Elections 2010 CCM Maswa watuhumiana, wapeana uhamisho (source Nipashe)

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
743
44
BAADA ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Chadema imeibuka kidedea kwa nafasi za ubunge katika majimbo mawili ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi Mkoa wa Shinyanga ,viongozi wa CCM wilayani humo wameanza kutimuana kwa madai kuwa wamekisaliti chama hicho.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa CCM wilayani humo, zilisema kuwa tayari Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Maswa,Nuru Mselemo ametimuliwa kwa madai ya kukiunga mkono Chadema wakati wa uchaguzi.

Source Nipashe 5 November2010
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
743
44
Hahahahaahahahaha Baba rudia tena Kauli yako ahahahahahaha
 

Lorah

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
1,193
202
Na kweli Makamba ndo ameiua CCM hasa kipindi cha kura za maoni....
huyu hata kwetu alipita akaweka mijitu yake na kule Dodoma akapitisha mibunge yote darasa la saba.... kisa wamechangia chama...
 

Lalashe

Member
Nov 4, 2010
84
1
Si shinyanga tu na arusha wameanza kutimuana kwenye uongozi kupia kamati zao za siasa ngazi ya kata kisa kukosa ubunge arusha mjini bado itafika ngazi ya taifa na chama kife kabisa
 

silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
743
44
Nawaombea kifo chema CCM byeeeeeeee
Raha ya milele akipe ebwana na mwanga wa milele ukiangazie kipumzike kama KANU kwa amani aaameeen Byeeeeeeee Tulikipenda lakini Mungu kakipenda sana Mmmmmm
 

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,740
4,995
Nawaombea kifo chema CCM byeeeeeeee
Raha ya milele akipe ebwana na mwanga wa milele ukiangazie kipumzike kama KANU kwa amani aaameeen Byeeeeeeee Tulikipenda lakini Mungu kakipenda sana Mmmmmm


we mchungaji wa wapi utwaombeaje kifo alafu wapate raha ya milele wapate machungu ya milele na kupumzika motoni
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,093
3,466
Nawaombea kifo chema CCM byeeeeeeee
Raha ya milele akipe ebwana na mwanga wa milele ukiangazie kipumzike kama KANU kwa amani aaameeen Byeeeeeeee Tulikipenda lakini Mungu kakipenda sana Mmmmmm

Hii reply yako imenikumbusha kitu, kuna jamaa moja yuko kule Mbulu alinidokezea mkasa uliyompata mwana ccm moja aliyekuwa amevaa kofia iliyoandikwa chagua jk, basi kuna mtu alipoona ile kofia kwenye kichwa cha mwenzake aliamua kuiadhibu kofia alimtandika fimbo ya kichwa na kumsababishia jeraha kubwa sana mvaaji akasema mimi sijapigwa ila KOFIA ndiyo iliyoadhibiwa, makubwa hayaaaaaaaaaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom