CCM Kusambaratika!

CCM Kusambaratika!

Huyo FFU anayemvalisha Nape alikuwa analinda amani mkutanoni au alienda kufanya ushabiki wa siasa?


attachment.php
 
Nyie CCM endeleeni kubishana na wapenda haki !! subirini mvua ya MIKUKI TOKA ANGANI.
 
Imekaa vizuri ila chadema wanahitaji kukomaa zaidi hakuna haja ya kucompromise na nyinyiemu ni ngumu kupambana na adui ambaye siku nyingine mnakaa meza moja eti kuleta maridhiano.

Chadema wana miezi 20 tu kabla ya uchaguzi muhimu sana wa serikali za mitaa ambao ni lazima kushinda!
 
Nyie CCM endeleeni kubishana na wapenda haki !! subirini mvua ya MIKUKI TOKA ANGANI.

Kweli tupu, siku zote haki hutawala dhidi ya dhuruma na nguvu ya shetani haiwezi kushinda nguvu ya mungu
 
Acha kife tuu mana tumechoka kuwa wapumbavu kiasi hicho hapa nchini!:fencing:

Mkuu, kama CCM isipokufa basi kitakachokufa ni hili taifa letu ndilo litakufa!

Hatuwezi kukubali taifa letu life, tutapambana hadi mwisho.
 
Acha kife tuu mana tumechoka kuwa wapumbavu kiasi hicho hapa nchini!:fencing:

CCM lazima ife, isipokufa Na ikaendelea kutawala mjue baada ya miaka kumi mingine hatutakuwa na hii nchi
 
Ndugu wanabodi,
Sasa inaonekana dhahiri kwamba CCM Kama chama cha siasa kimekwishakufa.
Imebakia CCM inayoishi kwa nguvu ya dola kwa sababu CCM imekwishapoteza ushawishi wake kwa umma wa wakulima, Wafanyakazi na wafanyabiashara.

Kuna
matukio mengi yanayodhihirisha hili na hata sina haja ya kutoa mifano. Kwa bahati mbaya chama hiki kimejiingiza hadi kwenye kile wanasiasa wapenda haki, wanademokrasia na watetezi Wa haki za binadamu wanaita matumizi mabaya ya madaraka na vyombo vya dola na wakati mwingine kuua wananchi wake ili kudhibiti vyama vya upinzani Na harakati za wananchi kudai haki zao.

Wachunguzi Wa mambo ya kisiasa wanasema hali hii inaweza kupelekea rais aliyeko madarakani na viongozi wakuu Wa serikali Na vyombo vya usalama kufikishwa the Hague pindi watakapokuwa hawako madarakani.

Kwa hali ya kisiasa na vuguvugu iliyopo nchini ya wananchi wengi kutaka mabadiliko, CCM haiwezi tena kuendelea kuwepo bila nguvu hii ya vyombo vya dola kwa sababu CCM imekosa ushawishi wa kisiasa Na wananchi hawana tena imani Na chama hiki tawala.

Hali hii inamaanisha kwamba sasa hivi CCM imejivika gamba jingine la chama cha kiimla ( ki-dictator). Wachunguzi wa mambo wanasema chama cha siasa kinapofikia hali hii basi kinakuwa katika dakika za mwisho za utawala na kinachofuata ni kusambaratika.

Hii hali si salama kwa wananchi na vile vile si salama hata kidogo kwa CCM yenyewe.
U-dictator huu umeanza kusababisha mgawanyiko ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi wa nchi kama vile polisi, UWT na jeshi la wananchi. Haya makundi ndani ya vyombo vya usalama vile vile yamechagiwa pia kwa kuwepo makundi ya kuwania urais ndani ya chama tawala cha kidictator na kuwepo kwa chama cha upinzani-CHADEMA chenye nguvu na ushawishi Mkubwa kwa wananchi kuliko hata serikali Na chama tawala. Katika hali hii kila kundi linajitahidi kuwa na uungwaji mkono ndani ya vyombo vya usalama. Mpaka sasa hivi kuna makundi makubwa manne ndani ya vyombo vya usalama, kundi la nne likiwa ni la chama kikubwa cha upinzani yaani Chadema. Hata hivyo kuna kundi lingine ambalo halina upande na liko tayari kufanya kazi na kundi lolote litakaloingia madarakani 2015.

