CCM mnawakomoa wananchi, sio UKAWA!

Msituchanganye bana. Mnyika alisema kuwa ataleta maji Ubungo. Wala hakusema kuwa ataishirikisha serikali ya CCM kutekeleza hilo. Kama kazi imewashinda rudisheni majimbo kwa CCM

Waulize hao Wabunge wako fedha wanazopewa za mfuko wa Jimbo wanazitumiaje

mwambieni mnyika tunataka maji ubungo alisema ndani ya mwezi mmoja akichaguliwa ataleta maji ubungo yako wapi sasa hayo maji aliyosema mnyika.

kwani kwa mawazo yako pesa ya mfuko wa jimbo inafanya kazi gani.
Pesa za maji zipo, tena zipo nyingi tu, zilizotolewa na wafadhili na za ndani. Uzembe na ufisadi wa serikali ya CCM ndio unakwamisha. Mnyika anafuatilia na anafanya lile analopaswa kufanya kama mbunge.

Tutaanza kufichua mabilioni yaliyotengwa kwa ajili ya maji yanavyotumika vibaya.

Kwanza kuna pesa za MCA (Milennium Challenge AccounT) kama ambavyo mradi unajieleza kwenye website ya serikali.


Hizi ilipewa wizara ya fedha moja kwa moja. Je, Mnyika atafute nyingine na kuanza project mpya?

Alipopelekwa hoja yake binafsi ya kufuatilia mradi huu, Waziri alimzima, wote tunakumbuka.

Waziri mwenyewe alituambia kuwa kuna fedha hii kwenye bajeti ya 2012/13 Namnukuu hapa

Watanzania tumekuwa wajinga. Mahali ambapo uzembe uko wazi tu, tunaleta siasa eti kuadhibu upinzani.

Mimi ntaanza kulikuza hili, nahisi kuna uchafu kama wa EPA na ESCROW.

Kwa nini Maghembe alizima hoja binafsi ya Mnyika?

Kwa nini team Lumumba inaitumia hii kama propaganda ya kumchafua Mnyika?











Tatizo si kuwa pesa hakuna, tatizo zimetumikaje?

Baada ya Escrow mnaonaje tulikuze hili limtikise Maghembe?

Ukweli ni kwamba Mnyika anachukiwa na CCM kwa jinsi anavyohoji mambo bungeni!!
 
Yaani magamba yanafikiria wananchi ni vilaza mpaka leo,tumeshamuadhiri fisadi Makongoro jana kwa kumwapisha rais wa mtaa wake Kamanda kutoka Chadema bado kumng'oa yeye na vibaraka wenzie.
 

Umenena vyema mkuu. Tatizo la chama cha Majambazi (CCM) ni kwamba hakina tena viongozi bali wamebaki wachumia tumbo peke yake. unaweza kuamini kwamba eti Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Steven Wasira, Abdurahman Kinana na wengine wote wa type yao eti ndio THINK TANK ya CCM??! sasa unategemea utapata nini hapo?!
 
Hata wakibadilisha misimamo yao kwa sasa wamechelewa sana kitakacho waokowa nikuiba kura kwa nguvu nakusababisha vita itakayo UA watanzani nahiyo dam watailipa kwa garama kubwa sana
 
serkali ni kwa ajil ya wananch wake wote inao watawala, ikiwamo maendeleo, mgawanyo wa mapato ktk mirad ya maendeleo, ukusanyaj wa kodi,ulinzi na usalama,uwekezaji n.k......Bila ya kujali utofaut wa vyama,rang,din,kabila,asili, n.k...{political tolerance}}.

Mbunge kaz yake ni kuisimamia na kuishaur sirkal juu ya mirad na mipango yote ya maendeleo, bila ya kujal ni mbunge wa chama gani.......


NAAMIN NIMEKUTOA UJINGA.


Kwani hao Wabunge wa upinzani si walisema kuwa watawaletea maendeleo wananchi? Inakuwaje wanaiangukia CCM?
 

Maendeleo hayaletwi na chama cha siasa bali juhudi binafsi na kujituma. Jiulize utaifanyia nini Tanzania na sio Tanzania ikufanyie nini.Zinduka.
 
Songoro sijui kama hujui? unaandika kuonyesha umbumbumbu wako makusudi pole kwa kujifanya jinga
 

Asiye na macho haambiwi tazama:



Hii ni Dar?
 
Asiye na macho haambiwi tazama:



Hii ni Dar?

Mama kumbuka siko hapa kwenye ushindani bali kutoa mtazamo chanya wa mgawanyo sawa wa maendeleo kwa nchi nzima. Wewe unaonenaka unajibu hoja yangu kwa ushindani wa simba na yanga, mimi siko huko. nashindwa kuelewa, are you serious or your just kidding me kwa kunionyesha daraja? Ukijaribu kuangalia miradi mingi ama nguvu kubwa inatumika kuendeleza Dar kuliko sehemu nyingine za nchi. Tatizo hili limeiacha watu wa nchi nzima wanapohitaji huduma za serekali kujikuta wanapaswa kuelekea Dar. Angalia wizara zote ziko Dar, makao makuu ya taasisi nyingi za umma yako Dar, watunga sera karibia wote wako Dar. Hali hii inawafanya hata watawala kufikiria kutatua zaidi matatizo ya Dar kwani asilimia 90 wanakaa Dar.

