CCM kweli inaiba kura?

Sidhani CCM inaiba kura.

Wananchi tunajiibia kura! Wenyewe!

Pakulalama... kwenye dola.

Milalamo huwa ndio misuluhisho mbadala.

Wananchi ndio walioiba kura

Mwandani ni wako mwenyewe, pevuka utoe songosongo.
 
Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura au ni wapinzani na baadhi ya wananchi kudhani uchaguzi wa huru na haki ni chama tawala kushinda tu? Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo? Na hata useme CCM wanaiba kura kwenye ubunge tu bado haiji akilini. Kwa sababu.
1.Wananchi wengi huchagua chama badala ya mtu. Kama mgombea chama chake ni maarufu eneo fulani ana nafasi kubwa ya kushinda.

2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.

Mimi naona ni wakati upinzani waache kukinyooshea CCM kidole kila wakati na badala yake wajiangalie wao wenyewe ni wapi wanakosea. Hakuna uchaguzi ambao upinzani unashindwa bila wao kutoa sababu na visingizo. Uipende CCM au uichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ni chama makini kinacho jua nini cha kufanya kushinda. Upinzani una kazi kubwa ya kuifikia CCM. Kama tatizo ni katiba basi katiba ibadilishwe lakini sidhani kama CCM wana fanya kitu chochote ambacho chama kingine kisingefanya. Mfano ni Chadema ilipo sema itawa gawia wanawake nguo za ndani kama waki wachagua.

Mtazamo wangu tu. Upinzani kazeni buti muifikie CCM.


Nimesoma kwa makini lakini huo mfano wa kulinganisha...mhhh

Una maana CCM "itawa gawia wanawake nguo za ndani..." ikichaguliwa?

huo ndio uchaguzi mnaofikiria/unaofikiria?
'Je kwa takwimu zilizokuwepo, kura ziliibiwa?'
Kwa undani?
 
Vikisaidiana na mashirika ya dini!
Fikiria biharamulo mawakala mpaka sasa hivi hawajulikani walipo baada ya kuonyeshwa nyekundu ya msimbazi!!! umaskini huu wapiga kura wanauza shahada ili wapate mafuta ya taa kwenye kibatari ili wanunulie sukari robo kilo, hata wewe sitegemei!!! unapinga hoja harafu unaikubali mia kwa mia!!! hukumu ni moja tu aliyosema Selerii kuwa hatuoni makaburi tutaulizana mwenzangu na wewe kumbe ulikuwa mwizi wa kura?????
 
Pundamilia unazungumzia ushabiki na unazi wakati wenzio tunazungumzia athari na mustakabali wa Taifa letu. Wananchi watakapochoshwa na ulaghai wa CCM kitakachotokea ni watu kuingia mitaani na kuanza kuchoma nyumba na kupiga mawe magari ya viongozi ama wanene wenyekuvaa mashati ya kijani na njano. Hatutaki kamwe tufike huko ndio maana tunawaomba CCM waache mchezo wao mchafu. Siasa kwa watu makini na waadilifu si wizi na ulaghai ili tu ushindi upatikane. Hata ubishe vipi wanaoujua ukweli wanatambua kwamba CCM imewahi kufanya vitendo hivyo vya wizi wa kura.

Ukubali usikubali CCM si chama madhubuti kama kilivyokuwa. Kimepoteza na kitaendelea kupoteza umadhubuti kwa kwenda nje ya mstari na kukiuka kanuni kama zilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama hicho. Halikadhalika, CCM kilijengeka na kuwa na mtandao mpana kutokana na mfumo wa Chama kimoja pamoja na mvuto, uadilifu na uongozi thabiti wa Waasisi wa Chama hicho. Chama madhubiti hakina sababu ya kutafuta mbinu za ziada kama kugawa kanga, tshirts, kofia, sukari, chumvi ili kiweze kuchaguliwa! Wahenga walisema mfichaficha maradhi kilio kitamuumbua. CCM kinajitahidi kuficha maradhi lakini matokeo yake tunayaona viongozi wa CCM waliokuwa wakiheshimika huko nyuma wanaadhirika kwa kuzomewa majukwaani. CCM kijisahihishe!

Mkuu,

Pamoja na maelezo yako mazuri, lakini ni vema ukafahamu kuwa katika thread hii kila mtu anatoa hoja zake kwa kueleza kile anachoamini na kutolea maelezo.

Ninaheshimu mawazo yako 100% lakini si lazima nikubaliane na kila jambo unaloliandika. Wewe una mtazamo tofauti na ule nilionao mimi.

