CCM: Kwanini kisife?

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,119
2,000
Na Ansbert Ngurumo

NDANI ya miaka saba tu, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameteua makatibu wakuu watatu - Yusuf Makamba, Wilson Mukama, na Abdulrahman Kinana. Mtangulizi wake, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa miaka yote aliyokaa madarakani (10), alifanya kazi na Katibu Mkuu mmoja, Philip Mangula.

Si hilo tu. Hata serikalini, ndani ya miaka minne, Rais Kikwete ameteua mawaziri wakuu wawili - Edward Lowassa na Mizengo Pinda. Mtangulizi wake, Rais Mkapa, alifanya kazi na Waziri Mkuu mmoja tu, Frederick Sumaye - kwa miaka 10. Maana yake nini? Baadhi yetu tunaona kwamba Rais Kikwete bado anafanya ‘mazoezi' ya kuunda serikali.

Ni zaidi ya hapo. Hata kwa kutazama tu utendaji wa viongozi anaowateua serikalini na katika chama, ni dhahiri kwamba miongoni mwa vielelezo vya udhaifu wa Rais Kikwete ni uteuzi wa wasaidizi wake. Na wakati mwingine baadhi yetu tunadhani kwamba inawezekana Rais Kikwete anateua viongozi dhaifu kwa kuogopa ‘kufunikwa' na viongozi mahiri. Tunakumbuka, kwa mfano, jinsi mzozo wa kimadaraka kati yake na swaiba wake wa zamani, Edward Lowassa, ulianza kufukuta chini chini baada ya yeye na ‘watu wake' kugundua kwamba Lowassa alikuwa ‘anamfunika' bosi wake katika utendaji wa masuala mazito.

Lakini hilo lilikuwa tatizo la bosi, kwa kuwa utendaji mzuri wa mdogo wake ulikuwa unajenga sifa ya serikali nzima, hasa mkuu wa serikali mwenyewe. Na katika mazingira ya utendaji yasiyomtegemea mtu mmoja pekee, kiongozi mkuu anayejizungushia watendaji na wasaidizi dhaifu anakuwa anapalilia na kustawisha udhaifu wake mwenyewe. Kwa kutazama na kulinganisha utendaji wa Mkapa na Kikwete, hasa katika suala la uteuzi ndani ya chama na serikali, Watanzania wanajua nani mahiri, na nani dhaifu, kati ya viongozi hawa wawili.

Kwa maana hiyo, ‘ulegelege' wa Serikali katika masuala mazito na unyonge wa sasa wa CCM, ni matokeo ya uteuzi na usimamizi mbovu. Na hili limedhihirishwa na ukweli kwamba katika fursa zote alizopata za kuunda serikali upya, au kukipanga chama upya, Rais Kikwete hawezi kujisifu kwamba amezitumia vizuri. Kwa upande wa chama, tunapotazama hili la uchaguzi ndani ya chama uliomalizika - ambao kwa mara ya kwanza umeingiza mke wa rais na mtoto wake katika baadhi ya vikao vikubwa vya maamuzi - tunaona dhamira ya rais na familia yake kujaribu ‘kuteka' chama chao kwa masilahi wanayojua wao.

Lakini hitimisho la uchaguzi wao, na jinsi rais alivyounda upya sekretarieti ya CCM, umekuwa ushahidi mwingine wa kushindwa kwake kukibadilisha chama kuelekea matamanio yao ya kung'ang'ania madaraka. Katika sekretarieti hii ya Kinana, Zakia Meghji, Nape Nnauye, Mohamed Seif Khatib, Asha-Rose Migiro, Mwigulu Nchemba, na Vuai Vuai; CCM itakuwa inajipa sifa za kijinga kuamini inapiga hatua kubwa kwenda mbele.

Na kwa jinsi historia ya utawala wa Rais Kikwete ilivyo hadi sasa, baadhi yetu hatuamini kama hii ndiyo sekretarieti yake ya mwisho kabla hajaondoka madarakani. Hata Philip Mangula katika nafasi ya makamu mwenyekiti, hatarajiwi kuleta jipya katika CCM ya sasa iliyomong'onyoka, na inayoathiriwa na magonjwa sugu niliyotaja kwenye uchambuzi wangu wiki kama tatu zilizopita. Kama ambavyo JK alimwingiza Pius Msekwa ili kujipatanisha naye baada ya kumfanyia faulo za kumnyang'anya uspika mwaka 2005, ndiyo alivyomwingiza Mangula sasa kama njia ya kupoza machungu aliyomsababishia tangu wakati wa mchakato wa kugombea urais mwaka 2005.

Na kama ambavyo uteuzi wa Msekwa kuwa makamu mwenyekiti uliirudisha CCM nyuma miaka 35, ndivyo uteuzi wa Mangula, Kinana, Meghji, Khatib na wengine utakavyopunguza au kuondoa kasi ya chama hicho kukua. Hata wanaosifu historia binafsi za wateule wapya wa rais, kama ninavyoona baadhi yao wakimsifia Kinana, ingekuwa vema wakajikumbusha mbwembwe zilizomwingiza Wilson Mukama katika nafasi hiyo. Ameacha urithi gani? Sasa hivi, ingawa ndio wameteuliwa, tunapaswa kuanza kujiuliza, "nani anakuja baada ya Kinana?"

Na licha ya utendaji wa Mangula huko nyuma, nafasi aliyopewa sasa haimfanyi kuwa mtendaji. Na katika mazingira ambamo bosi wake ni Kikwete, tusitarajie lolote la maana kutoka kwake. Zaidi ya hayo, Kama CCM imekosa mbadala wa Mangula, Kinana, Meghji na Seif Khatib katika zama na changamoto tulizomo, ni ushahidi mwingine kwamba chama hicho kinaelekea makaburini.

Na Watanzania watamshukuru Rais Kikwete kwa kuwasaidia kuharakisha kifo cha chama alichodhamiria kukiua mwaka 2005 kama kisingemteua kuwa mgombea urais. Na kwanini kisife?


 

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,195
Hakuna sababu za kiasili wala kimapokeo kwamba ccm hakitakufa,nadharia ya kupanda,kudumaa na kushuka chini ndiyo itaiangusha serikali ya ccm na hivyo ndivyo ilivyo duniani kote.Hata kama siyo leo na kesho,basi kesho kutwa ccm kitakufa vibaya.Ni binadamu mpuuzi pekee,mwenye kuamini kuna marefu yasiyo na ncha
 

UPIU

JF-Expert Member
Jun 26, 2012
602
0
Hakuna sababu za kiasili
wala kimapokeo kwamba ccm hakitakufa,nadharia ya kupanda,kudumaa na
kushuka chini ndiyo itaiangusha serikali ya ccm na hivyo ndivyo ilivyo
duniani kote.Hata kama siyo leo na kesho,basi kesho kutwa ccm kitakufa
vibaya.Ni binadamu mpuuzi pekee,mwenye kuamini kuna marefu yasiyo na
ncha
kitakufa lakini si 2015
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,111
2,000
mtoa mada umeeleza mengi na kwa kina , lkn inajionesha umesimamia ktk misingi ya kila chenye mwanzo kina mwisho, basi ktk hilo unaielekeza jamii iamini kuwa ikae isubiri CCM ife ndipo iandae chama mbadala[maana vilivyopo vyaweza kufa kabla ya ccm] maana ktk uimarishaji chama kunamarekebisho ya katiba, kanuni na uongozi ili lengo lifikiwe ktk hatua mbalimbali ambazo ccm imepitia binafsi inanionyesha kuwa ccm hujitambua[ kiko imara] au[kiko dhaifu] na kifanye nini? kujirekebisha chama hiki kupata udhaifu si kipindi hiki tu ktk uhai wake, ktk miaka ya karibuni kabla ya kifo cha mwl nyerere kiliyumba saaana mwl akakikosoa ,kikamsikiliza,kikajipanga,kikarekebisha hivyo sina shaka MH MANGULA, MH KINANA, ni silaha bora zilizojaa busara,na thabiti ktk kuisimamia serikali ktk utekelezaji wa sera.
 

