CCM London wanyimwa mwaliko wa mkutano mkuu 2012 kwa kuchokonoa ulaji wa wakubwa CCM

Marekebisho

Member
Sep 21, 2012
15
0
Katika hali tete isiyo aminika ccm london wamenyimwa mwaliko wa kuhudhuria mkutano mkuu wa ccm 2012 dodoma kwa kile kinachosadikiwa kuchokonoa ufisadi wa mradi wa mamilioni uliofanywa na wakubwa wa ccm na ikulu. Mtandao umekamata.

Wakubwa hao walioko kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu; mshauri wa rais ikulu na afisa wa mambo nje wamemzunguka tena rais kikwete bila kujua na kutafuna dola za kimarekani $300,000 wakishirikiana na katibu mkuu mwenezi wa ccm london bwana keti katega anayejulikana kwa ufisadi tanzania na uk na sasa kufukuzwa vibaya na wanaccm wenzake na tayari wameshamshitaki kwenye dola la kuzuia hujuma za uchumi. Inasemekana katega amekua anawatishia wanaccm wenzake kuwa wakubwa hao watammaliza mtu yeyote anaefuatilia jambo hilo.

Habari toka kwa mdau east london zinasema mwaka jana wakati wa kikao cha kamati kuu ya ccm london mwenyekiti wao ccm uingereza bw. Maina owino alidai kuwa ccm uingereza sio jukwaa la walanguzi wa fedha na siasa na hivyo hawezi kukubali kashfa zozote za ufisadi wakati wa uongozi wake. Inasemekana bwana owino alijiandaa kustaafu baada ya kipindi kimoja cha miaka 5 lakini anataka amalize kashfa hii ndipo avue gamba rasmi.

Wakubwa hao inasemekana wamebana mwaliko wa ccm london wakihofia kuwa watamwagia rais kikwete siri zote za kashfa hiyo waliyoanza kuifuatilia mwaka 2010 bila mafanikio na kuamua kuunda tume ya uchunguzi ambayo ilitumwa na mawina owino kwenda mpaka bongo kufuatilia jambo hilo lakini wakagonga mwamba. Wanachama wengi wamekasirishwa na hali hii wakidai ccm kuu wamezidi kula hata vya watoto wadogo na wengi sasa wamekimbilia chadema london kwa hasira..

Inasemekana ccm london imekatiwa mawasiliano yote na ccm dar na hawatakiwi kupata mwanya wa kuwasiliana na jm kikwete hata kidogo wala hakuna mwasiliano ya kiofisi. Inasemekana sasa wakubwa hao wamewaweka kwenye list kali ya kushughulikiwa na kutopata kazi kabisa tanzania wafuatao mwenyekiti wao maina owino, wajumbe wa tume ya uchunguzi kapinga kapinga na sururu, mashamba, sukwa said suka, lilian baronga. Ili kuwaonyeshea wamemnyakua katibu wa zamani susi aliyekuwa ameikimbia ccm london kwa kukata tamaa na kupachikwa kazi ya mshauri maalum wa siasa wa waziri mkuu.

Uchunguzi unaendelea..........
 
Inaoneka unajambo hapo lakini maandiko yako hujayapanga katika hali inayoeleweka hebu iweke vema mkuu ieleweke.
 
Back
Top Bottom