OLESAIDIMU hivi vitu si vya kukurupukaSasa mkuu hao watu wanaominywa si waungane, maana unasema wote wana nguvu na wanapendwa. . . . .ugumu uko wapi??!!!
Bati inapovuja badala ya kusogeza kitanda we unalaumu bati. . . . .Inasaidia nini??!!!
Imekula kwenu!!!Nakubaliana na wewe ndugu,hata huku niliko watu wanasubiri tamko lake tu na wanasononeka sana na ukimya wa Lowassa. Siku Magufuri anatangazwa baadhi walikubaliana na matokeo lakini baada ya siku mbili watu wamebadiri msimamo na kuanza kuhofia mfumo uliopo CCM (SI MAGUFURI, HAWANA TATIZO NA MAGUFURI), wanasema haijawahi kutokea Watanzania walivyoweka imani kwa Kikwete na kumpa ushindi mkubwa,leo hii ni majuto ambayo wanaamini hata Magufuri atapita humo humo hivyo lao ni kuiweka pembeni CCM na Magufuri wao. Niko Geita Nyakumbu.
Imekula kwenu!!!
Magufuli is the president of United Republic of Tanzania for 2015 - 2025!
Mkuu,Mkuu mimi binafsi nilikuwa team Lowasa!
Lkn siwezi nikawa na mapenzi kwa mtu kupitiliza!
Kwasababu CCM haikumpitisha Lowasa, sina sababu ya kutokumsapoti Magufuli!
Na ni team Lowasa wengi tu wenye msimamo kama wangu!
Kamwe Lowasa hawezi kunishawishi niwapigie kura Ukawa hata yeye akijiunga nao!
CCM bado ni imara sana na pia yanayotokea ukawa asaivi ni madhaifu yao wenyewe na CCM has nothing to do with them!!
Ni jambo la ajabu kwamba maCCm hawahawa wanamwita Lowassa fisadi ndio hawahawa walimuita gamba lakini bado ni mwanachama wao..........Hivi Fisi anaweza kukaa na Kondoo kweli? Mbona hawawezi kumfukuza fisadi?mshana Jnr,umeeleza ukweli lakini wengi watakubeza.Lakini kwa uhakika hizo pesa wangenunua madawati au dawa za mahospitali.
Lakini ninachokiona wengi wa wanaCCM hawajui maana ya upinzani wanaona UPINZANI ni uadui,wengi wa wanachama wa CCM hata UTAIFA umewatoka kabisa,wanakumbatia wizi na rushwa imeonekana ni haki.
Sijui tunakoelekea na dhana hii ya pesa kununua madaraka.Watanzania bila kujali itikadi zetu ilibidi tujiulize kwanini watu watumie pesa nyingi kugombea madaraka.
Ninajiuliza kwanini CCM itenge hizo milioni kuwalipa vifungu vya wachache waliopo upinzani ili kuusambaratisha upinzani,kama ni kweli basi ningependa kujua sababu zake.Na kwanini wanaolipwa hizo pesa wasijiulize kwanini wananunuliwa?
Kapige mswaki kwanza.... Maneno yanaonekana mdomo sio mfasi.... Unawaza kama kingunge ww
Ni jambo la ajabu kwamba maCCm hawahawa wanamwita Lowassa fisadi ndio hawahawa walimuita gamba lakini bado ni mwanachama wao..........Hivi Fisi anaweza kukaa na Kondoo kweli? Mbona hawawezi kumfukuza fisadi?
Wote ni mafisi au wote ni kondoo au wote ni Kambale......
Lowassa afanye maamuzi magumu sasa tuone kama CCM itabaki salama, aache kumbwelambwela!
Michango mingi hapa itategemea nani ana mtazamo gani kwenye nini na ni wa kundi la nani, hayo pengine ni matusi ya kawaida sana yapo muhimu tujadili hoja iliyopo mezani
Nakubaliana nawe kwamba ameshindwa kufanya TIMING.....lakini nyuma ya pazia yapo mengi yanayoendelea. Hata ujasiri wa Kingunge kusema hadharani kwamba CC haijachagua tano bora bali imetoka/kulazimishwa na KITENGO ni muendelezo wa kumomonyoka.Bigirita,alikosea toka mwanzo ,angeachia mapema impact yake ingekuwa kubwa ,na si kuhama chama kususia tu ule mkutano mkuu lazima wengine wangeondoka naye na pale ndipo ngoma ilipoishia,kwa sasa anacheza ngoma ya mwenyekigoda.
Pili anajua hatari itakayomfika pindi akiondoka sasa,kukaa kwake kimya ni dawa zaidi kuliko kuongea.Maana hata mwenyekigoda anatamani ajue nini akifikiriacho.
Kwa uhakika Lowassa hawezi kuhama CCM ,sababu ndiko kuliko mlea,ndiko kwenye madogoli yao (yeye na wenzake) wanajuana siri zao wote,yeye ni mshindwa zaidi kuliko aliye madarakani sasa.Wote waliokwenye uongozi CCM kwa sasa wanacheza ngoma ya mwenyekigoda.
Kuna wale waliomback Lowassa hawa wanahatari ya kwenda na maji ndiyo maana kwa sasa Mzee hana marafiki tena,wamemuacha,yuko peke yake akiliwazwa na familia yake.Ameshapoteza vingi,pesa,ubinadamu (UTU) wake,SIFA yake,uungwana wake,marafiki zake ndiyo maana move yoyote atakayochukua lazima awe makini vinginevyo maisha yake yataondoka kama mshumaa uwakao............
Nakubaliana nawe kwamba ameshindwa kufanya TIMING.....lakini nyuma ya pazia yapo mengi yanayoendelea. Hata ujasiri wa Kingunge kusema hadharani kwamba CC haijachagua tano bora bali imetoka/kulazimishwa na KITENGO ni muendelezo wa kumomonyoka.
Lowassa anaweza asitoke CCM, lakini watu wake wachace wanaweza kutoka. Ninaamini ana watu wanaomuamini sana, na wapo wanaompenda kwasababu ya fedha alizonazo (wanapata chenji kidogo).
Kumbuka pia kwamba hawezi kutoka bila mazungumzo na sehemu anayotaka kwenda....yeye hataki kuhama chama akawe mwanachama wa kawaida. Hii ni swala la kulifikiri sana.