Hapo Dar kilichoshindikana ni kuhamishia mlima Kilimanjaro, Mbuga ya ngorongoro nk tu. Hoja yangu iko wazi, panua miji mingine kwa kupanua ama kuboresha miundo mbinu yake kama bandari, reli, viwanda na nikatolea mfano wa Tanga na Mtwara. Ukiweza kufanyia kazi mikoa hiyo automatically msongamano usio wa lazima hapo Dar utapungua na unatoa fursa ya maendeleo kwa maeneo mengine ya nchi. Sasa unaponionyesha daraja ndio umeua hoja yangu kwa jibu muafaka, ama hilo daraja limepunguza msongamano na watu kukimbilia hapo Dar? Ama wewe na wengine mmeamua kuufanyia kazi wimbo wa mwanamuziki Hamza Kalala wa kwamba tutabanana hapa hapa Dar? Ama kwa mfano mrahisi, imetokea mzazi ana familia ya watoto wengi, yakaanza kuzuka malalamiko kwa wanafamilia kwamba mmoja anapendelewa sana kwa kupewa kila kitu wakati wote wanahaki sawa, anatokea mpambe anajaribu kumtetea mzazi mwenye upendeleo kwa kuonyesha kiatu cha bei mbaya alichopewa mtoto mwingine ambaye hafanyiwi upendeleo. Ndio unachojaribu wewe kuua hoja kwa kunionyesha daraja, japo sipingi hilo daraja na sina haja ya kuwa mtovu wa fadhila, kwa hilo daraja napongeza.

Nadhani tujaribu kuweka ushabiki pembeni tunahitaji maendeleo ya uwiano kwa nchi nzima na sio kulimbikiza kila kitu sehemu moja. Matokeo yake ndio hayo hakuna mipango miji inayoeleweka ama inatekelezeka kwa shida kutokana na msongamano wa watu. Tujaribu kupunguza wizara kutoka hapo Dar na kuhamishia nyingine mikoa kama ya Mwanza, Arusha, Mbeya nk. Pia makao makuu ya taasisi za umma nyingi zinapaswa kupunguzwa hapo Dar nakuhamia sehemu mbalimbali za nchi ili kupanua ama kupeleka maendeleo kwa uwiano sehemu kubwa kama si yote ya nchi. Tukifanya hivyo kwa taasisi za umma, itachagiza na sekta binafsi kwenda sehemu hizo na watunga sera wataweza kuona kwa uhalisia nini kifanyike maeneo mengine ya nchi, na sio kutunga sera wakiwa maofisini hapo Dar. Matokeo yake kuwa na sera zisizotekelezeka sehemu kubwa ya nchi kwani watungaji hawajui uhalisia wa maeneo wanayoyatungia sera.
 


Porojo nyingi, miaka 44 ya Uhuru uliona nani kabla ya Kikwete akipeleka maendeleo, Kigoma? Kusini? Tanga, Tabora?

Leo tunayaona huko.
 
Porojo nyingi, miaka 44 ya Uhuru uliona nani kabla ya Kikwete akipeleka maendeleo, Kigoma? Kusini? Tanga, Tabora?

Leo tunayaona huko.

Nashukuru kwa kuona porojo zangu. Je huyo anayefanya sasa anatoa hisani? Naomba nikuulize swali moja ambalo ninataraji utalijibu kwa kina ili nione unajenga hoja ya kuendeleza ama unatafuta ushindi. Unaweza kuniambia tofauti ya deni letu la miaka 44 na maendeleo yaliyofikiwa na deni la taifa la miaka hii 10 ukilinganisha na maendeleo yake? Naomba usipapase macho kwani hapa panahitaji uelewa wa kina ili tuone hoja inalalia wapi. Please naamini utajenga hoja inayoendana na uelewa wako na uzito wa swali husika, kwani swali hili sikuulizi kwa bahati mbaya bali najua ninachokuuliza. Nataraji utakuja na majibu ya kina na sio majibu ya mtaani na ubishani usio na tija.
 

Naam, ni hisani kubwa sana kwa Watanzania wa mikoa hiyo ambao wengi wao hawajawahi kuona hata lami toka wazaliwe.

Deni likiwa kubwa ujuwe na uwezo wakulilipa umekuwa mkubwa. Nenda kakope wewe uone vigezo vyako vitakupa kiasi gani cha mkopo.
 
Naam, ni hisani kubwa sana kwa Watanzai wa mikoa hiyo ambao wengi wao hawajawahi kuona hata lami toka wazaliwe.

Deni likiwa kubwa ujuwe na uwezo wakulilipa umekuwa mkubwa. Nenda kakope wewe uone vigezo vyako vitakupa kiasi gani cha mkopo.

Kwa aina hii ya majibu na ujengaji hoja huo naomba niseme umenishinda. Nakupongeza kwa ushindi kwani nilitarajia tuongee kwa data na sio aina hii ya majibu na swali langu ambalo lilitaka zaidi data na sio mistari miwili ya kebehi. Asante mama umeshinda. Sishangai kwani haya ni aina ya majibu yanayotolewa hata na viongozi wetu walio wengi. Halafu tunabaiki tunashangaa kwanini sisi ni maskini. Hongera mama.
 

Wewe ulete swali linalotaka data wakati wewe mwenyewe umekuja na maneno matupu? Unanchekesha.
 
Maendeleo hayaletwi na chama cha siasa bali juhudi binafsi na kujituma. Jiulize utaifanyia nini Tanzania na sio Tanzania ikufanyie nini.Zinduka.

kodi wanazokusanya ni za kazi gani?
 
Wewe ulete swali linalotaka data wakati wewe mwenyewe umekuja na maneno matupu? Unanchekesha.

kumbe kujenga barabara nk ni hisani sio wajibu?kwahyo hizi kodi tunalipa kwa ajili ya MAFISADI tuu?kwahyo wasipoleta maendeleo tusihoji kwakua sio wajibu ni hisani tu? we natamani hata nione sura yako maana nahisi ubongo wako umeoza kama wa nape.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…