CCM kweli inaiba kura? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kweli inaiba kura?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jul 10, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura au ni wapinzani na baadhi ya wananchi kudhani uchaguzi wa huru na haki ni chama tawala kushinda tu? Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo? Na hata useme CCM wanaiba kura kwenye ubunge tu bado haiji akilini. Kwa sababu.
  1.Wananchi wengi huchagua chama badala ya mtu. Kama mgombea chama chake ni maarufu eneo fulani ana nafasi kubwa ya kushinda.

  2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.

  Mimi naona ni wakati upinzani waache kukinyooshea CCM kidole kila wakati na badala yake wajiangalie wao wenyewe ni wapi wanakosea. Hakuna uchaguzi ambao upinzani unashindwa bila wao kutoa sababu na visingizo. Uipende CCM au uichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ni chama makini kinacho jua nini cha kufanya kushinda. Upinzani una kazi kubwa ya kuifikia CCM. Kama tatizo ni katiba basi katiba ibadilishwe lakini sidhani kama CCM wana fanya kitu chochote ambacho chama kingine kisingefanya. Mfano ni Chadema ilipo sema itawa gawia wanawake nguo za ndani kama waki wachagua.


  Mtazamo wangu tu. Upinzani kazeni buti muifikie CCM.
   
 2. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mbona Masatu, Tumain na wengine wenye fikra sawa za CHAMA CHA MASELA hawajaleta maoni yao ktk hili? It takes too long to wait...lol!

  Ila, kwa kuwa CCM ni kinara wa kuiba kura na kubadilisha matokeo...ulieleta hoja hii ingawaje nawe ni mwezao CCM, omba wafuatao watoe hoja zao ili usione tuna toa porojo

  1. Wananchi wa Biharamulo
  2. W3ananchi wa Tarime
  3. Wananchi wa Busanda
  4. Mzee Ndesamburo
  5. John Mnyika

  Hawa niliowataja wana majibu ya moja kwa moja...Baada ya hapo nitakuwa tayari kuleta kuchangia
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Baada ya nini mkuu?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kweli, kijuu juu hapo huwezi kuona kuwa dhana ya wizi wa kura inakuja. Lakini Mkuu wizi wa kura hauanzii na kuishia katika kupiga na kuisabu kura tu. Ni mchakato mreefu unaohusisha mfumo mzima wa uchaguzi. Hapa na maanisha Mipango au maandalizi ya uchaguzi wenyewe, tume ya uchaguzi, mawakala wa tume,wapiga kura(wananchi), zoezi la kuandikisha wapiga kura,vyama vyenyewe vya siasa, kampeni za uchaguzi, zoezi la kupiga kura, kuisabu, matokeo. Mbali na hayo kuna sheria za uchaguzi, usajili wa vyama vya siasa, vyombo vya sheri, vyombo vya kusimamia sheria hizon.

  Kwa ufipi tu, yote niliyoyataja hapo juu, yapochezewa chezewa ,kupelekwa pelekwa na kupindishwa pindishwa kwa maslahi na matakwa ya chama tawala ndiyo husemwa kisiasa kuwa ni wizi wa kura.

  Neno wizi au kuiba, lina nukta nyingi hata kuthibitisha kutokea kwake, kwa mfano unapomshitaki mwizi mahakamani lazima uthibitishe pasipo shaka kuwa pamoja na mambo mengine ingredients za kosa lenyewe kama zilivyo katka kanuni ya adhabu au sheria yoyote ya namna kama hiyo kwa mfano, Uthibitishe nia au dhamira ya unyanganyi (fraudulent intention to deprive...), uhamisho wa hicho kilichoibiwa tena kiwe na sifa ya kuibika(..extortion of anything capable of being stolen...)..n.k

  Kwa hiyo unaposikia CCM wameiba kura si lazima waibe kwa kubeba masanduku(japo inaweza kuwa hivyo), ni kufanya mipango kama hiyo kupunguza kura zenu na kufanya zao zionekane nyingi( ndo unashangaa JK kupata 80% kwa staili hiyo), au hata kuwanyima fursa ya kuandikishwa watu wanaowanona si wapiga kura wao kama inavyofanyika hivisasa Micheweni kule Pemba, wote huu pamoja na mengine ni mchakato wa kuiba kura kwa kutumia au kuchezea sytem ya uchaguzi siyo!
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wanaoamini kuwa JK alipata 80% mwaka 2005 wanahitaji kupimwa vichwa vyao.
   
