CCM Kusambaratika!

CCM Kusambaratika!

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,217
Reaction score
426
Ndugu wanabodi,
Sasa inaonekana dhahiri kwamba CCM Kama chama cha siasa kimekwishakufa.
Imebakia CCM inayoishi kwa nguvu ya dola kwa sababu CCM imekwishapoteza ushawishi wake kwa umma wa wakulima, Wafanyakazi na wafanyabiashara.

Kuna
matukio mengi yanayodhihirisha hili na hata sina haja ya kutoa mifano. Kwa bahati mbaya chama hiki kimejiingiza hadi kwenye kile wanasiasa wapenda haki, wanademokrasia na watetezi Wa haki za binadamu wanaita matumizi mabaya ya madaraka na vyombo vya dola na wakati mwingine kuua wananchi wake ili kudhibiti vyama vya upinzani Na harakati za wananchi kudai haki zao.

Wachunguzi Wa mambo ya kisiasa wanasema hali hii inaweza kupelekea rais aliyeko madarakani na viongozi wakuu Wa serikali Na vyombo vya usalama kufikishwa the Hague pindi watakapokuwa hawako madarakani.

Kwa hali ya kisiasa na vuguvugu iliyopo nchini ya wananchi wengi kutaka mabadiliko, CCM haiwezi tena kuendelea kuwepo bila nguvu hii ya vyombo vya dola kwa sababu CCM imekosa ushawishi wa kisiasa Na wananchi hawana tena imani Na chama hiki tawala.

Hali hii inamaanisha kwamba sasa hivi CCM imejivika gamba jingine la chama cha kiimla ( ki-dictator). Wachunguzi wa mambo wanasema chama cha siasa kinapofikia hali hii basi kinakuwa katika dakika za mwisho za utawala na kinachofuata ni kusambaratika.

Hii hali si salama kwa wananchi na vile vile si salama hata kidogo kwa CCM yenyewe.
U-dictator huu umeanza kusababisha mgawanyiko ndani ya vyombo vya usalama na ulinzi wa nchi kama vile polisi, UWT na jeshi la wananchi. Haya makundi ndani ya vyombo vya usalama vile vile yamechagiwa pia kwa kuwepo makundi ya kuwania urais ndani ya chama tawala cha kidictator na kuwepo kwa chama cha upinzani-CHADEMA chenye nguvu na ushawishi Mkubwa kwa wananchi kuliko hata serikali Na chama tawala. Katika hali hii kila kundi linajitahidi kuwa na uungwaji mkono ndani ya vyombo vya usalama. Mpaka sasa hivi kuna makundi makubwa manne ndani ya vyombo vya usalama, kundi la nne likiwa ni la chama kikubwa cha upinzani yaani Chadema. Hata hivyo kuna kundi lingine ambalo halina upande na liko tayari kufanya kazi na kundi lolote litakaloingia madarakani 2015.

Chama kikuu cha upinzani kimeweza kujipatia uungwaji mkubwa wa wananchi wanaopenda mabadiliko na vile vile kuwa na uungwaji mkubwa ndani ya vyombo vya usalama. Hata hivyo serikali na chama tawala vimekuwa kwenye harakati za ku brain wash watu wa usalama hasa watendaji wakuu ili wajione kwamba wao ni part ya serikali inayo fail ya chama cha mapinduzi na kwamba kama CCM itashindwa uchaguzi basi na wao watanyang'anywa nyadhifa zao. Watendaji hawa wamekuwa vile vile wakidanganywa na kuaminishwa kwamba ni wajibu wao kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi kwa kutumia mbinu hata zisizo halali ili kubaki madarakani.

Ukweli ni kwamba vyombo vya usalama vinawajibika kulinda serikali ilivyo madarakani isiondolewe kwa njia zisizo za kidemokrasia kama vile mapinduzi.

Vyombo vya usalama haviwajibiki na havipaswi kuzuia demokrasia au kuwa upande wa chama tawala wakati wa uchaguzi.

Kwa Kushika hatamu ya udictator kwa chama tawala imekusudiwa kunyamazisha na kuogopesha wananchi na viongozi Wa vyama vya upinzani wajitoe au wasishiriki kuleta mabadiliko. Hata hivyo hii mbinu inaelekea kushindwa kunyamazisha harakati za nguvu ya umma za kutaka mabadiliko ya kweli. Badala yake hali hii ya vitisho na dhuruma kwa wananchi inasababisha chuki zaidi kwa serikali na inasadikiwa itasababisha wananchi kuwa shupavu zaidi na kuondokana na uoga na kujifunza mbinu za kupambana na nguvu za dhuruma kwa kutumia mbinu zile zile zinazotumiwa na watawala.

Kwa hali ya mgawanyiko ndani ya vyombo vya usalama Wachunguzi wa mambo wanabainisha kwamba kama upinzani utashinda na serikali ikaamua kung'ang'ania madarakani vyombo vya usalama ikiwemo jeshi litagawanyika na kunaweza kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe-Mungu apishie mbali.

