Nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu,niliandika makala yenye kichwa hiki,nilipowaonyesha baadhi ya rafiki zangu,walinitisha,wakanidharau,wakaniona mwehu,wakaona mtu ninayetaka kuhatarisha maisha yangu ya shule,nikatishika,nikaachana na huo mpango.sijui kwa nini?,labda kwa vile nilikuwa 'form one' au kwa vile nilikuwa mwoga wa siasa. Leo nimepata ujasiri upya,nguvu mpya za kurudia kusema sisiem mfu anayeishi. Muda si mrefu tutamzika. Msiba ambao watakaohudhuria na kulia ni ndugu wa karibu tu. Cha ajabu,hata wale ambao ndugu wa karibu baadhi watacheka sana. Si kwa sababu nyingine,bali tu kwa sababu tu walibanwa,wakashindwa kuhema,wakakosa uhuru na mfumo wa kizandiki,kinafiki,kifisadi,kibinafsi wa marehemu. Najua wengi mtajiuliza kwanini nasema haya,ujasiri nautoa wapi? Kifo cha ccm si cha ghafla,dalili zote za kuonesha kuwa ugonjwa hauna tiba ziko wazi kabisa. Kila daktari wa siasa atakwambia hana uwezo wa kuitibu,ccm itakufa tu. Zama za ccm kushika hatamu zimekwisha,dalili ya kwanza. Kura zimepungua kama mgonjwa wa vvu anavyopungua kilo,ccm imekonda,imekwisha. CCM inapumulia mashine(tume ya uchaguzi). Kambi ya upinzani imepata nguvu bungeni,vigogo wamedondoshwa majimboni. Wameanza kutafunana wenyewe,wanatangaza nafasi ya uspika kwa wote wanaongeza sifa ya ziada ambayo haikutajwa popote kwenye fomu za maombi,kituko! Watu wanakesi mahakamani,mwenyekiti wake anasema ni watu safi,kichekesho kingine. Makamba,anasema wametumia wanasheria wao wamegundua watashinda. Moja kumbe kesi inajulikana hukumu,pili tangu lini sheria ya kuzuia kesi isijadiliwe nje ya mahakama ilifutwa?wanasema uchumi unakua,utemezi wa bajeti unaongezeka,unakuaje? Nilikuwa kusema,hizi shule za kata ndio kaburi la ccm,huwezi amini! Hakuna mwenye uccm hata mmoja anayetoka shule za hizi. Hakuna kinachofundishwa zaidi ya kuichukia ccm. Ndio wana haki,hawawezi wakaipenda kama wanafundishwa fizikia na mwalimu wa uraria.wanamaliza miaka minne hawajui test tube ina rangi gani. Hawajui kama kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na kiti chake.