CCM msirudie tena

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Si jambo jema. Kura zitanguliwe na ubinaadamu. Siku ya Jumamosi,kulitokea ajali iliyohusisha pikipiki na lori maeneo ya Visiga Kibaha Pwani. Ni kwenye kona mpya ya Visiga Seminari. Katika ajali hiyo,mwendesha pikipiki alifariki papo hapo huku pikipiki yake yote ikiteketea kwa moto.

Ni siku hiyo hiyo,msafara wa CCM ukiongozwa na Kinana na Nape ulikuwa unaelekea Mlandizi baada ya mkutano wa Mailimoja siku ya Ijumaa. Wakati watu wakikusanyika kumsitiri na kumuondoa marehemu kuelekea hospitali,msafara wa CCM ukapita.Wakati huo maiti ipo na pikipiki linawaka.

Pamoja na watu wengi kuwa eneo la ajali,msafara haukusimama. Kubwa zaidi,gari la matangazo lilizidisha sauti na kuweka taarabu. Hakika,marehemu alikuwa anaonekana pale. Wananchi waliguswa sana na jambo hilo. Hawakuamini walichokiona. Ajalini kweli ipigwe taarabu??!?

Wananchi wamefikia kuuliza,wangekuwa wa vyama vya upinzani wangepita wakipiga taarabu? Naomba wahusika wasirudie tena. Nasema,kura na sera zitanguliwe na utu.Wananchi wa Pwani sio cheap kihivyo!
 
Wanajishusha wenyewe kwa kukubali cheap corruption km ya kanga ,wali,n.k wakati wa uchaguzi.
Waamue moja na siyo kulalamika.
 
Hao akina kinana kila wakiona pikipiki wanafikiri na za lowasa.

Chuki ni mbaya sana.
 
Hao ndio zao usishangae wewe ujaona wananchi wanavyo tabika maji shule hospitali nk lakini kila siku kule mjengoni lakini tatu zinazama kwenye mifuko kama samaki anavyoingia baharini
 
Na ukimwona kimya leo ujue Signatory pale Lumumba leo hajafika kuidhinisha kale kaposho kao hivyo kanuna. Yaani yuko kwenye mgomo.

Ha! Ha! Haaa! Ni kweli mkuu , watoa hela wako ziarani kimanzichana .
 
Of course CCM ni chama cha wanyama wanaofanya unyama. Utu na ubinadamu kwao mwiko!!
 
Mleta uzi.hiv ukimleta diblo dibala,dally kimoko na wapiga gita wote maarufu halaf wawapigie mbuzi gita watawaelewa kwel
 
Hilo tukio nililishuhudia laivu ila basi letu lilisimama kwa muda wa dk kama 5, tulikuta wananchi ndo wanamlaza marehemu pembeni na kumfunika na jaketi kichwani huku pikipiki yake ikiteketea kwa moto, nadhani aliumia sana kichwani.

Jamani watumiaji wa bodaboda helmet ni muhimu, ukikodi pikipiki/boda abiria msione aibu kuwadhibiti hawa madereva maana wanaendesha utadhani wako kwenye mashindano sijui wanajitoaga ufahamu hawa watu hata sielewi.

Watu wa pwani nanyie mkome kuikumbatia sisiem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…