Chama kikuu cha upinzani kimeweza kujipatia uungwaji mkubwa wa wananchi wanaopenda mabadiliko na vile vile kuwa na uungwaji mkubwa ndani ya vyombo vya usalama. Hata hivyo serikali na chama tawala vimekuwa kwenye harakati za ku brain wash watu wa usalama hasa watendaji wakuu ili wajione kwamba wao ni part ya serikali inayo fail ya chama cha mapinduzi na kwamba kama CCM itashindwa uchaguzi basi na wao watanyang'anywa nyadhifa zao. Watendaji hawa wamekuwa vile vile wakidanganywa na kuaminishwa kwamba ni wajibu wao kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi kwa kutumia mbinu hata zisizo halali ili kubaki madarakani.

Ukweli ni kwamba vyombo vya usalama vinawajibika kulinda serikali ilivyo madarakani isiondolewe kwa njia zisizo za kidemokrasia kama vile mapinduzi.

Vyombo vya usalama haviwajibiki na havipaswi kuzuia demokrasia au kuwa upande wa chama tawala wakati wa uchaguzi.

Kwa Kushika hatamu ya udictator kwa chama tawala imekusudiwa kunyamazisha na kuogopesha wananchi na viongozi Wa vyama vya upinzani wajitoe au wasishiriki kuleta mabadiliko. Hata hivyo hii mbinu inaelekea kushindwa kunyamazisha harakati za nguvu ya umma za kutaka mabadiliko ya kweli. Badala yake hali hii ya vitisho na dhuruma kwa wananchi inasababisha chuki zaidi kwa serikali na inasadikiwa itasababisha wananchi kuwa shupavu zaidi na kuondokana na uoga na kujifunza mbinu za kupambana na nguvu za dhuruma kwa kutumia mbinu zile zile zinazotumiwa na watawala.

Kwa hali ya mgawanyiko ndani ya vyombo vya usalama Wachunguzi wa mambo wanabainisha kwamba kama upinzani utashinda na serikali ikaamua kung'ang'ania madarakani vyombo vya usalama ikiwemo jeshi litagawanyika na kunaweza kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe-Mungu apishie mbali.

CCM imepoteza uwepo wake kama chama cha siasa na kujikita kwenye uimla kwa sababu asilimia kubwa ya watanzania mijini Na vijijini, wasomi Na wasio wasomi hawana tena imani na Chama Cha Mapinduzi kwa chama hiki kushindwa kutekeleza ahadi karibu zote inazotoa kwa wananchi. Pamoja na kutotekelezwa ahadi nyingi hasa zilizoahidiwa wakati wa uchaguzi mwaka 2005 na 2010 bado Kila siku ahadi zingine zinaendelea kutolewa.

Licha ya kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, CCM imeendeleza siasa za ubabe na propaganda za uongo. Kwa sababu mambo mengi ambayo CCM inadai kuyatekeleza kwa wananchi hayapo, sasa hivi makada wa chama tawala wamelazimishwa na Katibu Mkuu (kwa kufuata maelekezo ya mwenyekiti) kwenda vivijini kuwaonyesha wananchi maendeleo.

Hizi jitihada zinaekekea kugonga mwamba kwani pamoja na wananchi kulazimishwa waone maendeleo wanashindwa kuyaona kwa sababu Hali zao zimezidi kuwa HOI.

Umasikini umewazidia kiasi wengi wao hata kula mlo mmoja kwa siku inakuwa ngumu.
Ardhi yao imezidi kuporwa na serikali kwa visingizio mbali mbali kama uwekezaji wa kilimo cha kisasa, kulima mivono (ardhi nyingi inatolewa na serikali kusaidia nchi nyingine wapate mafuta), na vile vile wananchi wakulima wengi wananyang'anywa ardhi yao na kuuziwa matajiri kwa kisingizio cha mipango miji.
Jambo la kushangaza ni kwa nini hawa wawekezaji wa mashamba wasiuziwe ardhi isoyokaliwa au kutumiwa na watu ilhali Tanzania kuna ardhi nyingi isiyotumika!

Wafanyakazi wameendelea kufanyakazi kwa malipo madogo ambayo yamekuwa hayakidhi hata kununulia chakula! Bei za vyakula Na bidhaa zimeendelea kuwa juu na kufanya Wafanyakazi wengi Na wakulima kushindwa kumudu bei.
Hata mijini wananchi wameendelea kunyanyaswa na kufukuzwa kwenye maeneo yao kwa sababu mbali mbali.
Wamachinga nao wameendelea kunyanyaswa kwa kufukuzwa kila wanapokwenda bila kupewa mipango endelevu.