Kwa mfano madai yako ya uwizi wa kura ni mepesi kwa sababu kila kituo kinapomaliza kupiga kura matokeo huhesabiwa palepale na mawakala wakati wote wa zoezi zima la kupiga kura na hata kuhesabu wanakuwepo, sasa ni vema ukaeleza kuwa katika nchi nzima mawakala wa vyama vya upinzani hawafanyi kazi zao (kitu ambacho hakileti mantiki)

Hivyo basi madai ya ko ya kwamba kura zinaibiwa mimi ninayaona ni sawasawa na madai ya mfamaji kwani haishi kutapatapa, njoo na maelezo ya kina na ushahidi usio na shaka kuwa kura za mahali fulani iliibiwa na ziliibiwaje na kumbukumbu ya kesi hizo na labda maamuzi ya mahakama yalikuwaje.

Vinginevyo huu wimbo wa CCM kuiba kura tumeshauzoea na kazi iliyopo mbele ya CCM ni kuzidi kujiimarisha na kuwa karibu zaidi na wananchi watanzania ambao wengi wao huishi vijijini.
 
Ukweli wenyewe CCM imenufaika na uelewa mdogo wa watu wengi wanaoishi vijijini,uvunjifu wa sheria zote zinazosimamia demokrasia,na imani yao mbovu kujiona wao ndio wanaweza kuendesha nchi au nchi hii ni yao wenyewe, na sio watanzania wengine wenye mtizamo tofauti kisiasa,na huo sio uhai,wanachochea chuki,wanapeleka nchi pabaya sijui nia yao nini,kila nikijiuliza sipati jibu na mwomba Mungu siku zote atusimamie ili nchi iwe na amani CCM inaelekeza nchi kwenye vita ya wenyewe, na ukweli ni kwamba siku za enda mbio,na wakati waja wa mapinduzi makuu,ambapo CCM watashangaa , maana ya nguvu ya umma bado hawaelewi mpaka sasa ,hadhi yake imeshuka sana kwa mizania katika kuaminika miongoni mwa wananchi wengi ,hata baadhi ya vijiji wanawajua ni mafiusadi tuu.

Froida,

Kadri nilivyosoma maelezo yako hapo juu, wewe ni moja kati ya wale wanaamini kuwa CCM ndiyo chama pekee chenye nguvu na kinachojali wananchi wake. Isipokuwa tatizo ulilonalo sasa hivi ni kwamba umejaa msongo wa mawazo kiasi cha kwamba fikra zako zimebeba hofu.

Ninakuhakikishia kuwa CCM ni imara na ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote wa Tanzania bila ya kujali imani na itikadi zao za kisiasa. Vilevile katika kipindi cha miaka 17 iliyopita tangu kuasisiwa mfumo wa vyama vingi hapa nchi Tanzania, CCM pamoja na serikali yake imeendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanashiriki ipasavyo katika kuhakikisha kuwa wanakuza demokrasia ya vyama vingi nje na ndani ya vyama vyao. CCM inatambua kuwa ustawi wa vyama vya kisiasa katka nchi hii ni moja kipimo cha maendeleo ya taifa.

Leo hiininafarijika kuona kuwa mazingira mazuri yaliyopo yanafanya vyama vya siasa kuweza kushiriki kwa uhuru mpana na mkubwa kabisa katika chaguzi mbalimbali na hata kuwa na viti vya ubunge na udiwani, haya ni maendeleo ya taifa. Ni matumaini yangu kuwa wananchi bado watapata fursa zaidi ya kujihusisha katika kuendeleza demokrasia hapa nchi mwetu, lakini pia ninaonya kuwa mchakato huo hauwezi kuwa na maana kama wananchi wenyewe hawatajua nini maana ya demokrasia.
 
Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura au ni wapinzani na baadhi ya wananchi kudhani uchaguzi wa huru na haki ni chama tawala kushinda tu? Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo? Na hata useme CCM wanaiba kura kwenye ubunge tu bado haiji akilini. Kwa sababu.
1.Wananchi wengi huchagua chama badala ya mtu. Kama mgombea chama chake ni maarufu eneo fulani ana nafasi kubwa ya kushinda.

2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.

Mimi naona ni wakati upinzani waache kukinyooshea CCM kidole kila wakati na badala yake wajiangalie wao wenyewe ni wapi wanakosea. Hakuna uchaguzi ambao upinzani unashindwa bila wao kutoa sababu na visingizo. Uipende CCM au uichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ni chama makini kinacho jua nini cha kufanya kushinda. Upinzani una kazi kubwa ya kuifikia CCM. Kama tatizo ni katiba basi katiba ibadilishwe lakini sidhani kama CCM wana fanya kitu chochote ambacho chama kingine kisingefanya. Mfano ni Chadema ilipo sema itawa gawia wanawake nguo za ndani kama waki wachagua.


