CCM kwa nini mnataka watu wakimbie nchi?


M

MLO

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
157
Likes
24
Points
35
M

MLO

Senior Member
Joined Apr 2, 2012
157 24 35
Nasikitika sana jinsi hali ya amani inavyozidi kuhujumiwa kila kukicha na hakuna baba wa kukemea.
Kauli ya Nape ni kauli ambazo zinatakiwa kukemewa vikali katika kipindi hiki tata.Ubaguzi wa dhhili kwa watanzania ambao wameungana kutaka kuleta mabadiliko kama katiba inavyoruhusu.

Chama cha mapinduzi kinawajibika kukadhi madaraka kwa amani kwa kikundi kinginge kitakachopewa ridhaa na wananchi bila hujuma na kusabaisha wanachama wa ccm watakaoachishwa kazi na kura za wananchi waendelee na shughuli za kama kawaida ndani ya Tanzania.

Viongozi wa ccm hawatakiwi kuwarubuni watanzania kama hawana akili kuwa ccm pekee ndiyo kundi teule la kutufikisha katika mafanikio yetu.ubaguzi huu utawafanya watanzania wakatane mapanga kutetea ccm wakati ccm yenyewe imebakiwa na kundi dogo ambalo halina nguvu ya wananchi.

ccm itambue kuwa mapanga yakilia kwa kipenga chao marefa watambue kuwa kuna watanzania wataikimbia nchi, ccm ikipoteza dola kwa sababu ya kauli zao.

Nape atambue vyombo vya dola ni mali ya nchi siyo ya chama kama anavyodhani.kuondoka kwa ccm madarakani hakifuti katiba ya Tanzania.Hivyo kuvitia hofu vyombo vya dola visishirikiane na kundi la watanzania linalotambuliwa na katiba ni uhaini

Ccm watambue wakati wao wanacheza wanatumia muda mwingi kulinda walichonacho,wakati huohuo waliko nje wanangalia mapungufu yao na kuyatumia.Hivyo basi ni wajibu wao kuziba mianya hiyo ili kuhifadhi walichonacho.siyo kuwatemea mate wapinzani,mashabiki na waamuzi ili wasione madhaifu yenu.

Ccm iliandae jeshi la polisi kufanya kazi na vyama vyote kama linavyotakiwa na katiba.kwani hata polisi wanandugu zao waliko upinzani.Wasitake kulifanya jeshi liwachukie wananchi na wananchi waone kuwa jeshi la polisi ni kikwazo kwa mabadliko yao.

ccm itambue kumtumia Waziri wa mambo ya ndani kama ngao yao sio nusura yao.nini kilitokea kwa Omary mapuri.
bora uzungukwe na wananchi kuliko jeshi la polisi kwa hicho ni kikundi kidogo sana katika jamii.

Ccm itambue kuwatisha viongozi wa vyombo vya dola kuwa madaraka yao ni ya ccm huo ni uhaini pia, kwani dola ipo kwa mujibu wa katiba.Ingawa wanajibika kuilinda serikali ya wananchi na sio ya ccm.hivyo wananci wakisema chadema oyee,cuf oyee dola inalinda mali ya wananchi.

Ccm inaligawa Taifa kwa matamushi yasio na mjengo kama ya Nape kuwa watanzinia wanapanga kuwaua watanzania wenza na walinzi wao.Ccm imepotosha utendaji kazi wa polisi na kulifanya kama green guard.

Ccm itambue katika nchi nyingi uongozi ni wa kubadilishana leo Republican na kesho democratic kwa nchi kama marekani.hivyo ccm iwashukuru wananchi kwa kuaminiwa kwa miaka hamsini hivyo iwaache wakiwa kitu kimoja.

Mungu ibariki dunia,africa,TANZANIA iwe na mabadiliko yenye AMANI.
 
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Messages
4,787
Likes
3,112
Points
280
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2011
4,787 3,112 280
CCM hawana kipya cha kuongea mkuu,wamebakiwa na propaganda chafu dhidi ya CDM na kulitumia jeshi la polisi kubaki madarakani japo najua mwishovwa siku haitawasaidia sana
 
Sizinga

Sizinga

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2007
Messages
8,280
Likes
915
Points
280
Sizinga

Sizinga

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2007
8,280 915 280
duh sioni mwishomzuri kwa huku tunakoelekea.
 
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
4,214
Likes
1
Points
0
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
4,214 1 0
Tatizo la ccm ni kupenda watanzania waitumikie ccm na si ccm iwatumikie watanzania! Binafsi naamini ili itanzania iendelee kuwa moja lazima ccm itoke madarakani, vinginevyo....
 
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
15,618
Likes
6,131
Points
280
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
15,618 6,131 280
Eti NCHIMBI kukutana na KINANA huko songea kuijadili chadema!subiri katiba mpya waziri sii mwanasiasa sijui mtafanyaje
 
Ranks

Ranks

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
2,597
Likes
866
Points
280
Ranks

Ranks

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
2,597 866 280
Mbaya zaidi wana CCM wanakosa hoja zenye mashiko za kutetea magamba,hivyo wanavaa ngozi ya CUF na kuwahadaa wanacuf kama wenzao kumbe ni magamba,kisha kujenga hoja na ushawishi wa kipuuzi ndani ya cuf kuonyesha adui ni CHADEMA."UKWELI KWA HAPA CCM ILIPOFIKIA NI JANGA KWA TAIFA"
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,115
Likes
650
Points
280
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,115 650 280
Usiwape kichwa wajinga hawa wao ndio watakaokimbia nani atamkimbia mhalifu
 
F

Froida

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Messages
8,477
Likes
1,793
Points
280
F

Froida

JF-Expert Member
Joined May 25, 2009
8,477 1,793 280
Amwthibitisha kwamba Nchimbi ni mshirika wa maandalizi ya mauaji ya wananchi kwenye mikutano na maandamano ya chadema tatizo huwa hawana siri wakipanga mipango kwa laana walizonazo wanaropoka kwanza kabla ya mpango kufanywa,anayoyasema Nape yanatokea Arusha sasa mikutano ya kampeni inavamia nchemba alisema maneno haya haya kuhusu video kumbe ikajulikana ndie aliyeiichora santuri hiyo
 
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
1,339
Likes
5
Points
0
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
1,339 5 0
Hizo kauli za Nape zitampleka The Hague, asidhani kwamba atasalimika kwani vyombo vipovinarekodi kumbukumbu. Kauli za kijinga kama hizo zitamweka pabaya kama aliipenda CCM hivyo kwa nini alianzisha CCJ na mzee Sitta?
 

Forum statistics

Threads 1,275,122
Members 490,908
Posts 30,533,310