CCM imepoteza uwepo wake kama chama cha siasa na kujikita kwenye uimla kwa sababu asilimia kubwa ya watanzania mijini Na vijijini, wasomi Na wasio wasomi hawana tena imani na Chama Cha Mapinduzi kwa chama hiki kushindwa kutekeleza ahadi karibu zote inazotoa kwa wananchi. Pamoja na kutotekelezwa ahadi nyingi hasa zilizoahidiwa wakati wa uchaguzi mwaka 2005 na 2010 bado Kila siku ahadi zingine zinaendelea kutolewa.

Licha ya kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, CCM imeendeleza siasa za ubabe na propaganda za uongo. Kwa sababu mambo mengi ambayo CCM inadai kuyatekeleza kwa wananchi hayapo, sasa hivi makada wa chama tawala wamelazimishwa na Katibu Mkuu (kwa kufuata maelekezo ya mwenyekiti) kwenda vivijini kuwaonyesha wananchi maendeleo.

Hizi jitihada zinaekekea kugonga mwamba kwani pamoja na wananchi kulazimishwa waone maendeleo wanashindwa kuyaona kwa sababu Hali zao zimezidi kuwa HOI.

Umasikini umewazidia kiasi wengi wao hata kula mlo mmoja kwa siku inakuwa ngumu.
Ardhi yao imezidi kuporwa na serikali kwa visingizio mbali mbali kama uwekezaji wa kilimo cha kisasa, kulima mivono (ardhi nyingi inatolewa na serikali kusaidia nchi nyingine wapate mafuta), na vile vile wananchi wakulima wengi wananyang'anywa ardhi yao na kuuziwa matajiri kwa kisingizio cha mipango miji.
Jambo la kushangaza ni kwa nini hawa wawekezaji wa mashamba wasiuziwe ardhi isoyokaliwa au kutumiwa na watu ilhali Tanzania kuna ardhi nyingi isiyotumika!

Wafanyakazi wameendelea kufanyakazi kwa malipo madogo ambayo yamekuwa hayakidhi hata kununulia chakula! Bei za vyakula Na bidhaa zimeendelea kuwa juu na kufanya Wafanyakazi wengi Na wakulima kushindwa kumudu bei.
Hata mijini wananchi wameendelea kunyanyaswa na kufukuzwa kwenye maeneo yao kwa sababu mbali mbali.
Wamachinga nao wameendelea kunyanyaswa kwa kufukuzwa kila wanapokwenda bila kupewa mipango endelevu.

Rushwa Na ufisadi vimeendelea kushamiri na kuwa ndiyo sera rasmi ya serikali Na chama tawala. Chama tawala kimeshindwa vita dhidi ya ufisadi baada ya kushindwa kujivua gamba. Ufisadi wa rasilimali za nchi umewafanya wananchi kuwa maskini zaidi kwa kuporwa rasilimali zao Na haki yao.

Hali ya usalama wa wananchi imezidi kuwa tete na Polisi wamebakia kulinda usalama wa viongozi na kudhibiti mikutano ya vyama vya upinzani.

Watu wengi hasa vijana hawana kazi kwa sababu serikali yenyewe iliamua kuua viwanda na kugeuza nchi kuwa ya wachuuzi.

Pamoja na ardhi nzuri na mito na Maji ya kutosha serikali yenyewe iliamua kutotilia maanani kilimo cha kisasa wakati ikielewa wananchi wengi wanategemea kilimo na kilimo kingeweza kutoa ajira isiyo kikomo kwa wananchi.

Watoto wengi Wa wakulima na Wafanyakazi wameshindwa kusoma kwa kukosa mikopo na wengi wanaosoma vyuoni ni watoto wa mafisadi au ambao wazazi wao wana uwezo mkubwa kifedha.

Kwa ujumla badala ya serikali kuongoza wananchi wake ili kuleta maendeleo ya watu na nchi yao kwa kutumia rasilimali lukuki tulizojaliwa na nwenyezi mungu, serikali Imefeuka na kuwa dalali wa kugawa rasilimali za nchi yetu kwa wageni!

Kwa yote haya na mengine mengi ambayo sijayataja hapa serikali ya CCM imekwishapoteza uhalali wa kuongoza nchi na ni vizuri ikajiandaa kuachia madaraka kwa njia ya Amani mwaka 2015.
 
Unawapa shida kina Mafilili (na wote wanaotumikia mafisadi) ndugu! Kuthibitisha hilo subiri waje hapa ujionee watakachosema!
 
Mkuu umesomeka vizuri, japo najua watakuja wafuasi wa NAPE hapa na kubisha huku mishipa ya shingo ikiwa imewatoka huko walipo, lakini ndio ukweli wenyewe CCM ni mkosi katika NCHI hii kwa sasa, wamefanya waliyofanya, kwa yale mema tunawashukuru na tutayaendeleza hayo mengine tutaona jinsi ya kuyaweka sawa wakiwa wameshatoka madarakani wakati huo.
 
