CCM, misifa kwa Kikwete na deni la taifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, misifa kwa Kikwete na deni la taifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theHAVARD_product, Sep 21, 2012.

 1. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Wana JF nimekuja hapa tena baada kusikitishwa na Jinsi Nyerere na Ukiachilia mbali wailomtangulia wanavyobezwa katika Majukwaa ya 'Kisiasa' ya Serikali hii katika kuzindua Miradi ya TAIFA ! Iwe katika Barabara,Hospitali au pengine pale! Ni MISIFAAAAA tuuuuuu! kana kwamba R.I.P Nyerere hakufanya chochote... Leo ntagusia katika BARABARA,si mara MOJA au MBILI,"BINGWA" wa takwimu Magufuli amekuwa akirudia sentesi ya KM ZAIDI ya 15000 za barabara ya LAMI akilinganisha na zile zilizokuwapo kipindi cha MWALIMU! Kana kwamba hajui SERIKALI hiihii ndio imesababisha deni la TAIFA kufika TIRIONI 24(kwa kukopa)! Nadhani hii ni kebehi kubwa SANA,SANA kwa Hayati Nyerere,kuonesha kwamba hakufanya chochote! Alirudia kutamka tena Majuzi pale JANGWANI! Ngoja niHOJI,
  1)Je ,Si ndo serikali ya KIKWETE ambayo imetia aibu kwa Deni la Taifa kufika TIRIONI 24?!!

  2)Na Ndio SERIKALI ya Tanzania OMBAOMBA kuliko zoote??!!

  3)JE,WANATAKA KUJISIFU na 'VIMIRADI' uchwara vya BaraBara ambavyo vinaongeza Deni la TAIFA kila SIKU?

  4)MAGUFULI anajua KIKWETE Alikuta Deni la Taifa Sh.Ngp?!

  5)CCM wanaweza kutueleza Katika MIRADI ya BARABARA ipi imechangiwa na DENI la TAIFA na KODI za Wananchi??!!
  NINGESIFU sana MIRADI ya KIKWETE kama DENI la TAIFA lingebaki palepale alipoachiwa na
  MKAPA,,Ningemsifu pia kwa hizo zinzoitwa 'KM 15000 ZA KIKWETE'.
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapa kijijini kwetu jamaa mmoja alikuwa na nyumba yake ndogo ya vyumba kama vinne matofali ya kuchoma na imeezekwa kwa mabati. Aliijenga kutokana na akiba yake aliyoipata kutokana na kuuza kahawa, maziwa ya ng'ombe wake wanaokaribia 40 hivi na shamba la migomba kama heka sita hivi. Watoto wake wanaweza kwenda sekondari kwa vitega uchumi vyake hivi pia.

  Sasa katokea jamaa mmoja akaamua kumzidi kimaisha na kwenda kuchukua mkopo wa million kadhaa benki ili ajenge ghorofa. Hilo ghorofa ni miaka zaidi ya kumi na tano sasa lakini halieleweki kama limeisha au halijaisha na huyu jamaa kuonekana kwake ni nadra maana watu wa benki wanamsaka usiku na mchana ili awalipe mkopo wake!

  Sina uhakika kama hii hali ya hawa mabwana wawili unaweza kuifananisha na kinachoendelea hivi sasa hapa Tanzania!
   
 3. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nanukuu:
  .... hata katika mambo ya hovyo uongozi uliopo madarakani ni dhaifu.
  Haipandi akilini kuwa na fikra na dhamira ya kujenga JIJI linalopendeza hata kuzidi New York wakati wananchi wako hawana access na elimu bora, afya, makazi bora miundo mbinu ya uhakika na services nyingine muhimu na katika viwango stahiki. Sina nia ya kurudia rudia matatizo lukuki tuliyo nayo na ambayo yanahitaji ufumbuzi na utekelezwaji. Tulishaonywa na Mwalimu (RIP) kuhusu upendeleo wa maendeleo ya VITU badala ya umuhimu (priority) kwenye maendeleo ya WATU kwanza. Tunlijua hilo. Leo hii vilaza walioteka chama cha wakulima na Wafanyakazi wa nchi hii wamevimbiwa kabisa na ulafi, wizi n.k kiasi ambacho na akili zao kama zimevia vile. Wale wale walotoka kule kijijini ambako bado ni taabu mno kuliko mika ya sitini weshajisahau kabisa. Utafikiri hawakuzaliwa huko. Inasikitisha mno.
   
 4. theHAVARD_product

  theHAVARD_product JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 292
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  kidogo inaleta picha,Nadhani ni Muhimu kuishi vizuri pasipo na DENI,kuliko PARADISO yenye MSONGO wa MAWAZO! Nyerere alisimamia MAADILI
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red, nimeipenda sana na nilimuona kwenye tv akitamka mwenyewe na asijesema wamemsingizia au mameedit picha!!!
  Yaana pamoja na kutembe kote kweli jk hajui kuwa kote kwenye maendeleo au umasikini vinasababishwa au kuwa sustained na wakaaji wa eneo husika!??
  Ukisema New York kuna watu wanaitwa 'new yorkers', London kuna 'Londoners' nk na huko hutegemei kuwa unapita mitaani na kukutana na kibao au tangazo linalosema "USIKOJOE HAPA". Wale wamewekeza kwenye akili za watu wao then wakafanya mabadiliko ya mazingira na maisha na sio kuwa waliwekeza kwenye Vitu na mazingira then vika-transform watu!
  Hawa wabongo na wamatumbi ninaowafahamu mimi wanaweza kweli kuishi kwenye mazingira kama ya hiyo 'New York' yake aliyotuahidi!??? ...labda atwambie inatumia miaka mia mbili na ngapi kufikia huko!
  Kweli nchi imejaliwa vitu lakini imekosa watu!

