CCM msiigeuze Igunga yetu Somalia

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
TUMEFIKA pabaya naaapa! Mbona haya mambo hatukuwahi kuyashuhudia huko nyuma? Lazima iwepo namna.

Ukiwa mlokole hukawii kusema siku za kiyama zimefika na haya ndiyo yaliyonenwa kwenye maandiko.

Hivi watu hawajui mipaka ya kazi zao? Igunga wanatuletea siasa za aina mpya nawaapia. Kumbe ndiyo maana yule wanayemwita gamba alisema kuna siasa uchwara? Sasa tumeziona lakini miye simo!

Kuna hiki kituko cha mwakilishi wa mkuu wa kaya katika ngazi ya wilaya kukamatwa na wanaodai alikuwa akihujumu jambo! Hivi inawezekana vipi mwakilishi wa rais awe kwenye ziara ya kikazi halafu akakosa ulinzi wa dola?

Hapana. Hapa tunataka maelezo enyi wana. Mbona katika ngazi ya wilaya ukiona DC ndiyo umeona dola yenyewe? Ifike vipi mahali tuone watu wameiweka dola ngazi ya wilaya chini ya ulinzi?

Hiki ni kituko cha karne nawaapia lakini nasema pande zote mbili zimetuthibitishia kwamba siasa zetu sasa zimevuka mpaka.

Nasikia mama wa watu analalamika alikuwa kwenye kikao cha kikazi. Kwani maafande walikwenda wapi ili wamlinde asikumbwe na yaliyomkumba? Yeye si ndiye amiri jeshi mkuu ngazi ya wilaya? Huyo si ndiye mwakilishi wa rais? Huyo si ndiye mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya wilaya? Sasa kama usalama wake mwenyewe aliuweka rehani ataweza vipi usalama wa wengine? Nasema hapa lazima mtu ujitoe mtu wangu.

Huko si tumeshuhudia pia vituko vya watu kudai kumwagiwa tindikali na nyumba kuchomwa? Nasikia vyote hivi vinahusishwa na siasa. Tumefika huko? Hayo mambo mbona tulidhani haya yanaweza kutokea tu Somalia na huko Kandahar?

Nasikia yametokea Igunga. Tumekubali vipi kufikishwa kwenye hizi siasa za kihasama? Kumbe hatamu ina utamu watu awataki kuiachia eh? Wacha nikae kimya tu.

Nimeona na wengine wakilishwa ubwabwa. Karne ya leo ya teknolojia bado tunakubali tunachanganywa na kitu kinachogeuka kinyesi baada ya dakika chache? Kumbe mwadhani wali ule utakaa tumboni saa ngapi? Baada ya wali wewe unampa mtu ulaji miaka mitano.

Hapo unajiuliza kama huku vichwani mwetu kuna ubongo au funza? Ngoja ninyamaze maana hamkawii kusema ninatukana mtoto wa mama miye.

Hizo sarakasi nasikia zimezidi hadi kuna wakubwa kwenye hicho chama nambari wahedi wanadai eti CHADEMA wameleta makomandoo waliopata mafunzo Afghanistan na Libya.

My God! Kama huo ni ukweli basi tujue chama tawala kimeshindwa kutawala. Hadi wapinzani waweze kuingiza makomandoo intelijensia ilikuwa wapi enyi ndugu?

Kama hayo ya chama tawala ni kweli basi wapo wengi wa kujiuzulu na chama kuachia ngazi hadi makomandoo wasio rasmi wakaingia nchini. Hoja zimefika hapo?

Nasema haya ya Igunga yanatuthibitishia namna ambavyo fujo huanzishwa. Hivi mna hamu sana ya kupelekwa kizimbani na Ocampo siyo? Miye simo kabisa huko.

Kweli kabisa nchi hii yenye jeshi lake na intelijensia inayoweza kujua fujo itatokea hata kabla watu hawajakusanyika inaweza kushindwa kuwanasa makomandoo wa chama cha upinzani?

Tuambiwe lingine lenye mashiko, hili lina ukakasi watu wangu. Lakini ukiacha hayo hivi hamkuona picha ya Bwana Aden Rage yule mbunge wa Tabora Mjini akienda kwenye mkutano wa siasa na bastola kiunoni? Tumefika hapo enyi watu.