Kufa sio ishu, ishu ni kutangulia time will tell everything happen for a reason
 
Kama CCM kufa ni sawa lakini 2015 CCM lazima itashinda uchaguzi hasa kwa ujinga wa Chadema kubweteka na watu kama wewe kuwa na matamanio ya ushindi 2015 bila kujipanga,Chadema bado haipo kwenye grass root,juzi tumeshudia Chadema ikipigwa kwenye udiwani kwa kupata viti 5 na CCM wakizoa viti 22! Matamanio ya kisiasa yasiwe kipeumbele na kuji sifia kushinda wakati mkakati wa chini haupo,Chadema bado ina kazi kuishinda CCM ila kwa kujifariji unaweza sema Chadema itashinda 2015
 
Hapa Nape na Malecela hoi.

Ngoja tuwasubiri, hawakosi la kusema kwa sababu wao na chama chao ni watu wa propaganda tu bila utendaji. Wakifanya kitu ujue wamepata msaada na waliotoa msaada wamesimamia msaada usiliwe
 
CCM inasabaratika na CDM nayo inasambaratika kwaiyo 2015 Lipumba ndio anatinga Ikulu?
 
Kama CCM kufa ni sawa lakini 2015 CCM lazima itashinda uchaguzi hasa kwa ujinga wa Chadema kubweteka na watu kama wewe kuwa na matamanio ya ushindi 2015 bila kujipanga,Chadema bado haipo kwenye grass root,juzi tumeshudia Chadema ikipigwa kwenye udiwani kwa kupata viti 5 na CCM wakizoa viti 22! Matamanio ya kisiasa yasiwe kipeumbele na kuji sifia kushinda wakati mkakati wa chini haupo,Chadema bado ina kazi kuishinda CCM ila kwa kujifariji unaweza sema Chadema itashinda 2015

CCM haiwezi kushinda bila hujuma Na kusaidiwa na vyombo vya usalama na tume usiyo huru.

Wewe ndie unajidanganya na ushindi feki wa CCM
 
Kama CCM kufa ni sawa lakini 2015 CCM lazima itashinda uchaguzi hasa kwa ujinga wa Chadema kubweteka na watu kama wewe kuwa na matamanio ya ushindi 2015 bila kujipanga,Chadema bado haipo kwenye grass root,juzi tumeshudia Chadema ikipigwa kwenye udiwani kwa kupata viti 5 na CCM wakizoa viti 22! Matamanio ya kisiasa yasiwe kipeumbele na kuji sifia kushinda wakati mkakati wa chini haupo,Chadema bado ina kazi kuishinda CCM ila kwa kujifariji unaweza sema Chadema itashinda 2015

Unasahau (au umechagua kusahau) yafuatayo:

1: Ccm pamoja na kushinda Viti 22 hawakuweza kuwapokonya CHADEMA hata kiti kimoja walichokuwa wanakishikilia awali (wakati CHADEMA) walifanikiwa kuwanyang'anya ccm Vito walivyokuwa navyo awali

2: Hata pale ccm waliposhinda tofauti ya kura ilikuwa ndogo.
 
Wewe ndiye utasambatika ccm itaendelea kudumu na kutawala daima ccm oyeeeeeee
 
Thank you very much Blueray , nimekugongea like kubwa sana , andiko lako limejaa ukweli mtupu , if someone in our country did not see about what you said , He/She may not be a human .
 
Wewe ndiye utasambatika ccm itaendelea kudumu na kutawala daima ccm oyeeeeeee

CCM itaendelea kukutawala wewe mwenyewe kwa sababu imekwishakudumaza akili na upeo wako wa kufikiri
 
Unasahau (au umechagua kusahau) yafuatayo:

1: Ccm pamoja na kushinda Viti 22 hawakuweza kuwapokonya CHADEMA hata kiti kimoja walichokuwa wanakishikilia awali (wakati CHADEMA) walifanikiwa kuwanyang'anya ccm Vito walivyokuwa navyo awali

2: Hata pale ccm waliposhinda tofauti ya kura ilikuwa ndogo.

Kweli Mkuu, tena kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ushindi wa kupewa na tume yao baada ya kukataa hata kurekebisha daftari la wapiga kura.
 
Kama CCM kufa ni sawa lakini 2015 CCM lazima itashinda uchaguzi hasa kwa ujinga wa Chadema kubweteka na watu kama wewe kuwa na matamanio ya ushindi 2015 bila kujipanga,Chadema bado haipo kwenye grass root,juzi tumeshudia Chadema ikipigwa kwenye udiwani kwa kupata viti 5 na CCM wakizoa viti 22! Matamanio ya kisiasa yasiwe kipeumbele na kuji sifia kushinda wakati mkakati wa chini haupo,Chadema bado ina kazi kuishinda CCM ila kwa kujifariji unaweza sema Chadema itashinda 2015

Waambie waache kuchakachua katika chaguzi uone kama watatoka na kiti hata kimoja. Usiringie hivyo viti mlivyovipata kwa kuchakachua
 
Back
Top Bottom