (brain dead) kiasi kwamba hawana hofu kutenda kosa lolote. Hii ni dharau iliyopitiliza.....let's put them aside for a while wajifunze
Mrithi husana.
Alianza baba yake kuwa fisadi yeye anaendeleza tu ila hizi taarifa kama za upande mmoja na source ni chombo cha habari makini Tz daima tulitaka mizani ya habari kwa kumtafuta Yussuf mwenyewe naye ajibu "mashitaka" yake.
Mara nyingi watu wa tabia hii huwa hawajibu simu kutoka namba ya wasiyemjua. Hata hivyo atakanusha tu, bila ya kutoa hoja zozote, kama vile RA anavyokanusha tuhuma zake kem kem. Wamezoea hivyo.
mkuu kwa kigezo cha umri tunawafukuza wengi wa kina Edwin sanda, beno malisa
Katiba yao inasema "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko".....Kwani kuna ubaya gani wakifukuzwa?
unless awe mzee wa Igunga
Sijui chama chao cha kifisadi kama kitamwajibisha kwa kuwa ile ahadi ya kusema ukweli daima siku hizi imezidishwa kwa hasi moja.
Hii ndio Tanzania yenye wenyewe....Huu mfumo hauwezi ku last we need to do something kama taifa...ni pale ambapo tutaweza kuweka tofauti zetu za kisiasa,kidini na kikabila pembeni na kupambana na uchawi,ukafiri, vinyago vya namna hii...! sijui tunawarithisha nini watoto wetu....any way sikumbuki hata mimi nimerithi nini!MWENYEKITI wa UVCCM, Hamad Masauni Yussuf, anadaiwa kughushi cheti cha kuzaliwa kwa lengo la kudanganya umri ili aweze kupata nafasi ya uongozi.
Anamiliki cheti cha kuzaliwa bandia chenye namba E. 00023509 kilichotolewa Juni 15, 2007 na kuonyesha kwamba amezaliwa Oktoba 3, 1979.
KUMBE
Detail toka Pasi ya kusafiria ya Januari 28, 2005 zina maelezo kwamba alizaliwa Oktoba, 1973.
KATIBA YA CCM: Nitasema ukweli daima, fitina kwangu ni mwiko!!
🙂::KICHEKESHO::🙂
Source: Tanzania daima
Kumtendea Masuni haki ni pamoja na kutoa data ya kusupport hiyo ya kugushi. Labda kulikuwa na makosa wakati wa kutoa pasi ya kusafiria ambapo iliandikwa mwaka 1973 badala ya 1979. Lakini kwa kuwa hakuishi kwenye dunia yake pekee, tofuati ya miaka 6 ni kubwa sana! Mathalani shule ya msingi wengi walianza wakiwa na umri wa miaka 6-7, tukipata shule alizosoma na miaka aliyosoma itatupa mwanga zaidi ya kuanza kubaini ukweli. Kwani hawezi alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 0, na wala hawezi kuwa alisoma peke yake, unless awe mzee wa Igunga
Sijui chama chao cha kifisadi kama kitamwajibisha kwa kuwa ile ahadi ya kusema ukweli daima siku hizi imezidishwa kwa hasi moja.
Hahaaaa.......Sina cha kuongezea Mkuu Nono maana hapo ni pagumu kwa Mh. Masauni kujinasua kuwa kaanza shule akiwa na umri wa miaka sifuri au akiwa kichanga cha mwaka mmoja, tunaomba waliokuwa wakimbeba na kumpa 'kichanga' hiki chupa ya maziwa darasani (shule ya msingi) watuletee data.
Sishangai kwa serikali hii ya CCM. Wao walishabariki kila aina ya ubazazi including forged certificates(being academic or birth).
Kama mnakumbuka, kulitolewa orodha ndefu ya wabunge na mawaziri/manaibu mawaziri waliokuwa na forged academic certificates, lakini katika hali ya 'huyu ni mwenzetu', spika 6 alifunika hiyo ishu na kuna taarifa baadhi wameingia darasani kutafuta elimu ya kweli kweli. Ni kitu serious kinachoweza hata kugharimu serikali ku-collapse pale mawaziri/manaibu mawaziri watano wame-forge elimu wanapothibitika kufanya hivyo ila kwa CCM, mambo ni tambarare (business as usual). Wapo wengi tu.
THE WAY FORWARD:
Hawa CCM wameshajiaminisha kwamba hakuna Tanzania bila CCM, na mbaya zaidi wamashaamini kwamba watanzania ni 'hamna kitu' (brain dead) kiasi kwamba hawana hofu kutenda kosa lolote. Hii ni dharau iliyopitiliza.....let's put them aside for a while wajifunze.