CCM kwanini mnamlea Mbowe kama kweli ni muuaji?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,838
Reaction score
50,542
Kuna propaganda inaenezwa na CCM kwamba ndani ya CHADEMA ukipingana na Mwenyekiti taifa wa chama hicho, basi ni lazima uuawe. Mbowe ana madhaifu yake kama binadamu mwingine yeyote yule, lakini hili la kusingizia kuua wapinzani wake limevuka Mpaka.

Alipokufa Chacha Wangwe kwa ajali kule Kibaigwa, tuliona jinsi CCM walivyotengeneza hisia miongoni mwa watanzania kwamba Wangwe kauawa na Mbowe kwa kuwa eti alikuwa anataka kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa.

Siku ya mazishi ya Wangwe kule Tarime kulikuwa na tafrani iliyofadhiliwa na CCM kiasi kwamba ilionekana kama vile Mbowe angeshambuliwa. Baada ya mazishi ya Wangwe, uchaguzi ukarudiwa na Charles Mwera wa CHADEMA akashinda na wananchi wa Tarime wakakataa Propaganda ya CCM kwamba Mbowe ndiyo alihusika kumuua Wangwe.

Ben Saanane Mwanachadema ambaye alikuwa anaibukia kwenye mijadala ya mitandaoni, akiwa ni kilongola kijana kwenye kuukosoa utawala wa Rais John Magufuli, alipotea ghafla na mpaka leo hajulikani alipo. Mara hii tena CCM wakaleta propaganda kwamba aulizwe Mbowe wapi alipo Saanane!

Juzi msemaji wa serikali (kama Akaunti iliyotumika ni ya kwake) mara tu baada ya Mbowe kuishutumu serika kuwa ni mshukiwa namba moja wa mashambulizi dhidi ya Lissu, msemaji huyo wa Serikali aliandika maneno kwamba inawezekana Mbowe naye ndiye mshukiwa namba moja.

Lakini CCM ndiyo inatowa mawaziri na ndiyo yenye rais anayeongoza nchi. Shutuma kwamba Mbowe anaua wanachadema wanaopingana naye ni ya kijinga ingawa inafikirikisha sana. Kama CCM ndiyo wenye dola kwa sasa wanashindwaje kutumia dola kukusanya ushahidi wa kutosha ili kumtia hatiani Mbowe?

Kama leo wanasisitiza kwamba mwenye ushahidi kuhusu Lissu kushambuliwa aupeleke Polisi ni kwa nini wao CCM hawapeleki ushahidi polisi kuthibitisha kwamba Mbowe huwa anaua wapinzani zake ndani ya CHADEMA?

Waziri wa sheria ni CCM, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ni CCM, Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa ni CCM, waziri anayesisimamia Idara ya Usalama wa Taifa ni CCM na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania ni CCM. Kwa nini CCM isitumie fursa hiyo kumuadabisha Mbowe?

Kwa nini CCM inamlea Mbowe pamoja na kujua uovu wake wote wa "kuua" wapinzani zake ndani ya CHADEMA?
 
Mbowe angekuwa na kosa lolote linalo weza kuadhibiwa lingeshawekwa wazi na kuadhibiwa juu. Hivi kama wanadiriki kuharibu hata bustan zake fikiria wangemfanya nini kama atauwa mtu!
 
Ukiishutumu serikali unakamatwa ukasaidie upelelezi,ukiishutumu CHADEMA kwamba inahusika upo huru vyombo vya dola havitajishughulisha na wewe,mpk hapo utakuwa unaelewa nani mhusika.
 
Kuna propaganda inaenezwa na CCM kwamba ndani ya CHADEMA ukipingana na Mwenyekiti taifa wa chama hicho, basi ni lazima uuawe. Mbowe ana madhaifu yake kama binadamu mwingine yeyote yule, lakini hili la kusingizia kuua wapinzani wake limevuka Mpaka.

Alipokufa Chacha Wangwe kwa ajali kule Kibaigwa, tuliona jinsi CCM walivyotengeneza hisia miongoni mwa watanzania kwamba Wangwe kauawa na Mbowe kwa kuwa eti alikuwa anataka kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa.

Siku ya mazishi ya Wangwe kule Tarime kulikuwa na tafrani iliyofadhiliwa na CCM kiasi kwamba ilionekana kama vile Mbowe angeshambuliwa. Baada ya mazishi ya Wangwe, uchaguzi ukarudiwa na Charles Mwera wa CHADEMA akashinda na wananchi wa Tarime wakakataa Propaganda ya CCM kwamba Mbowe ndiyo alihusika kumuua Wangwe.

Ben Saanane Mwanachadema ambaye alikuwa anaibukia kwenye mijadala ya mitandaoni, akiwa ni kilongola kijana kwenye kuukosoa utawala wa Rais John Magufuli, alipotea ghafla na mpaka leo hajulikani alipo. Mara hii tena CCM wakaleta propaganda kwamba aulizwe Mbowe wapi alipo Saanane!

Juzi msemaji wa serikali (kama Akaunti iliyotumika ni ya kwake) mara tu baada ya Mbowe kuishutumu serika kuwa ni mshukiwa namba moja wa mashambulizi dhidi ya Lissu, msemaji huyo wa Serikali aliandika maneno kwamba inawezekana Mbowe naye ndiye mshukiwa namba moja.

Lakini CCM ndiyo inatowa mawaziri na ndiyo yenye rais anayeongoza nchi. Shutuma kwamba Mbowe anaua wanachadema wanaopingana naye ni ya kijinga ingawa inafikirikisha sana. Kama CCM ndiyo wenye dola kwa sasa wanashindwaje kutumia dola kukusanya ushahidi wa kutosha ili kumtia hatiani Mbowe?

Kama leo wanasisitiza kwamba mwenye ushahidi kuhusu Lissu kushambuliwa aupeleke Polisi ni kwa nini wao CCM hawapeleki ushahidi polisi kuthibitisha kwamba Mbowe huwa anaua wapinzani zake ndani ya CHADEMA?

Waziri wa sheria ni CCM, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ni CCM, Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa ni CCM, waziri anayesisimamia Idara ya Usalama wa Taifa ni CCM na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania ni CCM. Kwa nini CCM isitumie fursa hiyo kumuadabisha Mbowe?

Kwa nini CCM inamlea Mbowe pamoja na kujua uovu wake wote wa "kuua" wapinzani zake ndani ya CHADEMA?
mkuu kwa serikali hii ya ccm mtu yeyote ambaye si mwanaccm,mtu ambaye ni mwanachama wa chadema au CUF añahesàbika ñi mtànzàñia pale linapokuja suala la kulipà kodi tu,ila kwa mambo meñgine hahesabiki kama ni mtanzania hivyo hasitahiri kulindwa wala anaewaua wenzake hatakiwi kuchukuliwa hatua, by the way wewe unaelewaje mtu mzima ñà akili yake anapokuambia mafisadi wamekimbia,eti kwa kuwa wamejiunga chadema
 
licha ya propaganda zao lakini kwa wenye akili washaelewa nani wauwaji, kwa wewe kuwa CCM ni sawa na mfu tu
 
Back
Top Bottom