CCM mnapoendelea kuwapokea wapinzani msisahau maendeleo

CCM mnapoendelea kuwapokea wapinzani msisahau maendeleo

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,019
Reaction score
4,695
Nawakumbusha wana CCM na watanzania kwa ujumla...kasi mliyonayo ya kuwapokea wapinzani msisasahau maendeleo ya nchi na watu wake.

Kama taifa litaendelea kuwa masikini kama ilivyo sasa sasa. Kipato cha mtu mmoja mmoja kikiendelea kushuka kama ilivyo sasa huduma za kijamii hasa maji, elimu na afya visipo boreshwa ninawahakikishia kuna wakati mtakuwa katika wakati mgumu kama chama na mtu mmoja mmoja kama kiongozi wa chama au serikali.

Kama mtaweza kutimiza hayo yote ila mkisahau umuhimu wa utawala bora na demokrasia hata kama nchi itakuwa na maendeleo kiasi gani basi msahau amani na utengamavu wa kitaifa.

Nina mfano mdogo hasa katika swala la elimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hakuna kipindi ambacho serikali na CCM imechukiwa kama kipindi cha mwaka jana na mwaka huu kwa wanafunzi wengi kukosa mikopo.

Nimeshuhudia wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya juu wakishindwa kwa sababu ya kukosa mikopo.

Yaani inafikia hatua mwanafunzi anafungasha virago vyake anawaacha wenzake wanaendelea na masomo kisa kakosa mkopo na wengine waliweza kumudu kusoma wanasoma kwa taabu sana.

Kwa swala la mikopo serikali na CCM mmeongeza hasira kubwa kwa kundi hili la kijamii kuna vijana wengi na wazazi walikuwa mashabiki wazuri wa CCM ila ukiwauliza leo wanaweza kukutukana hawataki tena kuisikia.

Pili, ugumu wa biashara hili silizungumzii sana mnaona wenyewe mtaani maduka mengi yamefungwa na kampuni nyingi zimefungwa nadhani chuki ya wale waliokuwa wanategemea biashara sasa inaongezeka juu yenu.

Tatu, ajira hakuna vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo wako mtaani, wengi waliosoma fani ya uwalimu uwe wa sanaa au sayansi wakitegemea ajira ya moja kwa moja wanalia kilio kikuu inafikia hatua shule binafsi zinawaajiri kwa ujira mdogo wengine wakiishia kujitolea na kupewa hela ya chakula, maisha yao ni magumu mno kilio hiki nacho mtakijibu.

Wafanyakazi kada hii siizungumzii kwa sasa ina hali ngumu. Maisha yanakuwa magumu mishahara ile ile mazingira ya kazi hayaboreshwi.

Nawakumbusha mnapojaribu kuua upinzani wa vyama msisahau haya mambo muhimu, siku haya makundi yakilipuka sumu yake haitakuwa sawa na Lissu au Mbowe wakisimama jukwaani na kuisema serikali nchi itakuwa na chama kimoja ila ndipo kila mwenye tatizo atawafata nyie msipotatua matatizo yao ndio mtajua.
 
Nchi haina kiongozi visionary, ina kiongozi boya tu.

Hajielewi wala hajitambui wala hajijui hata yeye mwenyewe kama ni nani?
 
mkuu bado hatujapata kiongozi mwenye uchungu na taifa letu zaidi ya mbwembwe...
 
Back
Top Bottom