CCM Mwaka 2025, mtamruhusu Rais Samia achukue fomu pamoja na wagombea wengine ndani ya chama chenu?

Sitaki kujadili Reaction ambayo Chama cha Mapinduzi kimechukua kufuatia kile kinachoitwa uzushi wa Gazeti linatolewa kila Siku la Chama cha Mapinduzi, Gazeti la UHURU juu ya mama kudai kuwa hatogombea Uraisi mwaka 2025.

Kimsingi, hatua zilizochukuliwa za kusimamishwa kazi kwa Uongozi wa Gazeti na Kufungiwa Gazeti lenyewe katika muda usiopungua saa Ishirini na nne(24) zimeniachia Tafakari kubwa sana. Na hicho ndio kimenifanya nilete bandiko hili.

Hebu kwanza naomba tukumbushane kweli Nne(4) hiv ambazo ndio kiini cha bandiko hili.

Mosi, sote tunajua kuwa mama aliingia Madarakani kwa kurithi nafasi ya Uraisi kutoka kwa Marehemu Magufuli. Marehemu Magufuli alipata nafasi ya kukiwakilisha Chama chake kwa mara ya kwanza mwaka 2015 baada ya kupenya Kinyang’anyiro cha uteuzi ndani ya Chama chake. Na kila msomaji na Mtanzania anakumbuka ni watia Nia wangapi walikuwa wamechukua Fomu wakati ule na mtanange ulikuwaje mpaka kubakia Magufuli peke yake.

Jambo la pili, kwa mjibu wa taratibu za CCM, mgombea akishapitishwa kuwania Uraisi baada ya mchujo kama ule wa mwaka 2015 na kutumikia nafasi ya Uraisi kwa miaka 5, basi ile miaka mitano mingine inayofuatia anakuwa ni mgombea pekee katika chama chake. Hali hii tuliishuhudia kwa Maraisi Ali Hassan Mwinyi, Benjamini William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na mwaka jana kwa marehemu John Pombe Joseph Magufuli.

Jambo la tatu
, Raisi anayetumikia muda wa miaka kumi anakuwa na Makamu wa Raisi.Huyu Makamu wa Raisi naye ni Raisi na ndio maana kwa mfano hata pale ambapo marehemu Magufuli alipofariki mama ameweza kuchukua nafasi hiyo ya Uraisi bila kuhitaji uchaguzi mwingine ambao ungalihitaji michakato ya wagombea ndani ya vyama kuomba kuteuliwa na vyama vyao. Kwa kukata maneno, ni kwamba mama ni Raisi anayetokana na uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na sio Raisi Mpya. Raisi mpya ni yule anayetokana na uchaguzi Mkuu. Mama hajatokana na uchaguzi mkuu. Nadhani Katiba inaeleza ukweli huo. Hapa kuna wengine wanachapia kuwa “…Mama baada ya kuchaguliwa alianza vizuri…”. Mama hajachaguliwa wala kuteuliwa.

Jambo la Nne,Marehemu Raisi Magufuli kwa kutambua kuwa Katiba inatoa ukomo wa Madaraka katika nafasi ya Uraisi na makamu wake, alikwisha kuweka hadharani kuwa baada ya miaka hii mingine mitano kumalizika yeye na aliyekuwa makamu wake wangeachia nafasi zao na kutoa mwanya kwa kinyang’anyiro kingine ndani ya chama chao kuanza ili kumpata mgombea mwingine. Jambo hili lilikuwa wazi na mama analijua maana lilisemwa mchana kweupe. Na kwa Lugha nyingine ni yeye pia alisema hivyo au alikubaliana na ukweli huo wa Kikatiba maana hakuwahi kukanusha.

Sasa bada ya utangulizi wangu huo wa hoja nne,ambazo kimsingi ni Utamaduni, Desturi na Utaratibu uliozoeleka ndani ya CCM na kufuatia tukio la Gazeti la UHURU kuandika uzushi kuwa mama hana nia ya kuendelea na kugombea Uraisi,mimi napenda kuchokoza mjadala. Nachokoza mjadala ili CCM itueleze:

1. Kwa kuwa mama hajasema kuwa hana nia ya kugombea nafasi aliyonayo mwaka 2025, yeye mama amejipangaje? Kama UHURU wameeleza Uongo,basi kinyume chake ni kweli kuwa ATAGOMBEA mwaka 2025?

