CCM kutawala toka uhuru ni udikteta

CCM kutawala toka uhuru ni udikteta

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,375
Reaction score
25,455
Wanajamvi, kwanza nianze na definition hii hapa chini.

“Single-party dictatorships are regimes in which one party dominates politics. In single-party dictatorships, a single party has access to political posts and control over policy.”

Kwasababu nchi yetu ni ya kidemokrasia, na inayotakiwa kufuata multiparty system (kikatiba), kuzuia shughuli za vyama hivyo ni uvunjaji wa katiba. Ni uvunjaji wa katiba wenye sifa kuu za udikteta.

Tokea tukubaliane na mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi, hatujawahi kupata chama tofauti na CCM. Ambao matatizo yote ya Taifa hili wao ndiyo wako responsible.

Hatujawahi kupata viongozi wa chama tofauti, kwasababu pia kuna party dictatorship, ambayo inasimamiwa na party leader ili kukwamisha maendeleo ya demokrasia. Hapo udikteta wa chama unasimamiwa na viongozi wa serikali na makada wa chama.

Mfano rais ambaye ni mwenyekiti wa chama, anapotumia madaraka yake kukiuka katiba ya kidemokrasia na kushinda uchaguzi kwa kupitia mabao ya mikono, ukandamizaji wa vyama pinzani, kuminya uhuru wao wa kikatiba, kuwatisha, kuwateka, kuwaua nk.

Kama tunasema tuna demokrasia, halafu tuna katiba ambayo kuna mwananchi yoyote anaweza akawa juu yake, hilo tatizo kubwa mno na matokeo yake ndo haya ya party dictatorship!

Kwenye demokrasia ya kweli, no one is above the law na kwasababu mwenyekiti wa CCM amekuwa above the law miaka yote toka tupate uhuru, na hata baada ya mabadiliko ya katiba kuingiza demokrasia ya vyama vingi, bado Mwenyekiti wa CCM yuko above the law. Na nyakati nyingine wanachama wa CCM wako above the law. Hata Mwenyekiti wao ambaye ndiye dikteta mkuu, aliwahi kusema “hao wa kijani wasiguswe”

Sasa kwa ujinga wetu, eti CCM wanataka kutupa lecture kuhusu demokrasia?! Huwa nashagazwa sana na akili zetu sisi Watanzania! Ama ni haki yetu kufanyiwa haya yote? Maana naona watu ni kama hawajitambui kwa kiasi kikubwa, na ndiyo maana tumefika hapa tulipo.

Na huyu Rais wa sasa ndo amefumbuwa wengi macho hadi katiba mpya inaanza kudaiwa kidogo. Lakini bado kabisa inapokuja kwenye mwamko. Halafu pia upinzani umenishangaza sana kwa kuendelea kushiriki viini macho! Sijui ni idadi kidogo ya wabunge waliopatikana?

Kwa maoni yangu, hata hao wabunge waliopatikana, ni CCM tu iliamua kuwaachia ili kuuficha udikteta wao! Maana huyu mwenyekiti wao wa sasa si anatumia madaraka yale yale ambayo ni “above the law”?
 
muda mwingine wajinga wanaficha ujinga wanapokaa kimya lakini ona sasa kila mtu kajua mjinga kwa kushindwa kukaa kimya. kuilewa CCM inabidi uondokane na ujinga.

Chama hata kutawala miaka 1000 hamna shida kwa sababu inawezekana kabisa chama kukosa mbadala lakini kukumbatia MTU mmoja na kudai hana mbadala ni fedheha kubwa sana
 
Umedhihirisha upumbavu wako

Hebu jaribu kupata exposure kidogo maana maandishi yako yanaonesha una mawazo mgando
Kama umeshindwa kwenda America( USA & Canada) nenda hata Europe tu akili ipate akili kha unakera kwa ufupi!
 
toka nje ya box la fikra mgando, ni USA,Canada na Europe pekee kwa kupata exposure duniani? exposure niliyoipata chini chini ya CPCC inatosha na kubwa mno
 
Mkuu nashukuru kwa intake. Naomba nikwambie tu kwamba chini ya mfumo huu, hatutaweza kuwa na chama ambacho kina nguvu kama ccm. Labda sijakuelewa unachomaanisha unaposema “chama kukosa mbadala”

Kuna shida chama kutawala miaka 1000. Especially kama kuna demokrasia ya kweli. Maana hilo halitawezekana kwa Taifa a lenye wananchi wanaojielewa.

Ndiyo maana nilitangulia kusema hata hizo nafasi chache za ubunge, ccm waliamuwa tu kuwaachia.

Mfano juzi kati ndipo niligunduwa zaidi kuwa huwa walikuwa wanawaachia upinzani. Maana Mrema alilalamika kuwa eti hawajamuachia hata kijiji kimoja kule Kiraracha! Akalalamika sana! Nikagunduwa enzi zile wakisema alikuwa pandikizi.

CCM huwa walikuwa wanaachia majimbo kidogo ili wasinyimwe misaada. Huyu wa sasa ametuthibitishia udikteta wa ccm.
 
Umedhihirisha upumbavu wako

Hebu jaribu kupata exposure kidogo maana maandishi yako yanaonesha una mawazo mgando
Kama umeshindwa kwenda America( USA & Canada) nenda hata Europe tu akili ipate akili kha unakera kwa ufupi!
Eti anasema “kuilewa ccm lazima uondokane na ujinga”, hapo nimeshindwa kumwelewa.

Kwa upande mwingine, ni kweli kufahamu uovu wa ccm, ni lazima uondokane na ujinga. CCM wamekuwa wakitegemea sana ujinga wa wanachama wao walio wengi.
 
toka nje ya box la fikra mgando, ni USA,Canada na Europe pekee kwa kupata exposure duniani? exposure niliyoipata chini chini ya CPCC inatosha na kubwa mno
Wait a minute mkuu, umeipata exposure kupitia CPCC? Hilo Taifa liko bara gani? Au unazungumzia “chemically exposed?”
 
Back
Top Bottom