CCM Moshi Vijijini yamtuhumu Mbatia kutakatisha fedha kupitia asasi ya VDF

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi Vijijini kupitia tamko lake la tarehe 18/12/2018 lililotolewa na kusainiwa na Katibu wa CCM Wilaya Ndg. Miriam S. Kaaya imemtuhumu moja kwa moja mbunge wa Vunjo Mh. James Mbatia kupitia asasi isiyo ya serikali ijulikanyo Vunjo Develeopment Foundation kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu na kuitaka Serikali kupitia TAKUKURU kuichunguza haraka iwezekanavyo.

Chama Cha Mapinduzi kimepata wasiwasi mkubwa juu ya mienendo ya ufanyaji wa shughuli za asasi hiyo ya VDF kuwa inakiuka taratibu za nchi na kutoa mashaka yao juu asasi hiyo.

Ukisoma sheria ya kuzuia utakatishaji Fedha haramu sura ya 256; “ Makosa ya uhalifu ambayo ni msingi wa utakatishaji wa Fedha haramu” ina maana ya :-

(i) kugushi
(n) kujipatia Fedha au Mali kwa vitisho
(x) Uhalifu wa mazingira.

Chama Cha Mapinduzi kimetoa hoja tatu za msingi ambazo kimsingi inapata mashaka na asasi ya VDF kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu.

Hoja ya kwanza, uchangishaji wa fedha za wananchi kinyume na utaratibu. Utaratibu wa kuchangisha pesa za wananchi ni makubaliano yao kupitia mikutano mikuu wa kijiji, na kupata baraka zote toka kwa Mkuu wa Wilaya.

Asasi VDF imeshindwa kufata utaratibu na kuanza kukusanya michango kwa wananchi bila ya ridhaa yao na asasi hiyo imekuwa ikitoa vitisho kwa wananchi ambao hawajato (kubangua).

Hoja ya pili, asasi ya VDF kutumia risiti zenye nembo ya serikali. Risiti zote zinazotumika na asasi ya VDF zina nembo ya Serikali (kugushi nembo ya serikali) kimsingi ni kosa kisheria. CCM imetafsiri tendo hilo ni asasi hiyo kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Hoja ya tatu, uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanyika. Asasi ya VDF imefanya uharibifu mkubwa wa mazingira kata ya Marangu Mashariki Kijiji cha Mshiri n.k ambao unakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi million 30 kwa kukata miti ovyo na kuharibu mali za watu bila ya kibali toka serikalini.

Kwa mantiki hiyo Chama Cha Mapinduzi kimeitaka serikali kuichukulia hatua kali asasi ya VDF na mbunge wa Vunjo Mh. James Mbatia.

Nakala ya risiti za kughushi zimeambatanishwa.

#UongoziNiUtumishi #SiasaNiMaendeleo
IMG-20181226-WA0028.jpeg
IMG-20181226-WA0029.jpeg
 

Attachments

  • IMG-20181226-WA0027.jpeg
    IMG-20181226-WA0027.jpeg
    65 KB · Views: 16
Kweli huko kuna mambumbu nimesoma sijaona wapi wametakatisha fedha hapo kama hamjui mana ya utakatishaji wa fedha kaeni kimya
 
Back
Top Bottom