Rushwa Na ufisadi vimeendelea kushamiri na kuwa ndiyo sera rasmi ya serikali Na chama tawala. Chama tawala kimeshindwa vita dhidi ya ufisadi baada ya kushindwa kujivua gamba. Ufisadi wa rasilimali za nchi umewafanya wananchi kuwa maskini zaidi kwa kuporwa rasilimali zao Na haki yao.

Hali ya usalama wa wananchi imezidi kuwa tete na Polisi wamebakia kulinda usalama wa viongozi na kudhibiti mikutano ya vyama vya upinzani.

Watu wengi hasa vijana hawana kazi kwa sababu serikali yenyewe iliamua kuua viwanda na kugeuza nchi kuwa ya wachuuzi.

Pamoja na ardhi nzuri na mito na Maji ya kutosha serikali yenyewe iliamua kutotilia maanani kilimo cha kisasa wakati ikielewa wananchi wengi wanategemea kilimo na kilimo kingeweza kutoa ajira isiyo kikomo kwa wananchi.

Watoto wengi Wa wakulima na Wafanyakazi wameshindwa kusoma kwa kukosa mikopo na wengi wanaosoma vyuoni ni watoto wa mafisadi au ambao wazazi wao wana uwezo mkubwa kifedha.

Kwa ujumla badala ya serikali kuongoza wananchi wake ili kuleta maendeleo ya watu na nchi yao kwa kutumia rasilimali lukuki tulizojaliwa na nwenyezi mungu, serikali Imefeuka na kuwa dalali wa kugawa rasilimali za nchi yetu kwa wageni!

Kwa yote haya na mengine mengi ambayo sijayataja hapa serikali ya CCM imekwishapoteza uhalali wa kuongoza nchi na ni vizuri ikajiandaa kuachia madaraka kwa njia ya Amani mwaka 2015.
Tuanzie kuorodhesha tuhuma kwa umakini na ushahidi hata kama mahakama za kangaroo aka magamba zilitoa maamuzi:
1. Ulimboka alikamatwa akapigwa na watuhumiwa wakalindwa na kufichwa. Pia mfumo wa mahakama ukatumika kufunika malalamiko pale alipokamatwa taahira na kusema "jambo liko mahakamani"
2. Arusha watanzania walipigwa risasi wakauawa- Mfumo Kangaroo ukakamata watanzania wengine ili kuficha mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola.
3. Mwangosi aliuawa ikaundwa tume ya "kikangaroo" na kufukia ukweli.
4. Tarime wananchi waliuawa kama mbuzi pori na majeneza yakaporwa na miili ikaibwa na kutupwa mabarabara na polisi wa "kikangaroo"
5. Mwanza viongozi wa upinzani walivamiwa na kukatwa mapanga mbele polisi wa "kikangaroo"
Tuoredheshe mkuu sasa kwa sababu mengi yanakuja maji yanapowafika shingoni watapigana na kuua tena na tena. Tuendelee kukusanya takwimu na ushahidi!!
 
Mkuu haya yote na mengine mengi yako kwenye kumbukumbu. CCM wanahangaika sana na dr Slaa kwa sababu wanadhani ni yeye pekee anayeweza kuwapeleka The Hague na wakishindana nae katika urais wana uhakika wa kushindwa. Wao wanaamini wengine wote wanaweza kununulika.

Wamejaribu sana kumnunua dr Slaa, wameshindwa. Lakini wanajidanganya! Sasa hivi M4C ni zaidi ya mtu mmoja. Kitu cha kujivunia ni kwamba sasa hivi katika CHADEMA kuna kina dr Slaa wengi wasiohesabika.
 
Kada wa kutegemewa amepigwa ban kwa id zote

W. J. Malecela
user-offline.png

Banned
verified.png

reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Field Marshall ES
user-offline.png

Banned
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
 
Kada wa kutegemewa amepigwa ban kwa id zote

W. J. Malecela
user-offline.png

Banned
verified.png

reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



Field Marshall ES
user-offline.png

Banned
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Mkuu Ina maana W. J. Malecela na Field Marshall ES kila mmoja an ID's zote hizo!
 
Kama W. J. Malecela na Field Marshall wamepigwa ban ni sahihi kabisa, Hasa huyu Le Mutuz amekuwa akiandika habari za uongo na za uzushi hata mimi kama ningekuwa mod ningempa ban tena ya muda usiojulikana
 
Ni kweli Mkuu, kumbe alijiita Field Marshall akitaka kuungwa mkono kama kamanda mpambanaji kumbe alikuwa ni kenge katika msafara Wa mamba. Sasa amerudi kwa magamba wenzake
 
Back
Top Bottom