Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,543
- 664
Hizi taratibu ni jitahada za kujizuia na kimbunga kinachoendelea. Wasisahau kuwa ukizuia leo kesho itakuwa upande wa pili nawe ndiye utakayeumia.
Kushinikiza kuwa uchaguzi ufanyike siku moja ni kupitisha njia ya kushinda kwa mbinu ili kuwazuia watu wenye kupendwa na wananchi lakini wasiotakiwa na chama husika kuchinjiwa baharini.
Suala la chama kilichoshinda kuchagua mrithi endapo kifo kitatokea, pia ni njia ya kuwanyima watu haki, kwani anaechaguliwa ni mtu kupitia chama, na pale anapofariki uwakilishi unakuwa umekwisha. Labda kama huyo mwakilishi anawakilisha chama na sio watu. Pili, endapo tutapitisha sheria ya mgombea binafsi, nae akifariki atapatikana kwa utaratibu upi?
Ni kweli kuwa chaguzi ni gharama. Lakini ni haki ya msingi, kinachotakiwa ni sheria itakayoainisha kiwango cha fedha ikiwa ni pamoja na team ya kampeni. Timu isiyozidi watu 5-10