2. Ikiwa mama atagombea nafasi hiyo, atakuwa anagombea kwa utamaduni upi wa CCM kati ya hizo tamaduni nne(4) nilizozieleza hapo juu?

3. Je, Mama ikiwa atagombea, atakuwa radhi kuruhusu na wanachama wenzie wachukue fomu bila mizengwe na kisha wachuane katika kuteuliwa na Chama maana kimpangilio mwaka 2025 ni wakati tena wa mgombea ndani ya chama kupatikana baada ya kushindanishwa na wenzie?

4. Je, ikiwa mama atachukua fomu kugombea, atakuwa anaichukulia vipi ile kauli aliyokuwa ameshaitoa marehemu Raisi Magufuli kuwa baada ya miaka kumi wanapaswa kupumzika?

5. Je, ikiwa atagombea na watakatokea wapambe ndani ya Chama na madai kuwa mama anapaswa kuachiwa peke yake ili amalizie muda wake wa miaka mitano, si atakuwa ni Kiongozi wa kwanza Tanzania kutawala bila kuwa ameshiriki mchujo ndani ya Chama chake kama Viongozi wengine wa Taifa hili waliomtangulia? Na je katika mazingira kama hayo, CCM itakuwa imeongeza utamaduni mpya kabisa na ambao sasa utakuwa wa tano(5) katika zile Nne nilizozibainisha hapo juu?

6. Je, ikitokea wagombea wengine ndani ya Chama wamekatazwa kugombea pamoja na mama au wakaruhusiwa lakini wakafinywa kura zao zisitoshe ili kumtomuaibisha mwenyekiti wao wa Chama, mama naye atakuwa anajihesabu kama mgombea kipanga, mwenye weledi, aliye smart kichwani na ambaye ameshindanisha maono yake na wenzie na ambaye amewashinda wenzie kwa hoja na Agenda ndani ya Chama chake?

Ninaomba tujadiliane kujibu maswali haya na ikiwezekana wenye chama chao waje watusaidie kutafakari pamoja. Na kwa nafasi ya pekee akina Chongolo waje sasa wajibu hapa kwa kuwa mama hajasema kuwa hatogombea, sasa anasemaje? Atagombea na kama ndivyo, atagombeaje wakati walishaweka wazi kuwa wao mwaka 2025 wanapumzika?
Maelezo mareeeeefu lakini majibu yake mafupi tu. Utaratibu wa CCM, kama Rais aliye madarakani kupitia chama chake ana sifa ya kugombea kipindi kingine, basi anakuwa "Mgombea" pekee. Kwa Mama haijalishi ameingiaje, maadam ana sifa nilizotaja awali, basi ujue ATAGOMBEA PEKE YAKE NDANI YA CCM!
 
Kwa hali iliyopo sasa ( tume ya uchaguzi, Katiba nk. ) hata CCM wakiamua kuweka jiwe ili lishindine na vyama vingine kwenye uchaguzi...... ni wazi CCM watashinda
 
Huo ndio unapaswa kuwa ukweli kuwa mama anamalizia Awamu ya Tano ambayo waliianza na Mwenzie. Kutaka kujifanya eti hii ni awamu mpya ni kutaka kutafuta wepesi wa kutawala miaka 10. Yeye kama anaona anao uwezo wa kutawala kwa miaka 10 basi akubali kushindanishwa na wenzie. Huwezi kutaka kutawala miaka 10 kwa dezo. Wenzie wote waliomtangulia walitoka jasho kupitishwa na Chama. Yeye atoe nafasi na wenzie wachukue nafasi wachuane na akishinda kwa hoja na Agenda ndio abebe Bendera ya Chama chake na hiyo Demokrasia. Kifo cha mtu mwingine huwezi kukichukulia kama Bahati ya kuanza kutaka kufanikisha yale ambayo ulikuwa huwezi hata kuyafanya.
Mimi nilianza kushtuka pale mama aliposema hii ni awamu ya sita na si ya tano, anajiondoa kwenye awamu ya tano ambayo ni mmojawapo na ndio anayotumia kutuongoza! hii ya kusema ni utawala wa awamu ya sita una jambo nyuma ya pazia. Na hata kubadili slogan ya HAPA KAZI TU ni kutaka kujivua uzamani na kuwa mpya.
 
