CCM mkoa wa Lindi yakanusha wanachama wake kurudisha kadi na kujivua uanachama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Barnabas Essau amesema hakuna mwanachama yoyote wa chama hicho aliyerudisha kadi kama ilivyoripotiwa na ITV jana.

Mzee Essau amesema kadi zilizooneshwa jana walikuwa nazo makatibu wa Matawi wa CCM ambao hawajulikani walizitoa wapi na uchunguzi rasmi juu ya swala hilo umeanza na vikao husika vya chama vitatolea taarifa.

Source: ITV habari
 
21 December 2021
Njinjo, Kilwa
Lindi Tanzania

Wananchi wakata Tamaa Ahadi za CCM, Waamua kurejesha kadi za uanachama

Mamia warudisha Kadi za za CCM Kilwa Njinjo mkoani Lindi. Na viongozi wa CCM wakiri kuzipokea huku kuna taarifa kadi nyingi zaidi zitarejeshwa ...




Habari zaidi zinasema kuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilwa Bi. Mayasa Kimbau akihojiwa juu ya dhahama hiyo ya kisiasa asema pamoja ya kuwa Kilwa ina idadi ya wanachama wengi, chama hakiwezi kupuuza madai ya wanachama hao waliorudisha kadi hivyo watalifuatilia jambo hilo ili kuona kero zilizopelekea kurudishwa kwa mamia ya kadi za uanachama zinatatuliwa badala ya kuwakejeli kuwa waliorudisha ni wanachama wachache tu.

Bi. Mayasa Kimbau mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilwa awaomba radhi wanachama wa CCM Kilwa na kuanza kuhakikisha kero zinapatiwa ufumbuzi wa haraka na pia chama kutumia ushawishi kuwaomba wasirudishe kadi kwani changamoto zitapatiwa ufumbuzi, amemalizia taarifa yake mwenyekiti huyo CCM wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Tanzania.
Source : Mashujaa TV
 
Masasi, Tanzania

17 December 2021

CCM wilaya ya Masasi yavunja "ma-group" yake ya WhatsApp, Yadaiwa kutumika vibaya



CHAMA Cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Masasi kupitia kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo tarehe 12 December 2021 imetoa tamko la kuwataka wanachama wake wote ambao wanatumia makundi ya WhatsApp ambayo yamesajiliwa kwa kutumia jina la Chama hicho la CCM au jumuiya za CCM kwenye makundi ya mitandao hiyo kuvunja mara moja makundi hayo na kuyasajili upya kwa kutumia majina mengine badala ya CCM.

Tamko hilo limetolewa na katibu wa itikadi na uenezi CCM Wilaya ya Masasi kwa niaba ya Chama hicho Twahil Mayola alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kwa lengo la kutoa tamko hilo.

Aidha,Mayola amesema tamko hilo limekuja baada ya kamati ya siasa Wilaya kuketi hivi karibu kupitia kikao chake na kubaini kuwa makundi yote ambayo yenye nembo ya CCM ambayo wanachama wanayatumia wapo baadhi ya wanachama wanayatumia vibaya ikiwemo kuwachafua viongozi wa Chama na serikali hivyo kutia doa Chama na serikali.

Twahil Mayola amesema kuwa kufuatia agizo hilo mwanachama yoyote ambaye atakaidi agizo hilo na kukutwa bado akitumia mitandao hiyo kwa jina la CCM au jumuiya zake atachukuliwa hatua.

Source : Masasi One Online TV
 
Back
Top Bottom