Kwa hiyo ukisusa wewe kwa kuwa ni wachache basi walio wengi wasiendelee na shughuli zao? wewe punguani kweli kweli.
Kwa bahati mbaya na wewe niliyekutegemea umeangukia kwenye udhaifu uleule wa wanaccm wote. Kujibu maswali na kujenga hoja imekuwa ni tatizo kubwa na matokeo yake ndio hapo jeshi la polisi kutumika kupiga watanzania wenye mtazamo tofauti na ccm. Hukuwa na haja ya kutukana na tena kutukana kwenyewe bora ungejenga hoja wangalau kidogo wa utetezi wa baadhi ya maswali yenye utata. Na kwa bahati mbaya sio wewe, rais, au mjumbe yoyote wa BMK kasoro wa kura za hapana anayejenga hoja kwenye maeneo hayo yenye maswali lukuki. Haya mama kwa jinsi ulivyoitetea katiba pendekezwa nimeamini ni nzuri sana.
Mtazamo wako ulio tofauti unatazamwa lakini hautekelezwi kwa kuwa katika demokrasia ni; wengi wape wachache wasikilize. Na naam Kikwete amekuwa msikivu sana, au hukumbuki vyama vya upinzani vya wachache vinapokaribishwa Ikulu kusikilizwa? nikupe ushahidi?
Kwako wewe katiba nzuri eti mpaka iwe na serikali tatu ukawa ujuha huu sijui mtafika nao wapi.
Ndugu wana-jf,ninajiuliza maana ya kauli hizi za viongozi wa ccm ikiongozwa na Rais,pale aliposema"KATIBA HII NI NZURI WANANCHI MUIPIGIE KURA YA NDIO".hii inatoa tafsiri gani?
Nijuavyo mimi katiba pendekezwa inatakiwa iletwe kwa Wananchi,kila mmoja apewe nakala yake na apate muda wa kisoma ili aweze kutoa maamuzi sahihi. Sasa nawauliza viongozi wa CCM mnaopanda majukwaani na kuipigia debe katiba pendekezwa; mnadhani mnafanya sahihi wakati bado hata wananchi hawajaisoma? Swali linakuja; Kwani mnawasiwasi gani mpaka mnaanza kuipigia debe katiba hiyo ikiwa kama imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi?
Nawaombeni sana,Tanzania ya mwaka 1977 sio Tanzania ya leo!mmezoea kudanganyadanganya umma bila kutumia akili sasa mnaishia kubaya! Tumieni japo akili ili muendelee kijenga heshima ya Taifa letu kwani Tanzania si ya Chama chochote bali ni ya Watanzania.
Wale wanaowataka wananchi waipigie kura ya HAPANA hiyo katiba wanaeleza mapungufu yake ambayo hayana shaka hata kidogo kuyaelewa. Hivi kama katiba pendekezwa imetaja 50% kwa 50%,umilikaji wa ardhi kwa wanawake,haki za wakulima,wasanii,vyombo vya habari nk lakini wakaweka katazo la kudai au kuhoji haki hizo mahakamani au katika chombo chochote cha sheria,hiyo ni haki? Au kwako kumzuia mtu kikatiba kudai haki yake huo ndio UZALENDO? Bado safari ni ndefu.Kwanza waulize viongozi wako wanaojiita ukawa wana maana gani kuwaambia wananchi wapige kura ya hapana ndio utaelewa kwa nini na sisi tunawaambia wananchi wapige kura ya ndiyo.... Hao wanaowaambia muikatae wamewaletea mkaisoma???? sasa kimuhemuhe cha nini kwa nini usiwe na saburi ukasubiri ukaipata ukajisomea halafu ndio ukaamua uchukue ya ukawa au uchukue ya wazalendo waliokuandikia na kukuingizia yale yote ambayo kijana au mzee wa leo anayahitaji na sio serikali tatu kama wanavyong'ang'ania
Umeshajiuliza na UKAWA kwanini wanasema katiba hii si nzuri na kuwaambia wananchi wapige kura ya hapana?
Yaani kweli mnajiaibisha hamna cha kutetea kwenye katiba kwa hoja dhidi ya jazba na kejeli. Ndio maana mnasema watu wasisomewe waelewe wenyewe lakini nyinyi mnataja vifungu kama haki za wakulima, wafugaji, wasanii nk, kama gia ya kuwachanganya wananchi wenye uelewa mdogo. Nilitarajia ungetoa ufafanuzi wa hizo haki na wapi katiba pendekezwa inataja wataweza kuzidai. Halafu sio wewe tu ambaye umepewa jukumu humu jamvini kutetea hiyo aibu bali hata hao wajumbe wa BMk hawajitokezi kutoa ufafanuzi wa haya maswali, bali wamebaki kusema katiba ni nzuri sana imewalenga wananch, na udhaifu huu wa kuitetea hii aibu na hila ya ccm uko kwenu wote kuanzia Rais, wajumbe wote wa Bmk kasoro wa kura za hapana hawatoi ufafanuzi wa vifungu hivi mnavyoita vizuri. Sasa kama ni vizuri na hamuwezi kuvitolea ufafanuzi je hivyo vibaya itakuwaje. Andaeni jeshi kupiga watz kupitisha huu upuuzi maana hautapita kwa utashi wa wananchi.
Hakuna ambae hiyo title ya Umarehemu ataiepuka.
Kama huna hoja katika mambo mengine, nakushauri uwe msomaji badala ya kuandika utumbo.
Wale wanaowataka wananchi waipigie kura ya HAPANA hiyo katiba wanaeleza mapungufu yake ambayo hayana shaka hata kidogo kuyaelewa. Hivi kama katiba pendekezwa imetaja 50% kwa 50%,umilikaji wa ardhi kwa wanawake,haki za wakulima,wasanii,vyombo vya habari nk lakini wakaweka katazo la kudai au kuhoji haki hizo mahakamani au katika chombo chochote cha sheria,hiyo ni haki? Au kwako kumzuia mtu kikatiba kudai haki yake huo ndio UZALENDO? Bado safari ni ndefu.
Faiza hoja yangu ni kuwa ilikuwaje marehemu akapiga kura? utumbo ni marehemu kupiga kura au mimi kuhoji, hebu nifafanulie wewe mwenye hoja.
Wewe ulikuwepo wakati amrehemu akipiga kura?? au ni yale mnayoyadaka tu kutoka vinywani mwa lissuslaa? Huwezi mdanganya hata mtoto wa chekechea kuwa marehemu alipiga kura na ikahesabiwa....fungua tovuti ya BMK na utaona kura zote zilivyopigwa na hapo utatuambia marehemu ni nani kati ya hao waliopiga kura
Na yule wa Zenji ambaye hakupiga kura lakini jina lake likawemo kwenye orodha unaliteteaje? we tuyaache ndugu...
Faiza hoja yangu ni kuwa ilikuwaje marehemu akapiga kura? utumbo ni marehemu kupiga kura au mimi kuhoji, hebu nifafanulie wewe mwenye hoja.
Marehemu wengi sana wameshapiga kura walipokuwa hai na kura zao huhesabiwa hata kama wamekufa/
Unafikiri wapiga kura wote wa Tanzania wanakuwa hai zinapohesabiwa kura, hakuna anaekufa? fikiri!