Bumpkin Billionare
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 1,332
- 621
Kitendo alichokifanya Nape
leo yaani utafikiri ni kiongozi wa serikali kama RC au DC kuwa na mtu wa
chama tena upande wa propaganda!!!!
Ndiyo haya ya kumpigia salute mama Salma na kumsomea ripoti kama
kiongozi wa nchi!!!!!
Nadhani unaweza kupata picha ya upeo wa viongozi wateuliwa wa JK,...huyo ndo alikuwa DC wa wilaya fulani na utendaji ulikuwa kama hivyo. Hajui mipaka yake wala job descriptions za post yake. Hajui kama yeye na Mnyika ni sawa, tunasubiri Mnyika nae aende kukagua miradi ya serikali na kutoa amri kwa viongozi wa serikali. Nadhani siku hio FFU wote wa ukonga watahamia huko. Kaaaaaaazi queli queli....Leo katika taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku, kwa macho yangu nikiwa mzima sijalewa nimeshuhudia jambo ambalo mpk sasa nimeshindwa kulielewa. Nape anaanza kudata au siasa za Tanzania zinaruhusu hiyo?
Nape anaonekana akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida (ambayo iko kwenye ukarabati na utanuzi) pamoja na maafisa kadhaa wa Hospitali hiyo na Magamba wenzake. Kilichonishangaza hapo ni kauli za Nape kwa wale maafisa wa hospitali.
Mara baada ya hotuba za blah blah (kama kawaida ya CCM) Nape alisema (nanukuu) ''....nitaiagiza serikali ikae na kufanyia marekebisho ya hii sheria maana inakwamisha ujenzi wa majengo ya serikali kwa.........''.
Kama haitoshi Nape ambaye mimi nimekuwa nikimfahamu kama kiongozi wa CCM na si Serikali aliongezea "Haya majengo ma3 yaliyokwisha kukamilika yaanze tu kutumika, sioni sababu za kusubiri wakati wananchi wanahitaji kuyatumia......"
Je huyu Nape amekuwa nani kiasi anaweza kuamua yeye majengo ya hospitali yaanze kutumika as if Waziri wa wizara husika na uongozi wa serikali ya Mkoa hauna mamlaka mpaka aje kuamua yeye?
Si kwamba dogo anachanganyikiwa baada ya magamba kumshinda sasa kichwa kinamruka na anapata illusions kuwa yeye ni waziri au mkuu wa mkoa wa Singida?
Imefikia wakati sasa CCM imuonee huruma huyu ndugu yetu. Majukumu waliyompa yamemzidi uwezo kiasi ameanza kuyakimbia na kuingilia kazi za watu wengine absent minded. Poor him, illusions.
unafuatilia kama nani serikalini, we kazi yako kubwa uliyopewa ni kupuliza vuvuzela huko kwenye kambi yenu ya majangili, si kukagua miradi iliyotekelezwa kwa kodi za wananchiMhhh, Siwashangai sana watu wa aina yako, maana cha kwenu sio chama cha siasa ni kundi la wanaharakati hata Mwenyekiti wenu kakiri kwamba sasa ndo mnafanya juhudi za kukigeuza kuwa chama cha siasa. Ndio maana kutojua kwanini nakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na ahadi za CCM kwa umma si jambo linaloshangaza! Lakini hebu tafakarini hili, kwa muda mrefu hapahapa jf mlipigana vita ya kisaikolojia kuwa ahadi za jk na ilani havitekelezwi na mlikuwa mkiniuliza mie ni kwakiasi gani ahadi zinatekelezwa, sasa leo nafuatilia kuona kasi ya utekelezaji, MNAKURUPUKA BILA AIBU MNABWABWAJA MANENO YA AJABU!! AMA KWELI NDO TABU YA KUWA WAFUASI WA KUNDI LA WANAHARAKATI BADALA YA CHAMA CHA SIASA!!
Si kila jambo unaloulizwa lazima uihusishe CDM ku-justify jibu, jibu linatakiwa lijitegemee, inaonekana uko obsessed sana na Chadema. Ulitakiwa ujibu swali la msingi la mleta hoja kuwa ulikagua kama nani, kama unadai ni kupata taarifa za utekelezaji wa ilani ungeweza kuzipata kwa DC au RC au Mkurugenzi wa Halmashauri. Njia uliyotumia si sahihi kwa kiongozi wa ngazi yako ya kisiasa kukagua utekelezaji.Mhhh,
Siwashangai sana watu wa aina yako, maana cha kwenu sio chama cha siasa ni kundi la wanaharakati hata Mwenyekiti wenu kakiri kwamba sasa ndo mnafanya juhudi za kukigeuza kuwa chama cha siasa. Ndio maana kutojua kwanini nakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na ahadi za CCM kwa umma si jambo linaloshangaza!
Lakini hebu tafakarini hili, kwa muda mrefu hapahapa jf mlipigana vita ya kisaikolojia kuwa ahadi za jk na ilani havitekelezwi na mlikuwa mkiniuliza mie ni kwakiasi gani ahadi zinatekelezwa, sasa leo nafuatilia kuona kasi ya utekelezaji, MNAKURUPUKA BILA AIBU MNABWABWAJA MANENO YA AJABU!!
AMA KWELI NDO TABU YA KUWA WAFUASI WA KUNDI LA WANAHARAKATI BADALA YA CHAMA CHA SIASA!!
yeye si mjumbe wa CC ya chama tawala? anaweza kuiagiza serikali ya CCM