 6. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam, nasikia Zanzibar Seif Shariff alishinda lakini mbinu zikafanywa akapokwa ushindi! Kuna jamaa aliyehusika kwenye 'wizi' wa kura anasimulia jinsi walivyokimbia na masanduku ya kura! Wizi wa kura upo!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivyo vyama vya upinzani viibiwe nini? CCM haijawahi kuiba kura..!
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  CCM haihitaji kuiba kura ili ipate ushindi. Hao wenye dhana ya kufikiri ili chama kishinde ni lazima kiibe kura basi hao ndiyo wezi na hawafai kabisa.

  Lakini hata hivyo haingii akilini kabisa pale hizi kauli za kuiba kura zinapozushiwa CCM kwani wanaofanya hivyo wanajaribu kukimbia vivuli vyao kwa vile CCM ni chama imara na madhubuti kabisa kilichojijenga vizuri na pia chenye mtandao mkubwa na mpana. Japo sina takwimu, lakini nafiriki CCM ndiyo chama chenye mtandao mkubwa zaidi kuliko vyama vyote vya kisiasa katka Afrika Mashariki.

  Mbali ya hayo hapo juu, katika Tanzania, ni CCM tu ndiyo chama kinachoaminika kwa wananchi kuliko vyama vingine vya siasa na ndiyo maana katika uchaguzi wa 2005 katika baadhi ya majimbo ambayo upinzani ulishinda kiti cha ubunge, lakini kura za urais zilipigwa kwa mgombea wa CCM.

  Nadhani huu si wakati wa kuendelea kurudiarudia visingizio ambavyo havisaidii na wala havizuii CCM kushinda.
   
 9. K

  Kachero JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani nani hakumbuki kilichotokea 1995 CCM walishindwa karibu majimbo yote ya Dar pamoja na kuiba kura.Iliwalazimu walete mizengwe mpaka kura za Dar zikarudiwa ndipo waliposhinda.

  Uchaguzi ukiwa hiari na wa wazi CCM itapigwa chini tuu hata wafanye nini.Mtaji wao mkubwa ni wizi wa kura, lakini kile kilichotokea Iran mwaka huu kinaweza kutokea hapa kwetu pia kwani watanzania waliowengi wameshafunguka macho sasa na wako makini katika upigaji kura.
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama ni wizi wanaufanya kwa kulazimisha/kushawishi wapiga kura ambao wengi uelewa wao ni mdogo kuwapigia wagombea wa CCM. Vinginevyo kwa mfumo wa sasa wa upigaji kura, kuhesabu kura na kutangaza/kubandika matokeo ni vigumu sana kura kuibiwa. Kwa Zanzibar, hasa nafasi ya Urais wa SMZ hakuna jinsi, kura zinaibiwa kwa kutumia maguvu ya DOLA.
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pundamilia unazungumzia ushabiki na unazi wakati wenzio tunazungumzia athari na mustakabali wa Taifa letu. Wananchi watakapochoshwa na ulaghai wa CCM kitakachotokea ni watu kuingia mitaani na kuanza kuchoma nyumba na kupiga mawe magari ya viongozi ama wanene wenyekuvaa mashati ya kijani na njano. Hatutaki kamwe tufike huko ndio maana tunawaomba CCM waache mchezo wao mchafu. Siasa kwa watu makini na waadilifu si wizi na ulaghai ili tu ushindi upatikane. Hata ubishe vipi wanaoujua ukweli wanatambua kwamba CCM imewahi kufanya vitendo hivyo vya wizi wa kura.