Kweli vyeo hivi vinatafutwa kwa msaada wa risasi, bado hamuoni kuna noma? Hapana….hapana. Tumekwisha. Kwani mbona tulifunzwa kwamba siasa ni sera? Nasema afadhali hata udanganye utaleta mahakama ya kadhi halafu baadaye uiruke kimanga kama ilivyokwisha kutokea kuliko kutafuta ushindi kwa gharama ya roho za watu.

Hivi hamkujifunza kitu kule Pemba nyie? Tayari roho zetu zinapukutishwa na ukimwi, ujambazi, lishe mbovu, ajali za kujitakia na ajali za kweli bado mnatuletea tena siasa za fujo?

Hapana, hata kwenye umaskini wetu bado twazipenda roho zetu enyi wana. Kwanza kwa wengi wetu hakuna kingine tunachomiliki zaidi ya hizo roho. Chonde chonde Igunga.

Nasikia wengine wanajaribu kuingiza na dini ndani ili kupata kura za huruma.

Hivi hamumuogopi hata Mwenyezi Mungu? Jamani kwenye siasa kuna uchafu wa kila aina wala msithubutu kabisa kumuingiza Mola wetu huko. Huo uchaguzi si mmejitakia wenyewe mlipoanza kuitana magamba?

Kama si hizo siasa za kuwekana uchi mnadhani mngefika hapo mlipofika? Miye simo kabisa na kamwe sikubaliani nanyi. Narudia tena simo kwenye hayo mambo yenu.

Hivi nguvu hii inayotumika kwenye kampeni za kisiasa zingetumika kwenye uzalishaji mali mbona tungekuwa dunia ya kwanza?

Naapa natamani turudie enzi za Mwalimu wakati uongozi ulipokuwa utumishi. Uliwahi kuona enzi zile watu wakifikia kumuagiana tindikali au kupanda jukwaani na silaha kiunoni inaonekana? Ni vitisho au ubabe? Nasema kama tunataka kupata ukombozi wa kweli sasa tuandamane na mashirika yasiyo ya kiserikali tuachane na blah blah za siasa. Kwa sasa hivi Igunga inaonekana lulu miongoni mwa wanasiasa lakini subiri uchaguzi uishe. Utashangaa na roho yako.


Miye nilishawaambia wakwe zangu walioko huko Igunga waendelee kwenda makondeni kulima badala ya kwenda kwenye hii mikutano watu wanayoihutubia na bastola.

Yawezekana wengine wanaona huo ni ujanja lakini nasema ni dalili mbaya. Kwetu Tanzania hatujazoea kumwona raia akitembea na silaha hadharani, hiyo labda iko Somalia.

Utamaduni huu wa kuomba kura na bastola bado ni mgeni kwetu. Chonde chonde enyi watu wangu.

Hivi hoja zimeisha hadi sasa tunazungumzia tu kwamba watu wanabishana kwa misuli?

Hii ndiyo miaka 50 ya Uhuru sio? Uhuru wa kufanya kampeni huku amani ikiwekwa rehani? Kweli tumekubali uholela wa soko miye simo huko kote mtoto wa mama.

Nawausia tu Wanaigunga tumieni akili zenu kichwani, kwani mbona pumba na mchele vinaonekana kwa macho hata bila miwani? Miye simo huko!
 
Wale vijana wa ccm waliopata mafunzo haramu mkoani singida,wakiwa na VX mbili za Ccm wamevamia hotel walipo makamanda wa Chadema.Uvamizi uliokuwa na lengo la kuwajeruhi makamanda na pia kuchoma moto fuso mbili za matangazo(PA)
Jaribio hili ovu limeshindwa vibaya,kwani vijana wetu waliwakamata na kuwadhibiti kisha kuwapeleka polisi,kwa sasa tupo kituoni,ntaendelea kuwajuza
 
twashukuru kwa taarifa zako nzuri na zenye hekima endelea na moyo huo huo.
endelea ku2jua yanayojiri humo ...i.gu.ng.a
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom