VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Huku mwezi wa sita ukikaribia kwa kazi,mwezi wa kumkabidhi Uenyekiti wa CCM Rais John P. Magufuli,safu mpya ya uongozi wa CCM imeanza kuleta kizungumkuti chamani. Vigogo wa chama na makada wakongwe wameanza kupigana vikumbo vya tambo ili wachomoze katika safu mpya.
Makundi mbalimbali,sawia na yale ya wakati wa uchaguzi mkuu,yamechomoza upya huku kila kundi likitaka kupenyeza mtu wake kwenye safu mpya. Baada ya Mwenyekiti mpya wa kitaifa kupatikana,watateuliwa na kuchaguliwa viongozi wapya wa CCM wakiwemo Makamu wa Mwenyekiti wa Tanzania Bara na Zanzibar; Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu,Wajumbe wa Kamati Kuu na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kumekucha ndani ya CCM. Mtumbua majipu anakaribia kutwaa chama,vikumbo kwa maslahi gani?
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam