CCM kusimamisha mgombea mwanamke 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kusimamisha mgombea mwanamke 2015?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kibavu, Apr 30, 2011.

 1. kibavu

  kibavu Senior Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hodi hapa barazani, salaam!
  Hoja ya haja,
  Kwakua wakati wa uteuzi wa spika walitumia kigezo cha jinsia ili kuwaengua baadhi ya watu (Samuel Sitta mathalani) kutoka kwenye kinyang’anyiro cha uspika, je kigezo hicho hicho kinaweza kutumika mwaka 2015 kuteua mgombea mwanamke kwenye Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM. Hii inatokana na ukweli kwamba mvutano unaweza kuwa mkubwa kiasi cha kutishia mgawanyiko wa chama.
  Naomba kuwasilisha.
  NB: hii ni post yangu ya kwanza hapa jamvini nipo tayari kukosolewa kama hoja itaonekana kuwa na uzito wa unyoya.
   
 2. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yawezekana na pengine hii ndio njia pekee ya kuepukana na mpasuko mkubwa ndani ya chama...yaani makundi yote yakose....anapewa nafasi mtu kama Asha Migiro au Tibaijuka!

   
 3. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Labda mpango wa Mwinyi mdogo ugome ndipo wagombea wengine CCM watazuiliwa mbali kwa kigezo cha zamu ya akina mama kama ilivyotokea kwenye uspika.
   
 4. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
   
 5. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kama cdm wataendelea na spidi hii hii hakuna mgombea mwanamke kutoka ccm atakayefua dafu mbele ya mgombea kutoka cdm
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  walete kutoka kundi la walemavu ndipo wataepusha mpasuko.
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wacha uongo wewe kwanini asishinde? acha kuendekeza mfumo dume, mwanamke na mwanamume wanafanana kiutendaji kwani urais unahitaji akili au msuli? isitoshe CCM hata wakimsimamisha Anna Makinda anaweza kupita kwa kishindo itategemeana na utashi wa akina Lewis Makame na kundi lake lililowekwa na Chama pale kutekeleza maagizo ya chama. Ndiyo maana inatakiwa mimi na wewe tukeshe tukiomba dua katiba yetu ibadilishwe au tupate Tume huru ya uchaguzi ili kwa mara ya kwanza tushuhudie uchaguzi nchini kwetu.
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Piga ua, mafisadi nguvu zao za pesa watazipeleka kwa chaguo lao ambaye ni Sophia Simba achukue Urais kilaini huku akiwacha akina Dr. Slaa, Peter Mziray, Husein Rungwe na Dovutwa kwa mbali!
   
 9. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
   
 10. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kwa namna moja au nyingine ni kama tuko pamoja kifikra lakini kamwe sijagusia kuhusu jinsia ya mgombea kutoka cdm na tiyari umesha nihusisha na mfumo dume. Kulikoni.
   
 11. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  sofia simba akiwa rais nahama nchi
   
 12. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wakati mwingine hata kama si kawaida yako kuwa makini katika matamshi na maandiko yako jaribu walau kuonekana makini. Utaletaje jina la Sophia simba katika mada nzito kama hii.
   
Loading...