MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura ......
Mbona Masatu, Tumain na wengine wenye fikra sawa za CHAMA CHA MASELA hawajaleta maoni yao ktk hili? It takes too long to wait...lol!
Ila, kwa kuwa CCM ni kinara wa kuiba kura na kubadilisha matokeo...ulieleta hoja hii ingawaje nawe ni mwezao CCM, omba wafuatao watoe hoja zao ili usione tuna toa porojo
1. Wananchi wa Biharamulo
2. W3ananchi wa Tarime
3. Wananchi wa Busanda
4. Mzee Ndesamburo
5. John Mnyika
Hawa niliowataja wana majibu ya moja kwa moja...Baada ya hapo nitakuwa tayari kuleta kuchangia
Kweli, kijuu juu hapo huwezi kuona kuwa dhana ya wizi wa kura inakuja. Lakini Mkuu wizi wa kura hauanzii na kuishia katika kupiga na kuisabu kura tu. Ni mchakato mreefu unaohusisha mfumo mzima wa uchaguzi. Hapa na maanisha Mipango au maandalizi ya uchaguzi wenyewe, tume ya uchaguzi, mawakala wa tume,wapiga kura(wananchi), zoezi la kuandikisha wapiga kura,vyama vyenyewe vya siasa, kampeni za uchaguzi, zoezi la kupiga kura, kuisabu, matokeo. Mbali na hayo kuna sheria za uchaguzi, usajili wa vyama vya siasa, vyombo vya sheri, vyombo vya kusimamia sheria hizon....Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo?
2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.
Wanaoamini kuwa JK alipata 80% mwaka 2005 wanahitaji kupimwa vichwa vyao.
CCM haihitaji kuiba kura ili ipate ushindi. Hao wenye dhana ya kufikiri ili chama kishinde ni lazima kiibe kura basi hao ndiyo wezi na hawafai kabisa.
Lakini hata hivyo haingii akilini kabisa pale hizi kauli za kuiba kura zinapozushiwa CCM kwani wanaofanya hivyo wanajaribu kukimbia vivuli vyao kwa vile CCM ni chama imara na madhubuti kabisa kilichojijenga vizuri na pia chenye mtandao mkubwa na mpana. Japo sina takwimu, lakini nafiriki CCM ndiyo chama chenye mtandao mkubwa zaidi kuliko vyama vyote vya kisiasa katka Afrika Mashariki.
Mbali ya hayo hapo juu, katika Tanzania, ni CCM tu ndiyo chama kinachoaminika kwa wananchi kuliko vyama vingine vya siasa na ndiyo maana katika uchaguzi wa 2005 katika baadhi ya majimbo ambayo upinzani ulishinda kiti cha ubunge, lakini kura za urais zilipigwa kwa mgombea wa CCM.
Nadhani huu si wakati wa kuendelea kurudiarudia visingizio ambavyo havisaidii na wala havizuii CCM kushinda.

Kama ni wizi wanaufanya kwa kulazimisha/kushawishi wapiga kura ambao wengi uelewa wao ni mdogo kuwapigia wagombea wa CCM. Vinginevyo kwa mfumo wa sasa wa upigaji kura, kuhesabu kura na kutangaza/kubandika matokeo ni vigumu sana kura kuibiwa. Kwa Zanzibar, hasa nafasi ya Urais wa SMZ hakuna jinsi, kura zinaibiwa kwa kutumia maguvu ya DOLA.
Neno wizi au kuiba, lina nukta nyingi hata kuthibitisha kutokea kwake, kwa mfano unapomshitaki mwizi mahakamani lazima uthibitishe pasipo shaka kuwa pamoja na mambo mengine ingredients za kosa lenyewe kama zilivyo katka kanuni ya adhabu au sheria yoyote ya namna kama hiyo kwa mfano, Uthibitishe nia au dhamira ya unyanganyi (fraudulent intention to deprive...), uhamisho wa hicho kilichoibiwa tena kiwe na sifa ya kuibika(..extortion of anything capable of being stolen...)..n.k
Kwa hiyo unaposikia CCM wameiba kura si lazima waibe kwa kubeba masanduku(japo inaweza kuwa hivyo), ni kufanya mipango kama hiyo ..............................
, wote huu pamoja na mengine ni mchakato wa kuiba kura kwa kutumia au kuchezea sytem ya uchaguzi siyo!
Huwa najiuliza kila siku. Je ni kweli CCM huwa wanaiba kura au ni wapinzani na baadhi ya wananchi kudhani uchaguzi wa huru na haki ni chama tawala kushinda tu? Ukiangalia matokeo ya uraisi mwaka 2005 JK alipata kura karibia 80%. Sasa ingechukuwa wizi wa kiasi gani kufikia asilimia hiyo? Ingekua ni wizi wa kura watu wasingesha stukia hapo? Na hata useme CCM wanaiba kura kwenye ubunge tu bado haiji akilini. Kwa sababu.
1.Wananchi wengi huchagua chama badala ya mtu. Kama mgombea chama chake ni maarufu eneo fulani ana nafasi kubwa ya kushinda.
2.Kama mgombea uraisi anaweza kushinda kwa asilimia 80 basi ina maana chama chake kina umaarufu wa kutosha kuji nyakulia wabunge wa kutosha.
Mimi naona ni wakati upinzani waache kukinyooshea CCM kidole kila wakati na badala yake wajiangalie wao wenyewe ni wapi wanakosea. Hakuna uchaguzi ambao upinzani unashindwa bila wao kutoa sababu na visingizo. Uipende CCM au uichukie lakini ukweli unabaki kuwa CCM ni chama makini kinacho jua nini cha kufanya kushinda. Upinzani una kazi kubwa ya kuifikia CCM. Kama tatizo ni katiba basi katiba ibadilishwe lakini sidhani kama CCM wana fanya kitu chochote ambacho chama kingine kisingefanya. Mfano ni Chadema ilipo sema itawa gawia wanawake nguo za ndani kama waki wachagua.
Mtazamo wangu tu. Upinzani kazeni buti muifikie CCM.
Naam, nasikia Zanzibar Seif Shariff alishinda lakini mbinu zikafanywa akapokwa ushindi! Kuna jamaa aliyehusika kwenye 'wizi' wa kura anasimulia jinsi walivyokimbia na masanduku ya kura! Wizi wa kura upo!
Kwani nani hakumbuki kilichotokea 1995 CCM walishindwa karibu majimbo yote ya Dar pamoja na kuiba kura.Iliwalazimu walete mizengwe mpaka kura za Dar zikarudiwa ndipo waliposhinda.
Uchaguzi ukiwa hiari na wa wazi CCM itapigwa chini tuu hata wafanye nini.Mtaji wao mkubwa ni wizi wa kura, lakini kile kilichotokea Iran mwaka huu kinaweza kutokea hapa kwetu pia kwani watanzania waliowengi wameshafunguka macho sasa na wako makini katika upigaji kura.
Mi naona vyama vya upinzani vijishughulishe katika kutoa elimu ya vyama vyao kwa wapiga kura kwa kutumia misingi sahihi ambayo haitawaweka njia panda wapiga kura.