Jiandaeni kisaikolojia mama anamalizia kipindi cha mutangilizi wake hii miaka mi4 mpka 2025 atachukua fimu kwa ajili ya kugombea yeye kama yeye kwa mara ya 1 kwa iyo kipindi chake cha 1 kitaanza mwka 2025 ikifika 2030 atagombea tena kwa mara ya 2 akiwa kama yeye hivo kipindi chake cha 2 kitaa isha 2035 ndo mama katiba haitamruhusu kugombea kinyume na hapo yeue mwenyewe aamue kupumzika ila akitaka kuendelea katiba inamhmruhusu jmn tuendelee na mtori nyama tutazikuta chini
 
Larger than life Prof. Palamagamba Kabudi alitisha kila aliposimama ! Ingawa alikuwa mgeni katika chama chao na utumishi ktk baraza la mawaziri lakini ghafla akaibuka kuwa mzalendo namba 2 wa Taifa la Tanzania

TOKA MAKTABA
JANUARY 2, 2022

WAZIRI KABUDI, PROF LUOGA WAZUNGUMZA KWENYE MJADALA WA USIMAMIZI WA MIKOPO KATIKA MIRADI..

WAZIRI wa Katiba na sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, leo Januari 02, ameshiriki mjadala wa kujadili umuhimu wa usimamizi mzuri wa mikopo katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati na maendeleo ya wananchi..

Source : Global TV online
 
Sitaki kujadili Reaction ambayo Chama cha Mapinduzi kimechukua kufuatia kile kinachoitwa uzushi wa Gazeti linatolewa kila Siku la Chama cha Mapinduzi, Gazeti la UHURU juu ya mama kudai kuwa hatogombea Uraisi mwaka 2025.

Kimsingi, hatua zilizochukuliwa za kusimamishwa kazi kwa Uongozi wa Gazeti na Kufungiwa Gazeti lenyewe katika muda usiopungua saa Ishirini na nne(24) zimeniachia Tafakari kubwa sana. Na hicho ndio kimenifanya nilete bandiko hili.

Hebu kwanza naomba tukumbushane kweli Nne(4) hiv ambazo ndio kiini cha bandiko hili.

Mosi, sote tunajua kuwa mama aliingia Madarakani kwa kurithi nafasi ya Uraisi kutoka kwa Marehemu Magufuli. Marehemu Magufuli alipata nafasi ya kukiwakilisha Chama chake kwa mara ya kwanza mwaka 2015 baada ya kupenya Kinyang’anyiro cha uteuzi ndani ya Chama chake. Na kila msomaji na Mtanzania anakumbuka ni watia Nia wangapi walikuwa wamechukua Fomu wakati ule na mtanange ulikuwaje mpaka kubakia Magufuli peke yake.

Jambo la pili, kwa mjibu wa taratibu za CCM, mgombea akishapitishwa kuwania Uraisi baada ya mchujo kama ule wa mwaka 2015 na kutumikia nafasi ya Uraisi kwa miaka 5, basi ile miaka mitano mingine inayofuatia anakuwa ni mgombea pekee katika chama chake. Hali hii tuliishuhudia kwa Maraisi Ali Hassan Mwinyi, Benjamini William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na mwaka jana kwa marehemu John Pombe Joseph Magufuli.

Jambo la tatu
, Raisi anayetumikia muda wa miaka kumi anakuwa na Makamu wa Raisi.Huyu Makamu wa Raisi naye ni Raisi na ndio maana kwa mfano hata pale ambapo marehemu Magufuli alipofariki mama ameweza kuchukua nafasi hiyo ya Uraisi bila kuhitaji uchaguzi mwingine ambao ungalihitaji michakato ya wagombea ndani ya vyama kuomba kuteuliwa na vyama vyao. Kwa kukata maneno, ni kwamba mama ni Raisi anayetokana na uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na sio Raisi Mpya. Raisi mpya ni yule anayetokana na uchaguzi Mkuu. Mama hajatokana na uchaguzi mkuu. Nadhani Katiba inaeleza ukweli huo. Hapa kuna wengine wanachapia kuwa “…Mama baada ya kuchaguliwa alianza vizuri…”. Mama hajachaguliwa wala kuteuliwa.

