CCM Kwisha!

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Wiki hili tumekuwa bize kupokea wageni kutoka mikoani Kwa ajili ya tukio la harusi Jumamosi ya Kesho, tukiwa Kama vinara wa maandalizi, Jana Jioni tukawatoa wazee wetu kuwapeleka pahala wabadilishane mawazo Na kufahamiana zaidi pande zote mbili Mke/mme huku wakipata maji matam. wazee hawa toka mikoa Kama mitano tofauti timu ya watu Kama 14 hivi.. Wakati baraza likiendelea Kama kawa tukawa tunachombeza inshu Za kisiasa kupima hali ya Hewa huko mikoani..

Unajua tena wazee nao wanasoma upepo wa mazungumzo wasijejichomeka kusiko, pasina shaka yoyote tulijua wazee hawa wote au karibia wote WALIKUWA TANU DAMDAM Na sasa wako CCM vilevile so tukawa tukiwatia moyo Kwamba Chama Lao bado liko fit as per chaguzi Za madiwani Kwamba wamepata more seats..

Of couse Kwenye bunge letu lile lisilo rasmi tulijifanya nasi ni wafuasi Wa CCM ili tusiwakere wazee wetu hawa off couse harusi ianze Na kumalizika fresh.. Cha kushangaza mzee mmoja akafunguka Na kusema '' Tunawashangaa sana nyie watu wa Dar, mnaipenda sana CCM'' Kwa taarifa yenu huko mikoani CCM INACHUKIWA NA KUCHUKIKA.. '' hapo baraza likageuka Na kuchangamka kila mzee sasa akafunguka Na kuanza kutema Cheche jinsigani CCM inavyochukiwa Kwenye maeneo ya mkoa wake, imagine within 14 wazee and more 2 others waliotujoin baadae hakuna Hata mmoja aliyeonekana kuwaunga mkono nyinyiem. Mmoja akadirikii kusema Kwenye michezo Yao ya Bao akitokea mzee anaongelea kuisifia
CCM wanamtenga Na hawajishughulishi nae, Hata akipata tatizo hawaendi kumwona, manake ni MWIZI nae VILEVILE..

Mmoja akafunguka zaidi Na kudai kama watu wa DSM tutaendelea Na Tabia mbaya ya kuendekeza CCM Basi ni aheri mikoa ijitenge kila mmoja iwe Na serikali yake.. Mmoja akadakia wazara zote, Serikali kuu yote, Na Mali zake zote ziko Dar, makampuni yote yanayoinyonya nchi yako Dar na yanamilikiwa na viongozi waliopo Dar hii hii. Viongozi wote wakuu wa Chama na serikali yake wako Dar, hivyo Dar ndio inafaidi Jasho la watanzania wengine. Akasema pia ni kweli Dar Yenye wakazi zaidi ya milioni 5, ni kura nyingi sana hivyo wanaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi Kwa asilimia kubwa..

Wanasema zomea zomea sasa imepitwa Na wakati wanaanza mawe. 'kama wezi Wa kuku wanapigwa mawe KWANINI wezi wa taifa wasipigwe mawe vilevile?' alihoji mzee mmoja huku wengine wakimshangilia Kama shujaa flan.. Bunge lile tulilikatiza saa Saba Usiku, liliwavutia sana wananchi wengine around that place .. Nikapata Picha jamaa wanachukiwa mbaya..!!, Mtu mmoja nakumbuka aliuliza JE , Chama gani mnadhani ndicho kichukue Dola hiyo 2015, mzee mmoja akajibu Kwa upande wake yeye CCM hawaitakiiii..! Kiingie Chochote lakini sio CCM kauli iliyoonekana kuungwa mkono sana.

