Mageta Opanga
Member
- Jul 9, 2009
- 19
- 0
Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura au ni wapinzani na baadhi ya wananchi kudhani uchaguzi wa huru na haki ni chama tawala kushinda tu? Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo? Na hata useme CCM wanaiba kura kwenye ubunge tu bado haiji akilini. Kwa sababu.
1.Wananchi wengi huchagua chama badala ya mtu. Kama mgombea chama chake ni maarufu eneo fulani ana nafasi kubwa ya kushinda.
2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.
Mimi naona ni wakati upinzani waache kukinyooshea CCM kidole kila wakati na badala yake wajiangalie wao wenyewe ni wapi wanakosea. Hakuna uchaguzi ambao upinzani unashindwa bila wao kutoa sababu na visingizo. Uipende CCM au uichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ni chama makini kinacho jua nini cha kufanya kushinda. Upinzani una kazi kubwa ya kuifikia CCM. Kama tatizo ni katiba basi katiba ibadilishwe lakini sidhani kama CCM wana fanya kitu chochote ambacho chama kingine kisingefanya. Mfano ni Chadema ilipo sema itawa gawia wanawake nguo za ndani kama waki wachagua.
Mtazamo wangu tu. Upinzani kazeni buti muifikie CCM.
Fikiria biharamulo mawakala mpaka sasa hivi hawajulikani walipo baada ya kuonyeshwa nyekundu ya msimbazi!!! umaskini huu wapiga kura wanauza shahada ili wapate mafuta ya taa kwenye kibatari ili wanunulie sukari robo kilo, hata wewe sitegemei!!! unapinga hoja harafu unaikubali mia kwa mia!!! hukumu ni moja tu aliyosema Selerii kuwa hatuoni makaburi tutaulizana mwenzangu na wewe kumbe ulikuwa mwizi wa kura?????Vikisaidiana na mashirika ya dini!
Pundamilia unazungumzia ushabiki na unazi wakati wenzio tunazungumzia athari na mustakabali wa Taifa letu. Wananchi watakapochoshwa na ulaghai wa CCM kitakachotokea ni watu kuingia mitaani na kuanza kuchoma nyumba na kupiga mawe magari ya viongozi ama wanene wenyekuvaa mashati ya kijani na njano. Hatutaki kamwe tufike huko ndio maana tunawaomba CCM waache mchezo wao mchafu. Siasa kwa watu makini na waadilifu si wizi na ulaghai ili tu ushindi upatikane. Hata ubishe vipi wanaoujua ukweli wanatambua kwamba CCM imewahi kufanya vitendo hivyo vya wizi wa kura.
Ukubali usikubali CCM si chama madhubuti kama kilivyokuwa. Kimepoteza na kitaendelea kupoteza umadhubuti kwa kwenda nje ya mstari na kukiuka kanuni kama zilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama hicho. Halikadhalika, CCM kilijengeka na kuwa na mtandao mpana kutokana na mfumo wa Chama kimoja pamoja na mvuto, uadilifu na uongozi thabiti wa Waasisi wa Chama hicho. Chama madhubiti hakina sababu ya kutafuta mbinu za ziada kama kugawa kanga, tshirts, kofia, sukari, chumvi ili kiweze kuchaguliwa! Wahenga walisema mfichaficha maradhi kilio kitamuumbua. CCM kinajitahidi kuficha maradhi lakini matokeo yake tunayaona viongozi wa CCM waliokuwa wakiheshimika huko nyuma wanaadhirika kwa kuzomewa majukwaani. CCM kijisahihishe!
Ukweli wenyewe CCM imenufaika na uelewa mdogo wa watu wengi wanaoishi vijijini,uvunjifu wa sheria zote zinazosimamia demokrasia,na imani yao mbovu kujiona wao ndio wanaweza kuendesha nchi au nchi hii ni yao wenyewe, na sio watanzania wengine wenye mtizamo tofauti kisiasa,na huo sio uhai,wanachochea chuki,wanapeleka nchi pabaya sijui nia yao nini,kila nikijiuliza sipati jibu na mwomba Mungu siku zote atusimamie ili nchi iwe na amani CCM inaelekeza nchi kwenye vita ya wenyewe, na ukweli ni kwamba siku za enda mbio,na wakati waja wa mapinduzi makuu,ambapo CCM watashangaa , maana ya nguvu ya umma bado hawaelewi mpaka sasa ,hadhi yake imeshuka sana kwa mizania katika kuaminika miongoni mwa wananchi wengi ,hata baadhi ya vijiji wanawajua ni mafiusadi tuu.