lufungulo k
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 2,607
- 2,062
umeongea mengi mazuri, yanayopaswa kufanywa na jamii nzima ya tanzania, kama ushahidi upo hakuna aliye juu ya sheria tusihukumu watu kwa kuwa fulani kaema huyu fisadi tujenge utaratibu wa kumtaka ampeleke mahakamani nae atoe ushahidi sio kutumia vyombo vya habari kulalamika na kupakana matope, sio dhambi ndugu, jamaa, watoto, mke nk kushiriki kwa pamoja shughuli za kisiasa midhali wanapitia mchakato wa kupigiwa kura si kuteuliwa[hata kama hana sifa] tusiwahukumu wanasiasa peke yao yapo maeneo mengi ktk taifa baba,mama na watoto wamekuwa wakifanya kazi pamoja wakiwa wamepitia njia halali na upendeleo hilo ndilo taifa kwa uwazi kabisa hata vyama vingine vyenye nguvu hapa nchini undugu, ujamaa , baba na mtoto wanavyo lkn cha msingi je? wanastahili wamepatikana kwa uwazi kama upendeleo ndo taifa hilo mezea. utekelezaji wa sera ukisimamiwa vzr bila shaka hata vijana kuzurura itapungua kwani fursa nyingi za kijipatia kipato zitapatikana sote kwa pamoja tuuungane kuikosoa serikali inapokosea. na jamii ikubali kupokea maagizo, amri na maonyo toka kwa serikali ili kulinda amani na utulivu.Mnyonge anyongwe na atapata haki inapostahiki.
CCM inaweza tu kuwathabiti tena na kukubalika na watanzani kama sio wote basi waliowengi kama itafanya yafutayo nitataja machache
1. Kuwakamata, kuwafilisi na kuwafunga mafisadi wote wanaofahamika na watanzania kutuharibia na kutuhujumu.
2. Kuboresha huduma za afya na elimu bora, kwamba waliokata tamaa wakaona na kuamini hivyo, sio propaganada
3. Kurejesha na kusimamia nidhamu na maadili katika secta zote za utumishi serikalin na hasa utawala bora.
4. Kushughurika na tatizo la mfumko wa bei ambao sasa unawanufaisha matajiri wachache kupanga wanavyotaka.
5. Kufufua viwanda vilivyofilisika na kuanzisha vingine sambamba na kuongeza ajira kwa vijana wengi wanao zurula mitaani
6. Kuacha siasa za undugunization, chama kimekuwa cha wakubwa na familia zao baba, mama, watoto, mashemeji nk kiwe cha watanznia wote kama ilivyokuwa enzi za hayati baba wa taifa Mwl JK nyerere.
7. Kuacha siasa za udin, kwa kufanya hivyo baadhi ya watanzani wanajitoa kwa kuona wanabaguliwa au wenzao kupendelewa
8. Kuacha kutumia vyombo vya dolla kulazimisha maamuzi yasiyokubaliwa na wananchi (ukandamizaji)
Hayo ni machache sasa sioni kama kunahata moja kwa ccm ni jepesi ikaliacha - tusubili tuone tunakoelekea.