Mtazamo wangu tu. Upinzani kazeni buti muifikie CCM.

mkuu, jibu lako hili hapa: "Paul Muwanga telephoned Nyerere that very day and said: “Mr President, the Democratic Party has won the elections and Paul Semwogerere has just been here, he wants me to hand over to him. What should I do now?” Nyerere replied and said: “Paul Muwanga, you have got my army there – change all the results”. Muwanga changed all the results and gave victory to UPC/Obote. (The Commonwealth Observer Team declared the elections free and fair- Editor)"

link ya hii thread hii hapa. Nadhani utaona wizi wa kura ulianzia wapi na kwamba sio kitu kilicho-fictitious. Kuiba asilimia 80 ya kura ni kazi rahisi sana, hata wewe mwenyewe unaweza kufanya. Wewe huwezi hata siku moja kuwa mpigaji kura, muhesabu kura, msimamiaji kura, mchapishaji wa karatasi za kupigia kura, nk., alafu utegemee kura ziwe za haki. NEVER!!!

 
Aisifuye mvua imewahi kumnyea.
Chama kikupacho kula huwezi kukikashifu hata siku moja.

Sasa MH Obama anawapa Bichwa kwamba serikali ya CCM inajali watu wake! Mwaka 2010 watapa 110% ya kura zote, nikiwa na maana kwamba wapigaji kura wengine watatoka visiwa vya Comoro.
 
Safali hii tukimbaka mtu ,anavitambulisho vya kula,ana nyalaka za tume,ananunua vitambulisho,anakula zilizokwisha pigwa ,ole wake ajue tutamchoma moto tu ,na kumvisha taili ya mpila wa katapila .mwagia dizeli na petrol tunamuwasha moto mchana kweupe ,hakuna tena kumtafuta polisi au waangalizi wa uchaguzi au kupeleka malalamiko kwenye kamisheni sijui kamati ya usimamizi wa uchaguzi ,ni kiberiti tu ndicho kitakachowazuia vibaka hawa.

Nasema ole wao mwaka ujao wanaotumiliwa kufanya mikakati ya wizi basi wajue tutawatia moto hapa hapa duniani afu uko akhera wataenda kumalizia ,mambo ya kupelekana polisi hayaleti tija ,unampeleka mtu polisi sijui kwenye vyombo vya shelia halafu wanakugeukia na kukufanya wewe ndio mwenye kosa, adabu ni ile ile sera ya Muheshimiwa WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ,sera ya papo kwa papo.

Au mnasemaje ndugu wananchi hapa JF ?
 
Mwiba,
Siku hizi naona huwazi ya Mungu bali ya wanaadamu.Haya!!!
Sasa ile "Popo Bawa style" ndo basi tena. Nakumbuka ilivyofanya kazi kule Pemba hata Mh. Mkapa aliipata joto ya jiwe, walipo "mpopo bawa" na kumvunja mishipa ya kiuno, ilibidi akafanyiwe operesheni ya haja kule Ufaransa kurejesha hali sawa, lakini alikuwa kesha haribika. Hasira zake akajaku'nguta risasi mtindo mmoja. Popo bawa mchezo!
 
Nimekuwa nikiwaza na kuwazua, bila kupata majibu muafaka. Wananchi wana hali mbaya, wanaoishi kwa mlo mmoja kwa siku wanaongezeka. Walio tegemezi kwa wenzao wanaongezeka. Wanaomaliza vyuo na kukosa ajira wanaongezeka. Wakina mama wanajifungulia chini. Majambazi yanaua roho zetu kila uchao. Maisha yetu ni ya kuunga unga. Wananchi karibu wote wanalalamika kuwa hali ni mbaya!

Maisha ya leo ni magumu kuliko ya jana, na hali haionekani kutengemaa. Sijaweka takwimu zozote kwa sababu takwimu zimekwisha wekwa sana...na zote zinaonyesha kitu kile kile. Taifa linadidimia kwa umasikini.

Sababu ya umasikini wetu ni sisi wenyewe kuendelea kuchagua Chama Cha Mapinduzi kushika hatamu ya uongozi wa nchi yetu.

Hata wale wanaoishabikia CCM kwa kuvaa nguo za kijani, kushinda juani na kupepurusha bendera zao, maisha yao ni ya dhiki tu.

Swali la msingi. Kwanini CCM iendelee kushinda katika uchaguzi, na hususani uchaguzi ujao? nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom