Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,176
- 48,460
Leo nataka kujifunza toka kwa wana CCM waliomo JF kwamba wanaposema kwamba wapinzani hawana hoja kwenye jambo fulani huwa wanamaanisha nini hasa? Huwa wanamaanisha hoja ni kuunga mkono ama kupongeza kila kitu kinachofanywa na viongozi wa CCM ama huwa wanamaanisha nini?
Nilishawahi kuuliza kwa misamiati ya siasa za CCM "sera" inamaanisha nini mpaka leo sijapatiwa jibu. Utawasikia wakisema wapinzani hawana sera, sasa ukiwauliza sera ndiyo nini wananuna. Sasa hivi sasa wameibuka na huu msamiati mpya wa "Hoja" kwamba wapinzani hawana hoja ama wameishiwa hoja.
CCM mkituambia kwa mtazamo wenu "hoja" ni nini labda itatusaidia kufanya mijadala yenye tija na nyie. Kama wapinzani hawana hoja itatusaidia kupima kama na CCM nao wana hoja. CCM wa JF tuambieni ili iwe hoja inatakiwa iwe na sifa na vigezo gani!?