Tukachombeza Kwa kuuliza JE kikiingia Chama kingine wanauhakika gani hakitakuwa Kama CCM.. Mmoja fasta akafunguka Na kimsemo' Nyoka ukishajua kaingia chumbani huwezi kulala tena humo, lakini kama hujajua hatari iliyoko ndani utaingia Na kulala salama kabisa, sasa wameshamjua Nyoka iweje wamchague tena? By then nikawauliza kwani ubaya Wa CCM ni huu unaosemwa magazetini au upi, wazee hawa as if walishakaa kabla kupanga majibu mmoja akafunguka, CCM ya Mwalimu Kambarage sio hii, siku hizi kila kitu rushwa, ukienda serikali Za mitaa rushwa, polisi rushwa, mahakamani rushwa, mbaya zaidi hawakuombi rushwa ila utazungushwaaa hadi ugundue mwenyewe kutoa 'mafuta' hapo tayari haraka wanakushugh'ulikia, ukishtaki serikali Za mtaa umemchongea Mtu, unakuta Mtu kakuibia kitu, au kakufanyia fujo, ukienda kushataki polisi Basi polisi wanakusumbua wewe hadi unasamehe, ukishtaki sehemu basi taarifa lazima zimfikie yule uliyemshataki Basi anakuja kukutisha mzee lazima uhame mji, mzee mnoko sana wewe..!' sasa huu uonevu gani, ingekuwepo serikali imara wananchi wake tusingenyanyasika hivi..

Jamani was too long but I realize our mikoani pipo hate this party Kwa kiwango Kikubwa sana..kujisafisha Kwa Chama hiki Kwa sasa ni Ngumu sana, hakijaoza matawi bali shina Na mizizi yake imeshaoza siku nyingi, bidii ya kukunusuru Chama Kwa sasa haipo labda Kama alivyotabiri Nape Kwamba wengi watakikimbia Chama Na hatimae atabaki Yeye alikiunda upya, sasa sijui itakuwa ni baada ya miaka mingapi kikiwa Cha Upinzani.. !!!
 

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
1,137
Utakapo jua watu walivyochoka panda basi kutoka mkoa wowote hapa Tanzania chombezea eti CCM sijui nini utahari bu siku utavurmishiwa hayo maneno jamani
 

swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
37
bado labda kama kutakuwa na mikakati mizito ya kwenda vijijini hasa mwambao na iwe mapema sana
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,849
12,490
Hiyo mbona kawaida tu huku kwetu?mwenyewe nilishuhudia siku wanazi wa ccm waliposhushwa na lori lao lenye mabendera kibao ya chama huku wakiwa wamepigilia mijezi yao walivyo pata tabu ya kupata usafiri kurudi makwao?ilikuwa mida ya saa kumi na mbili hivi watu hao wakitolewa kwenye chaguzi za chama chao zilizoisha hivi karibuni,baada ya kushuka eneo la posta arusha walielekea kunako kituo cha mabasi madogo maarufu kama vi hiace,basi baada ya watatu kati yao kupanda kwenye gari zilisikika kelele zikiwataka watu hao washuke,hata kondakta wa gari hilo alipojaribu kuwatetea kama si kutetea hesabu ya bosi,bado raia walizidi kushinikiza watu hao washuke,kuona zogo linazidi na kuvuta umati ilibidi watii na kushuka,lakini hata walipojaribu kupanda gari jingine walizuiwa na abiria waliokuwa ndani,jingine liliondolewa kwa kasi mara tu walipolisogelea,niliwaacha hapo huku nikijiuliza ni dhambi gani kubwa hivyo waliyonayo raia hawa hadi wakattaliwe na wazawa wenzao,kweli chama kina hali ngumu.
 

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,215
1,752
iweje basi ccm washinde udiwani majuzi na uchaguzi mkuu juzi yake? Hao wazee wanazingua
 

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
iweje basi ccm washinde udiwani majuzi na uchaguzi mkuu juzi yake? Hao wazee wanazingua

Kwenye kao lile tulihoji uongozi wao huko ukoje wengi kuanzia Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, Diwali hadi Mbunge ni CCM, tukawauliza kwanini waliwachagua, wakakiri sababu mbili kwanza Hakukuwa Na Chama Cha kuwatoa matongotongo kuona nyuma ya Pazia la CCM kunani, pili matatizo mengi walisha yafanya sehemu ya maisha Yao Na walijua serikali zote duniani ziko hivyo na Hata hawajujua Kwamba wanakandamizwa.. Sasa wanajuonea wenyewe kupitia bunge uozo waliokuwa wakitendewa, wamema Hata chaguzi Za juzi CCM IMESHINDA vitongoji vya porini sana ambako Hata umeme hawajui ni nini.. Lakini hawawezi kata zenye welewa..
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,716
432298_4694578038896_1219583700_n.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom