CCM mambo magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM mambo magumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MawazoMatatu, Feb 11, 2009.

 1. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  TAHADHALI: MTUNDIKO HUU UMETOLEWA KWENYE GAZETI KAMA HAUPENDI MITUNDIKO TOKA MAGAZETINI TAFADHALI ENDELEA NA MITUNDIKO MINGINE!

  MWENENDO wa mambo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unazidi kuwa tete, baada ya makada wa chama hicho kushindwa kuvumiliana na kuanza kushambuliana katika vikao mbali mbali vya chama hicho na katika mikutano ya hadhara.

  Taarifa za karibuni zinazothibitisha kuwepo kwa hali hiyo, iliifikia Tanzania Daima Jumatano kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika Februari 5 katika ukumbi wa Pius Msekwa ulio ndani ya eneo la Bunge mjini Dodoma.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa katika kikao hicho kilichokuwa kikiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mbunge wa Mvomero, Suleiman Sadiq, alimshutumu Mweka Hazina wa CCM, Amos Makala, kuwa anatumia vibaya madaraka yake kwa kufuja mamilioni ya fedha za chama kwa masilahi yake binafsi.

  1.Habari ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa kikao hicho kiliitishwa mahususi kwa ajili ya kuwajadili wabunge wawili wa kambi ya upinzani, Dk. Willbrod Slaa, (CHADEMA) na Hamad Rashid (CUF).

  Wabunge hao ambao ni viongozi wa kambi ya upinzani waliandaliwa ajenda maalumu ya kuwajadili kuhusiana na nia zao za kuwasilisha hoja binafsi zilinazowahusu viongozi wa sasa wa serikali.

  Ilielezwa kuwa, katika kikao hicho, wabunge wa CCM walikuwa wakitafuta msimamo wa pamoja wa namna na kumdhibiti Dk. Slaa atapowasilisha hoja binafsi inayotaka maelezo ya serikali kuhusu hatua ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuingilia mkachato wa utengenezaji wa vitambulisho vya taifa.
  Mbali na Dk. Slaa, kikao hicho pia 2.kilijadili namna ya kumdhibiti kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid, atakapowasilisha hoja yake binafsi ya kutaka rais apunguziwe madaraka.
  Ajenda nyingine, ilikuwa ni 4.kujadili malalamiko kutoka kwa Sadiq kuhusu matumizi makubwa yanayofanywa na mweka hazina wa chama hicho anapokuwa katika safari zake binafsi.
  Mmoja wa wabunge wa CCM aliyekuwa ndani ya kikao hicho alilieleza gazeti hili, kuwa ingawa ajenda muhimu katika kikao hicho zilikuwa mbili, za Dk. Slaa na Hamad Rashid zilifunikwa na ajenda ya matumuzi makubwa ya fedha za chama, ambapo Mbunge Sadiq alionya kuwa iwapo hali hiyo haitakemewa na viongozi wakuu wa chama, yeye atalipeleka kwa wananchi.

  Alisema, baadhi wa wabunge walikuwa wakitoa tuhuma kwa viongozi wa juu wa CCM kutumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya masilahi yao binafsi pasipo kuwataja majina, lakini Sadiq alimtaja moja kwa moja Makala na kutangaza kupambana naye iwapo ataachwa aendelee kuchezea fedha za chama.

  “Aliyechafua upepo ndani ya kikao ni Sadiq, alisimama na kumwambia waziri mkuu kuwa Makala anatumia fedha za chama kwa masilahi yake binafsi, alisema kwa ukali kwamba kundi la wana CCM wanaochukua fedha za chama na kuzitumia kupandikiza watu wa kuwang’oa baadhi ya wabunge katika majimbo wasifikiri kwamba wabunge wanaowaandama hawana fedha.

  “Alimtuhumu moja kwa moja Makala kuwa katumia zaidi ya sh milioni 100 za chama kuendesha kampeni katika jimbo analolishikilia la Mvomero na kuonya kuwa yeye ana pesa nyingi zaidi ya hizo, hivyo atakapoanza kujibu mapigo kwa kumwaga fedha, kiongozi yeyote wa CCM asimuulize, kwa sababu hatarudi nyuma na akisumbuliwa atakihama chama kwa sababu ana uhakika wa kushinda ubunge akiwa katika chama chochote,” alisema mbunge huyo.

  Vyanzo vingine vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa baadhi ya wabunge walieleza wasiwasi wao kuhusu matumizi makubwa ya fedha za chama hicho na kwamba jambo hilo linawatia mashaka wanachama ambao wamekuwa wakiwahoji wanapokuwa majimboni kuwa viongozi wa CCM wanapata wapi mamilioni hayo ya fedha.

  “Wasiwasi wetu wabunge ni wananchi, huko majimboni wanahoji kama CCM si mafisadi, tunatoa wapi mamilioni ambayo baadhi ya viongozi wa chama wanayatumia kupiga kampeni kwenye baadhi ya majimbo wakati hata muda wa kampeni haujafika?

  “Itakuwa ni aibu kubwa kama itagundulika kuwa chama chetu kinahusika na ufisadi wakati hivi sasa tunakanusha, tena kwa nguvu. Ingawa sababu kubwa ni woga wa baadhi ya wabunge kunyang’anywa majimbo yao na mafisadi, lakini ni ukweli viongozi wa chama wanatumia vibaya fedha za chama kwa sababu huwa hazikaguliwi,” kilisema chanzo kingine cha habari hizi.

  Alipoulizwa kuthibitisha kama alitoa kauli hizo katika kikao hicho, Sadiq alijibu kwa ukali: “Wewe umeyajuaje mambo yaliyozungumzwa ndani ya kikao chetu, hayo ni mambo yetu ya ndani na wala hupaswi kabisa kuyajua wewe, nenda kwa hao hao wanaona ajabu mtu kueleza kile alichonacho moyoni kwa lengo la kukijenga chama,” alijibu kwa ukali huku akiondoka.

  Malalamiko ya baadhi ya wabunge wa CCM kuhusu baadhi ya makada wa chama hicho wenye ukwasi wa kutisha kuanza kampeni za uchaguzi mapema huku wengine wakidai wanaandaliwa mkakati wa kuwaangusha katika uchaguzi mkuu yamekuwepo kwa muda sasa.

  Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ni mmoja wa wana CCM waliokwisha kusikika akilalamika kuchezewa mchezo mchafu na watu aliodai kuwa ni wapinzani wake kisiasa ndani ya chama hicho, ambao kwa kutumia utajiri mkubwa wa fedha walizonazo, wamekuwa wakiendesha kampeni chafu dhidi yake, ikiwemo kumuweka mtu atakayempinga katika uchaguzi mkuu ujao.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hii nimeipenda!
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  So what? Murad kumshtaki Makala hakumsaidii anachotakiwa kufanya ni kuwaeleza wananchi wa mvomero miaka minne aliyokaa bungeni kawafanyia nini? that all
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hizo ni siasa za uoga, ina maana kikao hicho kisingeitishwa basi angekaa na dukuduku hilo mpaka afe, na kama alishindwa kuhoji mapema mambo hayo ambayo aliyaona, anawezaje kuwasaidia wapiga kura wake ilimradi hata kuwatembelea haendi,
  huo ni unafiki na uchungu alionao kwamba yeye yuko mbali na kapu la kuchukua chochote
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pengine hii itaonyesha sura halisi ya wanasiasa wa Tanzania na kuacha kuwasakama wanasiasa wa Upinzani kwa kuwaona wroho wa madaraka. Wanasiasa wa Tanzania nh! Waangalie pale wanapokuwa nje ya siasa na jitihada zao za kuingia kwenye madaraka, baadae hali zao zinavyobadilika kwa tajiri kuwa tajiri zaidi na masikini kutajirika, Ukiona mwanasiasa ni masikini basi hajayapata madaraka ndani ya chama akiyapata huusahau umasikini.
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,502
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Kama kungekuwa na utaratibu wa wabunge kutueleza wanachokifanya. Tz ingekuwa mbali. Siasa za Bongo ni longolongo tupu na ulaji kwa wingi!!!!!
   
 7. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  “Alimtuhumu moja kwa moja Makala kuwa katumia zaidi ya sh milioni 100 za chama kuendesha kampeni katika jimbo analolishikilia la Mvomero na kuonya kuwa yeye ana pesa nyingi zaidi ya hizo, hivyo atakapoanza kujibu mapigo kwa kumwaga fedha, kiongozi yeyote wa CCM asimuulize, kwa sababu hatarudi nyuma na akisumbuliwa atakihama chama kwa sababu ana uhakika wa kushinda ubunge akiwa katika chama chochote,” alisema mbunge huyo.

  duh kweli wapiga kura wa tanzania hawana thamani zaidi ya pesa.yaani jamaa anachimba mkwara kuwa ana ukwasi wa kutisha na wakimletea longolongo atahama chama na ana uhakika atashinda vilevile kwa vile ana pesa za kugawa pilau,kanga na vi tshirt!
   
 8. share

  share JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kituko, heshima yako. Sadiq alishapeleka malalamiko yake dhidi ya Makala siku nyingi kwa Halmashauri kuu ya chama. Nadhani bado Halmashauri Kuu ya chama bado haijaketi kujadili hili. Hivyo hakusubiri kikao hicho cha wabunge wa CCM. Ila unazoziita siasa za uoga zinaweza kuwa na uweli kiasi kwa sababu mbili: (1) Sadiq ni kihiyo - ex-form IV ya Forest Hill secondary (failure), hivyo anasita kupokwa ulaji na mtu aliyesoma walau kidogo zaidi yake, na (2) mafisadi wenzake - kina mkapa na sumaye- hawana nguvu tena kwenye chama. Ana wasiwasi kuwa hata huko kwenye Halmashauri Kuu anaweza kutupwa nje. Sidhani kama yeye ni mjumbe CC. Hana wa kumkingia kifua kama ilivyo kawaida ya mambo ndani ya CCM. Hivyo, silaha yake kubwa ni fedha (nyingi) alizonazo. Huyu ni tajiri wa kutupwa. Sasa, anataka kumvunja nguvu mapema Makala ili chama kimmulike na kumpunguzia makala nguvu ya fedha (ya chama) ili yeye sadiq azidi kupeta kwa nguvu ya fedha zake binafsi (za kifisadi).
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ahame Chama kama kweli anaona huko kumekumbatiwa mafisadi.na hawa wabunge wanaotishia kuhama Chama naona si wanasiasa wa kweli ,unajilabu una fedha sasa kama una fedha unalalamika nini ?Mara utahama Chama mara utamwaga kuliko wanazomwaga wao mbunge tukuelewe vipi ?
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Ogwalumapesa, kuna vyama vinavyotumia vikao kutatua matatizo yao. Suleiman Sadiq amefanya vizuri kuongelea dukuduku lake ndani ya kikao halali cha wabunge wa CCM. Hapo ndipo anapoweza kusema kwa uwazi na bila kuletewa majungu. Si umeona mara nyingi wanachama wa CCM wanaokwenda kwa wananchi kusema mambo yanayowakera wanavyokuwa vulnerable kwa attacks za viongozi wa chama? Yeye ameanza hivyo. Natumaini atakwenda pia kwa wapiga kura wake na kuwaeleza kinachotakiwa kuelezwa. Huo ndio ustaarabu.

  Mkuu Kituko, kikao kimeitishwa, kwahiyo suala la kisingeitishwa halipo tena. Kisingeitishwa ingekuwa mbaya. Kimeitishwa, kasema.

  Sina uhakika kama unajua kama anatembelea wapiga kura wake ama lah. Nadhani hilo litaonekana katika uchaguzi ujao. Kama kuna wajibu ambao hajautekeleza, sio suala la mjadala huu. Yeye kaongelea jinsi pesa za CCM zinavyotumika vibaya na hasa zinavyotumika kumbomoa kisiasa. Hawezi kukaa kimya. Hakuna mwanasiasa mahiri atakaeweza kukaa kimya. Ni wajibu wake binafsi kujilinda kisiasa.
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF wakati mwingine arguments zetu zinakuwa ni kama watu wasiojua siasa za Tanzania. Kama kuna mtu anayeweza kueleza mbunge wake amemfanyia nini basi ntafurahi sana, lakini siamini kama mtu huyo yupo. Nina hakika kuwa kuna mamilioni ya watu ambao wamewafanyia mengi wabunge wetu. Ukiangalia kinyang'anyiro cha ubungeutaona kuwa lengo kuu sio kuwapigania wananchi, bali ni kutafuta access ya kuchuma na kuvuna kodi za wananchi. Kwa hiyo wanaopigania ubunge wanajua wanachokifanya. Kama lengo lingekuwa ni kuwaendeleza wananchi basi mbona kungekuwa na maendeleo makubwa sana. Ndio maana Murad anasema atamwaga pesa ili kushinda anaua akimwaa pesa, inarudi within no time.
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Muheshimiwa Murad inaelekea maji yako kwa shingo, na akihama tu ataona kile kilichomtoa kanga manyoya!!
   
 13. t

  tk JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni lazima CCM itende inachohubiri. Hivi sasa muelekeo tunaohubiriwa ni kuwa viongozi wasiingie madarakani kwa fedha za rushwa. Sasa kama viongozi wa juu wa chama wanafedha nyingi namna hiyo wakati kila siku tuaambiwa chama hakina fedha, jee hizo fedha zinatoka wapi?

  Inaonyesha bado chama kinategemea matajiri wachache wenye fedha kuendesha mambo yake. Matokeo yake ndiyo hayo. Kama wanachama wenyewe hawakuyakemea nani ana wajibu wa kufanya hivyo?

  Napendekeza tuhuma zichunguzwe bila kujali kuwa mlalamikaji ni mtu wa Sumaye au Mkapa, ili ukweli ujulikane. Kama ikionekana ni uongo basi mlalamikaji achukuliwe hatua. Kama ni za kweli basi Makala achukuliwe hatua. Hongera Sadiq kwa ujasiri..
   
Loading...