CCM kwa hapa mmevuka mipaka

CCM kwa hapa mmevuka mipaka

DUH, Ama kweli tunaenda mbali sana WANA TZ, ilimradi mtu ajiandike kinacho kuja akilini mwake bila ya kufikiria. Sasa alipokuwa anapewa hiyo pete wewe ulikuwepo. Au mtu akiva pete basi ni Uchawi.


Amesilimishwa kuvaa mapete ya majini na Ramadhani Dau!!
 
1. Wameanguka chini kuashiria anguko la chama chao, lugha ya picha kwa Jerry!
2. Wanalia na kusaga meno kwa kula udongo; wanamdokeza Jerry ukomo CCM madarakani.
3. Jerry na mwenzake wamevaa roho ya CCM;wanacheka na kushangilia wakati wenzao wanaomboleza!!!
 
Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa Jerry Silaa akisindikizwa Jukwaani kwa staili ya aina yake ya kufagiliwa njia na WanaCCM waliokuwa wakibiringika mpaka kwenye ngazi za jukwaa. Anayemsindikiza ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi.​

Sijui kama mnasomaga magazeti au blogs wanapotoaga habari za huyu jamaa. Inaonekana anapenda utukufu. Simhukumu lakini nimesoma most of the time wanamuaddress kwa hali ya juu sana. Mfano utasikia wanamuita "His Lord...His Worship...and so on and so on.
Nakumbuka nyakati zile Mkapa anaingia madarakani watu walikua wanamuita mtukufu hususani media jinsi walivokua wanamuaddress. Akakataa kata kata kuitwa Mtukufu na majina mengine kama hayo.
Ila kijana naona anapeta sana na ndo anazidi kupewa mautukufu.
Kamekua kamungu kadogo hapa Dar kuliko hata Rais wake.
tehe tehe tehe tehe.
Mstahiki Meyaaaaaaaaa
 
njaa mbaya sana ndugu zangu, hao wamepewa chaao
 
Wanawake mnatia aibu,Hivi mwanaume utajisikiaje mke wako hajawahi kukufanyia vile hata mara moja hata kukupokea kwa busu tu nyumbani ila anaenda kuviringika kwa mwanaume mwingine namna hiyo? Be careful wanaume mnaoruhusu wake zenu wakaviringike namna vile.Halafu mbona wanaume hakuna ulikuwa mkutano wa wanawake tu?
 
kwani kipofu na maiti nani zaidi,kuna mtu humu anawaita wanaccm maiti.
 
Jina la huyo binti ni Mtumwa...kwa hiyo hakuna cha kushangaa hapo.
 
MBONA SIWAONI VIJANA? WAMEAMKA SASA HAWATAKI TENA KUBURUTWA.....NURU IMEANZA NA SISI KISHA ITAENDA KWAO (kina mama)

HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA KAMWE
 
Jerry Silaa kashaingia kwenye mambo ya ushirikina. angalieni PETE za Mzee Yahya !

Huu ndiyo ukweli mkuu huko lazima ukasafishwe nyota na waganga, CCM lazima uwe na majini zaidi ili kupenyeza kule juu. Unaweza kushangaa huyu dogo kama mganga wake ni mkali zaidi ya wale wengine anweza akapata hata ugombea Urais 2015 kwa ticketi ya magamba.
 
mnakumbuka katika biblia kuna mfalme alishabikiwa sana, akajiita Mungu, mwishowe ukawa mbaya sana, ajiulize silaha kwa nini hawa wanamshangilia wakibusu ardhi na majani wakimwabudu, ili hali:

1. asilimia 60 ya watoto wao wamefeli kidatao cha nne,

2. kuna mgao mkali wa umeme

3.hakuna maji bali mgao wa kutisha

4. kupanda kwa bei za vyakula, hakuna mwenye uhakika wa mlo
5. watu kujenga mabondeni, hakuna viwanja vilivyopimwa na yeye ni meya!

6. hakuna ajira

7 kuna vurugu za kidini na kikabila

8. kuna foleni za kutisha dsm

9. jiji ni chafu linanuka

10. shule za private ada ni mdundo

11. wanafunzi maskini hawapati mikopo bali watoto wa matajiri

12. mafisadi wa chama chake wanazidi kukomba hazina ya walipa kodi kwa mitindo ya epa, dowans, deep green, nk


SASA ANASHANGILIWA KWA LIPI?

I salute u, ponts well arngd
 
Poleni watanzania taifa la waji,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Kitabu kitakatifu cha Mungu (Biblia) Kinatushauri sisi waja wake maneno yafuatayo, nanukuu "waacheni wafu wawazike wafu wenzao".

astafiluh Jery tayari ushasahau mafundisho tuliopewa pale Azania Front! Msujudie Bwana Mungu wako.. unakumbuka hata shetani alipomjaribu Yesu.... hilo ni jaribu na limekushinda... usijali Mungu wenu ni wa Rehema tubu na siku nyingine ukumbuke amri kumi na Mungu. wengine wana mapepo hapo wanataka uruke wawe wamekuteka ki jumla
 
Aisee, maji yamezidi unga, Damn!!!!

attachment.php

hako kameya nasikia kapung'a sijui kweli?
 
Angefanyiwa Slaa tungesikia kila aina ya sifa,chandema tumewazoea. Kama hamna habari hao wamama ndio wapiga kura, sio vijana wenu wa viroba
 
502 Bad Gateway
nginx/1.2.7

Nikifungua baadhi ya post, why kwa leo?
 
Back
Top Bottom