seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Wanabodi, Siasa ni hoja,Mtindo wa ccm kujadili mtu badala ya hoja haitawasaidia ,Hoja za kujadili zipo nyingi sana zilizosababisha maisha ya watu kuwa ya hovyo na magumu
Takwimu za ugonjwa wa corona ni mwana ccm gani mwenye uwezo wa kuhoji mwenendo na hali halisi ya corona Tanzania bila hofu wala kuogopa? au wengi ni kama maisha ya konokono anatoa kichwa nje akiona hatari kichwa anaficha ndani
Leo hii ukiruhusu dodoso kuhoji watu kuhusu maisha utashangaa sana,Hao wanyonge wafanyabiashara ,wakulima na wafanyakazi ni kilio kila kona ya nchi
CCM hakuna anayejua matumizi ya pesa ya hiki chama,Uchaguzi wa mwaka 2005 Rais mstaafu wa awamu ya tatu amekiri kwenye kitabu chake kuwa pesa za EPA zilitumika kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 wa ccm,Je hizi pesa ccm wamerudisha kwa wananchi wanyonge?
Je, Mamlaka kuu tatu yaani serikali,Bunge na Mahakama zinaheshimiana na zipo huru,Kama zinaheshimiana kwanini katiba na sheria zinavunjwa hapa kuna mifano mingi sana,Spika kulazimisha mtu aliyeacha ubunge kurudi bungeni,Serikali kuiamrisha bunge kutolipa pesa halali kwa wabunge
Je, Wafanyakazi tangu 2015 mishahara yao imebadilika huku gharama za maisha na mahitaji zikiongezeka
Je, Wafanyabiashara wanafanya biashara kwa uhuru bila kuporwa mali zao na TRA, Hizi kejeli kwa wafanyabiashara kubambikiwa kodi nani anazijibu
Je, Kuna kiongozi yeyote wa kitaifa anamsomesha mtoto wake kwenye shule za msingi zisizo na umeme ,internet,maji na madawati ,Hizi shule mbovu ndio zinaitwa za wanyonge
Je, Matumizi ya kununua baadhi ya mazao kama korosho au kununua ndege yalipitishwa na Bunge
Je, Ofisi za CCM mikoani na viwanja vya mpira vilivyojengwa na wananchi wakati wa chama kimoja mfano uwanja wa Majimaji Songea ,Kodi mnazokusanya kwenye majengo na viwanja hivyo vya uma mnazipeleka kwa wananchi au mmegeuza ni mali za chama
Je, Tangu mwaka 2015 mpaka leo vijana wanaomaliza chuo na vyuo ni wangapi mmewatengenezea ajira au ndio kauli za kuwaambia mtajijua wenyewe bila mitaji au mikopo
Je, Kwanini watu waliokijenga chama kwa jasho na damu wakati wa shida na taabu hawapewei nafasi ya uongozi bali mamluki wanaojenga hoja siku moja bungeni ya kusifu si zaidi ya dakika 10 wanakabidhiwa mamlaka makubwa
Je, Kitendo cha wabunge wa ccm bungeni kuanza kwa kusifia mamlaka halafu mwishoni kuanza kulalamika kuwa huduma hakuna majimboni huu sio unafiki na kuwafanya Raia wapumbavu
CCM ikijibu hizi hoja nipo tayari kujiunga rasmi na chama hiki,Lakini kitendo cha kumjadili mtu badala ya hoja mezani hazitawasaidia kitu ,Maisha ya hao wanyonge yalishakuwa magumu na ya hovyo,Mna kazi kubwa kushawishi watu