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,451
1,170
mtoa mada umeeleza mengi na kwa kina , lkn inajionesha umesimamia ktk misingi ya kila chenye mwanzo kina mwisho, basi ktk hilo unaielekeza jamii iamini kuwa ikae isubiri CCM ife ndipo iandae chama mbadala[maana vilivyopo vyaweza kufa kabla ya ccm] maana ktk uimarishaji chama kunamarekebisho ya katiba, kanuni na uongozi ili lengo lifikiwe ktk hatua mbalimbali ambazo ccm imepitia binafsi inanionyesha kuwa ccm hujitambua[ kiko imara] au[kiko dhaifu] na kifanye nini? kujirekebisha chama hiki kupata udhaifu si kipindi hiki tu ktk uhai wake, ktk miaka ya karibuni kabla ya kifo cha mwl nyerere kiliyumba saaana mwl akakikosoa ,kikamsikiliza,kikajipanga,kikarekebisha hivyo sina shaka MH MANGULA, MH KINANA, ni silaha bora zilizojaa busara,na thabiti ktk kuisimamia serikali ktk utekelezaji wa sera.
Leo hii nani mwenye ubavu wa kufanya hayo hapo kwenye RED?
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,111
2,000
Leo hii nani mwenye ubavu wa kufanya hayo hapo kwenye RED?
wapo, wengi saana ,wewe, mimi na wengine kama nilivyosema daima hakisahau njia yake ndo maaana kimeyumba kimekosolewa, kimesikia , kimejipanga ktk kujirekebisha ili kikubaliwe tena na watanzania wachache waliokikimbia kwa kuona kinapotea ktk njia yake. nasisitiza kimerudi upya ktk njia yake serikali itabanwa ktk utekelezaji sera wa miradi mbalimbali chezea mangula weye.
 

Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,591
2,000
Mie sitaki kife..natamani kiwe chama pinzani imara mwaka 2015

ni lazima kife, CCM ni janga hata historia yake inabidi ichomwe moto, 2015 kusiwe na mtu atakayeitaja tena CCM ,ee mwenyezi mungu tuondolee balaa la CHAMA CHA MAFISADI hapa nchini.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,495
1,250
CCM kufa itakufa lakini inazo dawa za kurefushia maisha kwa sasa. Serikalini wapo akina Maghufuli, Muhongo, Mwakyembe,..., huku kwenye CCM yupo Nape, wameongezwa akina Mangula, Kinana, AshaRose Migiro,... Akina Mukama, Msekwa wameonekana zilikuwa dawa feki au zilizo-"expire"!

Gonjwa inalougua CCM halina tiba. Itakufa tu.
 

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,423
1,225
Kama sikosei kulikuwa na Jaka Mwambi kabla ya Makamba so inawezekana akawa na makatibu wakuu wanne.
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,066
1,225
Walioko CCM, SIO SIRI NI WALE AMBAO WANANUFAIKA MOJA KWA MOJA NA KUAKO HUKO. VINGINEVYO, HAKUNA MTANZANIA ANAEITAKIA MEMA NCHI HII, ANAENDELEA KUSUPPORT CCM. KWANI HATA MITAANI, TEMBEA MIKUSANYIKO YOTE YA KIJAMII, HAKUNA HATA MTU MMOJA ANAE THUBUTU KUJINASIBU NA CCM. WATU WAMESHA ELEWA. NA NGUVU YAO YA MWISHO, WAISLAMU, IMESHAGEUKA. SIDHANI KAMA KUTAKUA NA MUISLAMU TENA ATAKAE DANGANYWA NA KIONGOZI WAKE WA DINI KUICHAGUA CCM. ENOUGH IS ENOUGH. CCM TUMESHA IHUKUMU. TUNASUBIRI MUDA UFIKE TUINYONGE.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,495
1,250
Walioko CCM, SIO SIRI NI WALE AMBAO WANANUFAIKA MOJA KWA MOJA NA KUAKO HUKO. VINGINEVYO, HAKUNA MTANZANIA ANAEITAKIA MEMA NCHI HII, ANAENDELEA KUSUPPORT CCM. KWANI HATA MITAANI, TEMBEA MIKUSANYIKO YOTE YA KIJAMII, HAKUNA HATA MTU MMOJA ANAE THUBUTU KUJINASIBU NA CCM. WATU WAMESHA ELEWA. NA NGUVU YAO YA MWISHO, WAISLAMU, IMESHAGEUKA. SIDHANI KAMA KUTAKUA NA MUISLAMU TENA ATAKAE DANGANYWA NA KIONGOZI WAKE WA DINI KUICHAGUA CCM. ENOUGH IS ENOUGH. CCM TUMESHA IHUKUMU. TUNASUBIRI MUDA UFIKE TUINYONGE.
Uliona idadi ya waliochukua fomu kugombea UONGOZI katika ngazi mbalimbali za CCM? Uliona mapesa yalivyokuwa yakimwagwa kuusaka uongozi ndani ya CCM? Wewe ukisusa, wenzako wanakula!
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,066
1,225
uliona idadi ya waliochukua fomu kugombea uongozi katika ngazi mbalimbali za ccm? Uliona mapesa yalivyokuwa yakimwagwa kuusaka uongozi ndani ya ccm? Wewe ukisusa, wenzako wanakula!
time alone, oohhh time will tell.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,101
2,000
wapo, wengi saana ,wewe, mimi na wengine kama nilivyosema daima hakisahau njia yake ndo maaana kimeyumba kimekosolewa, kimesikia , kimejipanga ktk kujirekebisha ili kikubaliwe tena na watanzania wachache waliokikimbia kwa kuona kinapotea ktk njia yake. nasisitiza kimerudi upya ktk njia yake serikali itabanwa ktk utekelezaji sera wa miradi mbalimbali chezea mangula weye.

Mnyonge anyongwe na atapata haki inapostahiki.

CCM inaweza tu kuwathabiti tena na kukubalika na watanzani kama sio wote basi waliowengi kama itafanya yafutayo nitataja machache

1. Kuwakamata, kuwafilisi na kuwafunga mafisadi wote wanaofahamika na watanzania kutuharibia na kutuhujumu.

2. Kuboresha huduma za afya na elimu bora, kwamba waliokata tamaa wakaona na kuamini hivyo, sio propaganada

3. Kurejesha na kusimamia nidhamu na maadili katika secta zote za utumishi serikalin na hasa utawala bora.

4. Kushughurika na tatizo la mfumko wa bei ambao sasa unawanufaisha matajiri wachache kupanga wanavyotaka.

5. Kufufua viwanda vilivyofilisika na kuanzisha vingine sambamba na kuongeza ajira kwa vijana wengi wanao zurula mitaani

6. Kuacha siasa za undugunization, chama kimekuwa cha wakubwa na familia zao baba, mama, watoto, mashemeji nk kiwe cha watanznia wote kama ilivyokuwa enzi za hayati baba wa taifa Mwl JK nyerere.

7. Kuacha siasa za udin, kwa kufanya hivyo baadhi ya watanzani wanajitoa kwa kuona wanabaguliwa au wenzao kupendelewa

8. Kuacha kutumia vyombo vya dolla kulazimisha maamuzi yasiyokubaliwa na wananchi (ukandamizaji)


Hayo ni machache sasa sioni kama kunahata moja kwa ccm ni jepesi ikaliacha - tusubili tuone tunakoelekea.
 
Top Bottom