NyaniMzee
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 396
- 727
Jamani watanzania wenzangu. Kama kuna jambo linatia uchungu ni kuona Tanzania niijuayo ambayo miaka ya 70's na 80's ilikuwa inasomesha watoto bure kuanzia Shule ya msingi hadi Chuo Kikuu; Tanzania ambayo huduma za afya zilikuwa bure na bora.
Tanzania ambayo ungeweza kujipangia usome nini ili ufanye kazi gani; Tanzania ambayo viongozi wa kisiasa walikuwa wanapigwa msasa huko cha Kivukoni Idelogical College na walielewa maana ya kuwa kiongozi wa kisiasa.
Tanzania ambayo tulikuwa tunatumia product za viwanda vyetu, kumbukeni kiwanda cha Bora Shoes, Sungura Textiles, Kilitex, na vingine vingi tu.
Tanzania ambayo kulikuwa na miiko ya uongozi na kulikuwa na Tume ya Maadili ya Viongozi; Tanzania ambayo wanafunzi wakifunga shule wanapewa "go and return" ticket kwenda makwao na bado wanapewa mkate, siagi na karanga za kula njiani; Tanzania ambayo hatukuwa na matabaka wala kudharauliana bali tulijivunia kuwa wazalendo kwa kuitumikia nchi kwa uadilifu.
Nikikumbuka hayo yote na mengine ambayo sijaweza kuandika na kulinganisha na Tanzania hii ya awamu hii ambayo tumefikia kutukanwa na viongozi tuliowachangua; tunatozwa kodi hadi kwenye vocha; tuna viongozi wasiosoma; wenye viburi vya kutisha ; wasiogopa Mungu; wasiojua wanapeleka nchi wapi; wanaotumia madaraka vibaya; wanaotutukana na mengine mengi tunayoyashuhudia huwa naishia kusema poleni sana wajukuu wetu,watoto wetu na kizazi hiki kwa vile hii sio nchi tena.
Ni kati ya nchi tatu duniani ambako hakuna raha. Afadhani ya Yemen! yote haya tumeponzwa na waliotuchagulia na wakalazimisha utawala uliopo. Wanajulikana!