Jambo la Nne,Marehemu Raisi Magufuli kwa kutambua kuwa Katiba inatoa ukomo wa Madaraka katika nafasi ya Uraisi na makamu wake, alikwisha kuweka hadharani kuwa baada ya miaka hii mingine mitano kumalizika yeye na aliyekuwa makamu wake wangeachia nafasi zao na kutoa mwanya kwa kinyang’anyiro kingine ndani ya chama chao kuanza ili kumpata mgombea mwingine. Jambo hili lilikuwa wazi na mama analijua maana lilisemwa mchana kweupe. Na kwa Lugha nyingine ni yeye pia alisema hivyo au alikubaliana na ukweli huo wa Kikatiba maana hakuwahi kukanusha.

Sasa bada ya utangulizi wangu huo wa hoja nne,ambazo kimsingi ni Utamaduni, Desturi na Utaratibu uliozoeleka ndani ya CCM na kufuatia tukio la Gazeti la UHURU kuandika uzushi kuwa mama hana nia ya kuendelea na kugombea Uraisi,mimi napenda kuchokoza mjadala. Nachokoza mjadala ili CCM itueleze:

1. Kwa kuwa mama hajasema kuwa hana nia ya kugombea nafasi aliyonayo mwaka 2025, yeye mama amejipangaje? Kama UHURU wameeleza Uongo,basi kinyume chake ni kweli kuwa ATAGOMBEA mwaka 2025?

2. Ikiwa mama atagombea nafasi hiyo, atakuwa anagombea kwa utamaduni upi wa CCM kati ya hizo tamaduni nne(4) nilizozieleza hapo juu?

3. Je, Mama ikiwa atagombea, atakuwa radhi kuruhusu na wanachama wenzie wachukue fomu bila mizengwe na kisha wachuane katika kuteuliwa na Chama maana kimpangilio mwaka 2025 ni wakati tena wa mgombea ndani ya chama kupatikana baada ya kushindanishwa na wenzie?

4. Je, ikiwa mama atachukua fomu kugombea, atakuwa anaichukulia vipi ile kauli aliyokuwa ameshaitoa marehemu Raisi Magufuli kuwa baada ya miaka kumi wanapaswa kupumzika?

5. Je, ikiwa atagombea na watakatokea wapambe ndani ya Chama na madai kuwa mama anapaswa kuachiwa peke yake ili amalizie muda wake wa miaka mitano, si atakuwa ni Kiongozi wa kwanza Tanzania kutawala bila kuwa ameshiriki mchujo ndani ya Chama chake kama Viongozi wengine wa Taifa hili waliomtangulia? Na je katika mazingira kama hayo, CCM itakuwa imeongeza utamaduni mpya kabisa na ambao sasa utakuwa wa tano(5) katika zile Nne nilizozibainisha hapo juu?

6. Je, ikitokea wagombea wengine ndani ya Chama wamekatazwa kugombea pamoja na mama au wakaruhusiwa lakini wakafinywa kura zao zisitoshe ili kumtomuaibisha mwenyekiti wao wa Chama, mama naye atakuwa anajihesabu kama mgombea kipanga, mwenye weledi, aliye smart kichwani na ambaye ameshindanisha maono yake na wenzie na ambaye amewashinda wenzie kwa hoja na Agenda ndani ya Chama chake?

Ninaomba tujadiliane kujibu maswali haya na ikiwezekana wenye chama chao waje watusaidie kutafakari pamoja. Na kwa nafasi ya pekee akina Chongolo waje sasa wajibu hapa kwa kuwa mama hajasema kuwa hatogombea, sasa anasemaje? Atagombea na kama ndivyo, atagombeaje wakati walishaweka wazi kuwa wao mwaka 2025 wanapumzika?
Kimsingi Mama ni zao la Awamu ya 5 ambayo ilianza 2015 Na kama ni Miaka 10 basi UKOMO wa AWAMU ya 5 ni 2025
Awamu ya 6 inapaswa ije na WATU WAPYA KABISA ila Ngoja tusubiri MCHUZI ni Mwingi Nyama zipo Chini

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom