CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada wanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.

Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!

Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.

Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
ImageUploadedByJamiiForums1418627020.883607.jpg
 
Jumba bovu ni Nape na Kinana. Nape amekuwa na kauli mbovu sana kwa wananchi , anawaona mazuzu , wajinga na pia hizo mbinu zote mnazotumia kufanya hujuma zinakera wananchi
 
Ma zimwi buana ....... wanapenda sana mambo ya u profesa u profesa bila kujali side effect yake!
 
Huu uandishi huu unafurahisha sana sana iaseeee naam. MSALANI kajitutumua kujibu hapo, asante kwa kuokoa jahazi maana hii aibu ya mwaka hii. Kha CCM chama dume, imeshageuka CCM tezi dume mara hii??
 
Last edited by a moderator:
ImageUploadedByJamiiForums1418627097.705163.jpg
Ndio maisha bora hayo mliyokuwa mnayaimba majukwaaan?
Nyambaffffff ndio mshahara wenu huooo
 
Back
Top Bottom