CCM mpya bila strategies ni bure

naninibaraka

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
910
668
Mipango yoyote ya chama cha siasa ni kushika ama kuendelea kushika dola. Kuendelea kushika dola kunahitaji mikakati ya muda mrefu na ya muda mfupi, hivyo vyote hili vifanikiwe lazima uwe na right people na resources zingine.

Wanaosema CCM mpya ni wale wavivu wa kuwaza, Kwa sasa kinachoiweka CCM madarakani kwa sasa siyo mikakati bali ni taasisi ambazo bado zina utii kwa mamlaka iliyepo kama jeshi la polisi, tume ya taifa ya uchaguzi nk.

CCM kama chama kilipaswa kujitathimini kwa nini kinakosa uungwaji mkono kila kukicha? Ni nini wafanye ili siasa zao ziindane na wakati? CCM ina wasomi wengi lkn wakati mwingine ukiangalia hoja zao ni nyepesi sana, hawapo focused kabisa, kwa maana nyingine mfumo wao kichama ni mbovu kabisa.

Mfano utaratibu wa kumpata mwenyekiti wa chama haupo democratic, haikuwa na haja ya kupoteza gharama za kuandaa mkutano wote ule ili hali mnajua mgombea ni mmoja na hakuna atakaye shindana naye, kwenye siasa za sasa pamoja na favours zote CCM inayopata mfano kufanya mikutano ya kisiasa, support kutoka tume ya taifa ya uchaguzi,jeshi la polisi nk bado kimekosa agenda zinazoeleweka.

CCM kama haito jitathimini kwa hizi favours wanazo zipata ijiandae kuanguka. Hii strategy mpya ya kununua wapinzani is a very poor strategy kwa chama kikubwa kama CCM.

Tunapoteza resources nyingi sana ambazo zingesaidia kuwapa huduma watanzania masikini, hakukuwa na haja ya kuchezea hela za walipa kodi kununua mbunge ama diwani ambaye hana mchango wowote kwa taifa.

Kuna strategies nyingi tu ambazo wangetumia kama chama wangeweza kufanya siasa zinazoendana na mazingira ya sasa, wasomi mliopo ccm na wengine wengi siasa za fitna siyo rafiki tena, watanzania wengi kwa sasa wameelimika.

Technology nayo inakimbia! Acheni siasa za kizamani! Mnajua kabisa hakuna fair play kwenye siasa mnabebwa kila kukicha!

Fikirieni CCM mpya kwenye fair play ya democracy, fikirieni ccm bila support ya tume ya uchaguzi, fikirieni ccm bila jeshi la polisi nk

Nawasilisha,
Asalaam
Nanyororo Barikiel
 
Strategy ni kuwanunua polisi, viongozi wa wapinzani na tume ya uchaguzi.
Walifundishwa na baba wa taifa kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 1995.
 
Mipango yoyote ya chama cha siasa ni kushika ama kuendelea kushika dola, kuendelea kushika dola kunahitaji mikakati ya muda mrefu na ya muda mfupi, hivyo vyote hili vifanikiwe lazima uwe na right people na resources zingine,wanaosema CCM mpya ni wale wavivu wa kuwaza, Kwa sasa kinachoiweka Ccm madarakani kwa sasa siyo mikakati bali ni taasisi ambazo bado zina utii kwa mamlaka iliyepo kama jeshi la polisi, tume ya taifa ya uchaguzi nk, ccm kama chama kilipaswa kujitathimini kwa nini kinakosa uungwaji mkono kila kukicha? Ni nini wafanye ili siasa zao ziindane na wakati? Ccm ina wasomi wengi lkn wakati mwingine ukiangalia hoja zao ni nyepesi sana, hawapo focused kbs, kwa maana nyingine mfumo wao kichama ni mbovu kabisa, mfano utaratibu wa kumpata mwenyekiti wa chama haupo democratic, haikuwa na haja ya kupoteza gharama za kuandaa mkutano wote ule ilihali mnajua mgombea ni mmoja na hakuna atakaye shindana naye, kwenye siasa za sasa pamoja na favours zote CCM inayopata mfano kufanya mikutano ya kisiasa, support kutoka tume ya taifa ya uchaguzi,jeshi la polisi nk bado kimekosa agenda zinazoeleweka, ccm kama haito jitathimini kwa hizi favours wanazo zipata ijiandae kuanguka, hii strategy mpya ya kununua wapinzani is a very poor strategy kwa chama kikubwa kama CCm,tunapoteza resources nyingi sana ambazo zungesaidia kuwapa huduma watanzania masikini, hakukuwa na haja ya kuchezea hela za walipa kodi kununua mbunge ama diwani ambaye hana mchango wowote kwa taifa, kuna strategies nyingi tu ambazo wangetumia kama chama wangeweza kufanya siasa zinazoendana na mazingira ya sasa, wasomi mliopo ccm na wengine wengi siasa za fitna siyo rafiki tena, watanzania wengi kwa sasa wamelimika, technology nayo inakimbia! Acheni siasa za kizamani! Mnajua kabisa hakuna fair play kwenye siasa mnabebwa kila kukicha! Fikirieni CCM mpya kwenye fair play ya democracy, fikirieni ccm bila support ya tume ya uchaguzi, fikirieni ccm bila jeshi la polisi nk
Nawakilisha,
Asalamu
Nanyororo barikiel

 
Back
Top Bottom