CCM mmevuliwa nguo, kubali kuchutama

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
CCM wanajaribu kuficha uchi wao kwa majani ya mti bila kuelewa kuwa jua likiwaka hayo majani yatanyauka na uchi wao utaonekana.

Kosa kubwa sana mlilofanya ni mtindo wa kuendeasha siasa zenu kibabe; mliwanyanyasa washindani wenu kwa kiwango cha hali ya juu mkidhani kuwa Watanzania walikuwa hawayaoni hayo mnayoyafanya.

Mkaendesha nchi hii kwa kuvunja Katiba huku mkidhani wananchi ni vipofu na hawayaoni hayo mnayotenda.

Mkawa na kiburi cha kujiamulia mambo makubwa yanayohusu nchi yetu bila ya kufuata taratibu ambazo zimewekwa kwa mujibu wa Sheria.

Leo nkiambiwa ukweli mnakimbilia kutoa kauli na madai kuwa hizo shutma ni kauli za kichochezi. Hivi mnadhani watanzania wa leo bado hawajui kupambanua kati ya kauli za kweli na za kichochezi? Kubalini tu kuwa umefika wakati sasa mvune faida ya maovu yenu.

Washindani wenu wamewavua nguo msijaribu kuwakimbiza aibu ya uchi wenu itazidi kuonekana. Ni bora nkubali kuchutama ili mambo haya yaishe.
 
Hakika CCM wameanza kuvuna matunda ya maovu yao kwa miaka hii 5 mfululizo

Hivi sasa kila kinalotamkwa la ukweli la upinzani, wao CCM wanalitafsiri kuwa ni matusi au lugha ya uchochezi, ambayo hao wapinzani wametumwa na mabeberu wao!

Badala ya kujibu kwa hoja majukwaani wao CCM wamekuwa wakilitumia Jeshi letu la Polisi kuwatesa kwa kiwango cha juu wapinzani!
 
Hakika CCM wameanza kuvuna matunda ya maovu yao kwa miaka hii 5 mfululizo

Hivi sasa kila kinalotamkwa la ukweli la upinzani, wao CCM wanalitafsiri kuwa ni matusi au lugha ya uchochezi, ambayo hao wapinzani wametumwa na mabeberu wao!

Badala ya kujibu kwa hoja majukwaani wao CCM wamekuwa wakilitumia Jeshi letu la Polisi kuwatesa kwa kiwango cha juu wapinzani!
Kwa miaka mitano kila kilichofanyika serikalini kilikuwa ni amri kutoka kwa Rais, hakuna aliyekuwa na maamuzi zaidi ya Mheshimiwa Rais Dr JPM.

Kwa ushuhuda watendaji wote lazima waanze kwa kauli ya imani “tunamshukuru Rais Dr JPM”.
 
Kila Mwana CCM akiongea ni hofu kwa Lissu, sijui hofu ni ya nini hali ccm inamiliki kila kitu kuanzia viongozi wa dini,wasanii,polisi,nk still haijiamini iinawatuma kina sabaya wakawapige mawe wapinzani na kuchoma ofisi zao,kuzia vyombo binafsi visipwe nafasi.

Walikuwa biz e5 yrs kupambana na mbowe wakidhani ndio shida ya watz.Milioni 50 wamejengea chato international ya kutua ndege moja tu,leo hawana jipya la kuatuambia zaid ya mabeberu,flyover,sgr,
 
Watumishi wa umma ndo wameongoza kuishi maisha magumu kwenye awamu hii kwani tangu 2016 uhakiki wa vyeti uliendelea bila kukoma. Yaani kila siku wakikuwa wanalazimika kuzungusha vyeti vyao maofisini.

Achilia mbali hilo la kusumbuliwa kwa uhakiki usioisha, hakuna mtumishi aliyepata nyongeza ya mshahara kwa miaka mitano wala kupanda cheo, kisa, ujenzi wa madaraja.

Huyu rais hana utu hafai kabisa kuongoza nchi kwa awamu nyingine. Watanzania tusikubali kumchagua tena kwani tutakuwa tumejimaliza wenyewe.
 
Yaani Rais wa nchi anasimama hadharani huku anatafuta Mhindi kishamba anamwambia mama wa kitanzania eti "unataka upanuliwe wapi? " anarudia zaidi ya mara tatu maneno ya aibu na udharirishaji hayo!!

Ndio na akili zangu timamu nikampigie kura kiongozi wa hovyo namna hiyo?
Aisee ni aibu sana mkuu,sikuamini kwamba maneno yale yametoka kwake
 
Hakuna mtumishi wa umma wala mfanyabiashara atamchagua huyi mhutu wenu ambaye amekithiri kwa udhalimu.

Tunakwenda na Lissu awamu hii, hupendi, kunywa sumu ufe.
watumishi wa uma binafsi na serikalini hawazidi 2.5ml. wafanya biashara wenye hasira nchi hii hawazidi 2.5ml.

kati yao hapo wote hatujajua wasioa na kadi ni wangapi? wafuasi wa pole pole, ACT, CUF ni wangapi?

Mtaji wa cdm ni vijana wa chuo wasio na ajira, waliokosa mikopo, walifukuzwa kwa vyeti feki, waliovunjiwa nyumba kimara nk. wekezeni nguvu huko ndio kuna uhakika.

Sasa bahati mbaya mgombea wenu anamparua Magufuli na kuacha kuwaandaa wapiga kula ni nini amewaandalia endapo atashinda. akidhani kila mtu anajua yeye alivuliwa ubunge na ndugai amuonee huruma.

Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app
 
Unapomuona mtu anayekutuhumu kwa maovu uliyonayo, bila kuangalia mazuri uliyonayo, hali ya kuwa yeye anajiona hana maovu ni dhahiri mtu huyo anachokitafuta ni faida binafsi
 
Back
Top Bottom