   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Kikwete na CCM yake hawana lolote,hawana vision ya namna ya kutengeneza barabara zetu zikatumika hata kwa miaka mia tano ijayo
  Nilipokuja hapa mjini kujiunga na chuo nilishuhudia Mwinyi akizindua Morogoro road na new bagamoyo road chni ya miaka 25 tayari Mkapa amezindua barabara hizo hizo tayari kikwete amezindua barabara hizohizo huo ni unde wazimu tena kikwete barabara moja anazindua mara mbili pande tofauti anazindua kaskazini na kusini mwa barabara hiyo hiyo huu ni upuzi na matumizi mabovu ya fedha za walipa kodi inaudhi sana
  inahitajika masterplan na tutakapofanya mapinduzi ya upanuzi wa barabara za jiji la Dar es Salaam tufanye kweli lakini leo barabara ya morogoro itapoteza uhalali wa kudumu kwa sababu hakuna namna maji yatakavyotolewa pindi mvua zikinyesha,hakuna mahala utaweka mti au nyasi za kuhimili mmomnyoko wa ardhi pembeni mwa barabara hawa CCM na mainjia wetu wote wana vichwa vya kuku
   
 7. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ni kweli viongozi wetu wanabank sana kwenye maendeleo ya vitu kana kwamba ndio itakuwa suluhisho la matatizo ya mwananchi wa kawaida,nilishtuka pale aliposema kwamba mji huo mpya utatumika kama kivutio cha watalii sina hakika kama hawa wazungu wanapokuja Africa hususani bongo wanatalajia kitu zaidi ya walivyoviacha kwao wanachotarajia ni kuona vitu ambavyo ni tafauti au havipo kabisa kwao mathalani mbuga zetu za wanyama na wanyama walioko humo mbugani,hali yetu ya hewa,fukwe zetu majengo yetu ya kale,leo hii tuko busy tukibomoa majengo ya kale tukijaribu kuigeuza miji yetu na sky scrappers kama za British Columbia bila kuwa na mikakati ya kutunza historia ya majengo yetu ya kale.
   
 8. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama ulishawahi kumsikiliza John Perkins kuhusu Econonic Hitman basi utajua nini kinaendelea kati ya Tanzania na wale wanoitwa watoa misaada katika nchi lakini waibaji wazuri wa rasimali zetu kama dhahabu n.k.
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mji wa Kisasa wa Kigamboni......

  wataletwa wageni au ni hao hao wa Waswahili wetu ? Mji wa kisasa watu wajinga, wachovu, wagonjwa chini ya serikali legelege ..HUO utakuwa mji kweli wa kulinganishwa na NEW York? he heeeeeeeee. Yale yale ya mipasho
   
 10. controler

  controler JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 1,537
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe jamaa ulishawahi Kuwa mwalimu? Kama bado Tafadhali fanya mpango japo mwaka mmoja tu ufanye hiyo kazi kwa manufaa ya watu kama Zomba,Ritz,Rejao, Na watu wa Sampuli hiyo.
   
 11. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sio hivyo mkuu bali so many years of depression have rewarded us a vision!
   
 12. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  uko sawa kabisa daraja la kigamboni la nini muda huu ambapo idadi kubwa ya watanzania hawana maji ,elimu bora ,umeme , barabara. bei ndogo ya pamba, maisha magumu faida ninini ya daraja la mamilioni wakati walimu na madhawana mishahara mizuri au na hizo wamekopo kuongeza deni la taifa. hakika Nyerere ni kiongozi bora sana
   
 13. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Haya ni matokeo ya kuwachagua viongozi vilaza wanaofikiria kuhusu maendeleo ya vitu badala ya maendeleo ya watu!
   
 14. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Kweli JF kiboko - umenipasua mbavu!!!!
  Pamoja ni kunipasua mbavu, unachosema ni kweli.
  Hapa tunazungumzia falsafa mbili tofauti za maendeleo. Nyerere aliamini maendeleo ni kuboresha maisha ya kila mwananchi, iwe kijijini au mjini. Lakini kwa vile alitambua kuwa asilimia kubwa ya wananchi iko vijijini na ndio waliokuwa na maisha duni sana enzi hizo, akaelekeza nguvu kubwa huko. Ndio chanzo cha kubuni mfumo wa ujamaa na kujitegemea, maendeleo vijijini, elimu ya kujitegemea, na hata kujiwa na wazo la kuamishia serikali Dodoma.
  Hawa wagagagigikoko waliofuatia falsafa yao ni kupendezesha Dar es salaam, na si miji. Afadhali kama wangekuwa wanazungumzia maendeleao mijini. La hasha. Haishangazi unakuta nusu ya mijadala bungeni inazungumzia oh mara foleni za magari Dar, mara oh mgao wa umeme Dar, mara oh kutapeliana viwanja Dar, oh msongamano wa magari Dar ni ushahidi kuwa uchumi umekua, nk. Kwa ufinyu wao wa akili ni kwamba kila kitu kikienda vyema Dar basi nchi imeendelea!! Kwa bahati mbaya hata mipango ya kuboresha Dar nayo ni ya kigagagigikoko kama mdau ulivyobainisha. Inasikitisha sana.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,307
  Trophy Points: 280
  "Wachekeshaji wa mfalme wao wanawajibika kwa mfalme, kumsifia, kuremba kupiga vijembe, kuwa vibaraka, kujipendekeza, kumpamba, lakini kubwa zaidi ni kumchekesha mfalme hata kama amefanya mabaya,"
   
Loading...