  Ukubali usikubali CCM si chama madhubuti kama kilivyokuwa. Kimepoteza na kitaendelea kupoteza umadhubuti kwa kwenda nje ya mstari na kukiuka kanuni kama zilivyoainishwa ndani ya Katiba ya Chama hicho. Halikadhalika, CCM kilijengeka na kuwa na mtandao mpana kutokana na mfumo wa Chama kimoja pamoja na mvuto, uadilifu na uongozi thabiti wa Waasisi wa Chama hicho. Chama madhubiti hakina sababu ya kutafuta mbinu za ziada kama kugawa kanga, tshirts, kofia, sukari, chumvi ili kiweze kuchaguliwa! Wahenga walisema mfichaficha maradhi kilio kitamuumbua. CCM kinajitahidi kuficha maradhi lakini matokeo yake tunayaona viongozi wa CCM waliokuwa wakiheshimika huko nyuma wanaadhirika kwa kuzomewa majukwaani. CCM kijisahihishe!
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ukweli wenyewe CCM imenufaika na uelewa mdogo wa watu wengi wanaoishi vijijini,uvunjifu wa sheria zote zinazosimamia demokrasia,na imani yao mbovu kujiona wao ndio wanaweza kuendesha nchi au nchi hii ni yao wenyewe, na sio watanzania wengine wenye mtizamo tofauti kisiasa,na huo sio uhai,wanachochea chuki,wanapeleka nchi pabaya sijui nia yao nini,kila nikijiuliza sipati jibu na mwomba Mungu siku zote atusimamie ili nchi iwe na amani CCM inaelekeza nchi kwenye vita ya wenyewe, na ukweli ni kwamba siku za enda mbio,na wakati waja wa mapinduzi makuu,ambapo CCM watashangaa , maana ya nguvu ya umma bado hawaelewi mpaka sasa ,hadhi yake imeshuka sana kwa mizania katika kuaminika miongoni mwa wananchi wengi ,hata baadhi ya vijiji wanawajua ni mafiusadi tuu.
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam, wizi wa kura si tu ule wa kukimbia live na masanduku ya kura DOLA inaweza kuiba kura kwa njia mbalimbali. Kitendo cha 'wajumbe' wa Chama-Tawala kupita na kununua shahada za kupigia kura na kugawa vijizawadi kuwarubuni wananchi wasifanye uamuzi kwa utashi wao wenyewe pia ni aina ya 'wizi'. Vitendo vya Polisi na FFU kumwagwa kwenye maeneo ya kupigia kura nayo ni aina ya 'wizi' wa kumnyima mpigakura uhuru wake maana wapo ambao huogopa kujitokeza kupiga kura kwa kuhofia fujo inaweza kutokea wakapata madhara.
   
 14. F

  FrankGM Member

  #14
  Jul 10, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli tunahitaji kuwa na uthibitisho kabla ya kutamka bayana iwapo kuna wizi katika kura au la.
  Mazingira yenyewe yanaashiria au kutoa mwanya wa wananchi kufikiria kuwa upo uwezekano wa kura kuibwa!!!!!!!

  Mathalani katika uchaguzi wa jimbo la Busanda idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ni zaidi ya mara mbili ya waliopiga kura. Hali hii imejirudia tena katika uchaguzi wa jimbo la Biharamulo, waliojiandikisha kupiga ni zaidi ya mara mbili ya waliopiga kura!! Pana nini hapa??? Lazima kuna tatizo hapa.

  Ushindi katika uchaguzi ili usiwe na dalili za utata inapendeza takwimu zinaposhabihiana vizuri.
  Hata hivyo haya ni mazingira tu. Lakini kinachotushangaza serikali wala watendaji wake hawashtuki katika hili.

  Hapa ndipo wanapotoa mwanya kwa Watanzania kudhania kuwa upo uwezekano wa kura kuwa zinafanyiwa usanii kwa staili yoyote ile ambayo sisi hatujaijua bado.
   
 15. B

  Balingilaki Member

  #15
  Jul 10, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama wanaiba basi wamebobea......ila mi nadhani ni watz kukipigia kura mana 80% mabush na ccm damudamu
   
 16. B

  Balingilaki Member

  #16
  Jul 10, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unapinga na hilo........inabidi kupima kweli
   
 17. B

  Balingilaki Member

  #17
  Jul 10, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa dar na miji mikubwa wanaiba kweli......ila villa hawaibi
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wanaiba uchaguzi mzima hata kabla haujafanyika na huwa wanatembea na dataz ambazo zipo tayari ,yaani pale wakishapata waliojiandikisha kupiga kura hapo ndio huanza hesabu za plus au minus kura na huachwa blanks ili msimamizi wa tume ya uchaguzi iwe rahisi kujaza matokeo.
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kwasababu ya mabadiliko ya uelewa na elimu, wizi wa kura hautoi jibu la muda mrefu la chama cha siasa kuendelea kuongoza. Ilikuwa rahisi vyama vya upinzani vilipoanzishwa na kadri siku zinavyokwenda itakuwa almost impossible kama amani nayo itazingatiwa.

  Mi naona vyama vya upinzani vijishughulishe katika kutoa elimu ya vyama vyao kwa wapiga kura kwa kutumia misingi sahihi ambayo haitawaweka njia panda wapiga kura. Kwa mfano, unapoonyesha kuchukia ufisadi uonyeshe kwa vitendo. Mambo ya kutumia gharama kubwa kwenye chaguzi ndogo tu, inaleta mashaka ni nani anayelipia gharama hizo za uchaguzi kama sio huohuo ufisadi. Kiu ya watu wengi leo ni kuona wanaibuka viongozi bora na sio wababaishaji.

  Chama chenye hii cream ya viongozi bora naamini kitapata nafasi ya kuongoza kadri siku zinavyoongezeka.
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Vikisaidiana na mashirika ya dini!
   
Loading...