CCM kupendekeza mfumo mpya wa uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kupendekeza mfumo mpya wa uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Dec 1, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uchaguzi ambao mbunge au diwani akifa au kujiuzulu hakutahitajika uchaguzi mdogo. Badala yake katika mfumo huo (proportional representation) unaotumika pia Marekani na Afrika Kusini, chama kilichoshinda katika jimbo husika, kitapewa mamlaka ya kuteua mwanachama wa kurithi nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia orodha ya wanachama wake.

  Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifafanua utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Aprili mwaka huu na kufafanua kuwa, mfumo huo utasaidia kupunguza usumbufu na gharama za kurudia uchaguzi. Mbali na mfumo huo, pia kinafikiria kupendekeza kuanzishwa kwa mfumo mwingine wa uteuzi wa wagombea wa vyama ambao Mukama alisema unatumika Ujerumani, ambapo vyama vyote vya siasa vitatakiwa kuteua wagombea wake siku moja.

  Alikiri kuwa sababu ya mfumo huo mpya wa uteuzi wa wagombea wa vyama, ni kuzuia tabia ya baadhi ya vyama kusubiri uteuzi wa chama kimoja na kuchukua wagombea wa chama hicho walioachwa. "Huwezi kukaa kusubiri wanaokataliwa na CCM, kwa sasa tunamfumo wa uteuzi sawa na ule wa kupanga magoli (mfumo unaotumiwa na vilabu vya soka kupanga matokeo kumpata mshindi)," alisema Mukama.

  Chama hicho pia kwa mujibu wa Mukama, kinafikiria kuwafikisha katika vyombo vya kisheria watu waliokituhumu kuwa kimetumia zaidi ya Sh bilioni 3 katika uchaguzi mdogo wa Igunga. Mukama ambaye alikataa kutaja fedha zilizotumiwa na chama hicho katika uchaguzi huo, alisema taarifa hizo za kutumia fedha nyingi, zililenga kukifitinisha chama hicho kwa wananchi.

  HabariLeo | CCM kupendekeza mfumo mpya wa uchaguzi
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hili pendekezo la CCM vipi? Kuwa mbunge au diwani akifa au kujiuzulu hakutahitajika tena uchaguzi mdogo na badala yake chama kilichoshinda katika jimbo husika, kitapewa mamlaka ya kuteua mwanachama wa kurithi nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia orodha ya wanachama wake?
   
 3. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwani wananchi huwa wanachagua chama au mgombea?kama wanachagua chama ni sawa,lakini kamawanamchagua mgombea wana ihakika gani wa huyo watakempa kama ndiye wananchi wanaemtaka?Huu ni woga wa kupoteza viti wakati uchaguzi unaporudiwa.Na ni uhuni wa kufifisha demokrasia.demokrasia haina usumbufu,usumbufu wanaouona ndio Demokrasia yenyewe.Waache Uhuni wao hapa!
   
 4. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Chama muhimu ikumbukwe kwamba tunapofanya uchaguzi wa Mgombea wakati wa Uchaguzi Mkuu tunaangalia Materiality ya Mgombea na Sio chama kilichomsimamisha. Ndiyo maana unaweza ukaona leo jimbo hili linawakilishwa na CDM, next election CCM and son on. So Utaratibu wa Wilson Mukama kwamba Chama Kilichofiwa na Mbunge au Diwani kipewe fursa ya kuteua mwakilishi hadi next General Election ni kuwapora fursa wananchi husika haki yao ya kikatiba ya kuchagua mwakilishi wanaemtaka. Hii pia inaingiza dhana kwamba wananchi huwa wanachagua Chama badala ya Mgombea wakati wa Uchaguzi Mkuu dhana ambayo ni Potofu. Hili wazo la Mukama nalipinga kwa nguvu zote.
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hawana lolote hao zaidi ya kuogopa muziki ambao huwa wanaupata pale inapotakiwa uchaguzi urudiwe. Mapambano ya hoja kama ya igunga ni tatizo kubwa kwao!!
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Pengine wangesema chama/mgombea aliyeshika nafasi ya pili achukue nafasi husika ingekuwa nafuu, kuliko hilo pendekezo lake lisillokubalika. Hata hivyo, tatizo la hii pendekezo la kwangu ni kwamba aliyeshika nafasi ya pili atakuwa anamwombea mabaya mgombea aliyeshinda au kumzushia kashfa ili chama chake kikimfukuza yeye achukue nafasi.
   
 7. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Ilo la kupunguza gharama naona ni sahii kabisa. Ila nahisi CCM wamejiona wapo kwenye hali mbaya. Sasa wanaona hatakapo kufa mbunge au diwani,na uchaguzi ukarudiwa yawezekana isishinde. Na hii yote ni kwa sababu ya yaliyotokea Igunga. Na yanayotokea maeneo mengine ambapo uchaguzi wa madiwani uliporudiwa baada ya diwani kuachia madaraka au kufa wapinzani wameshinda.
   
 8. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Michael nakubali kwamba wangetaka ,wangesema aliyeshika nafasi ya pili ambaye kwa vyovyote vile kama kilishinda CCM wa pili ni lazima awe upinzai.sasa wangependa iwe hivyo?Lakini pia nafikiri wameishaanza kuhisi kupoteza watu wao wengi kwa hiyo kuhatarisha mustakabali wa chama chao.Maana hii minyukanoinayoendelea ndani ya chama ina ashiria kupoteza wapiganaji wao wengi.hivyo wameanza kujihami mapema.watamalizana sana na hivyo the only solution ni kuhakikisha wanajihakikishia zile nafasi walizo nazo wanazilinda.
   
 9. KASSON

  KASSON Senior Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  KICHEKESHO!kumbe leo umegundua kuna gharama,lakini hela zinazochukuliwa na Mafisadi ni nyingi kuliko hizo unazosema za kurudia uchaguzi jimboni,Maliza la Ufisadi kwanza ndio uje kwenye hili.
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huwezi pia kumchukua mshindi wa pili kwa sababu nae ana sifa ya kukataliwa na Wananchi dhidi ya mshindi wa kwanza na ndiyo maana akaambulia nafasi ya pili. Ili kukidhi dhana ya demokrasia na haki ya katiba ya wanananchi kumchagua mgombea wanaemtaka, Uchaguzi mdogo haukwepeki. Tatizo CCM wanakwepa Uchaguzi mdogo kwa sababu wanamatumizi makubwa ambayo si ya lazima na pia kutokuwa na hoja kwa wananchi wakati wa kampeni dhini ya wapinzani wao wakuu CDM.
   
 11. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm sasa hivi hawahitaji tena mambo ya kupigiwa kura,wameshaona wapiga kura hawaitaki CCM tena.Wanachokifanya ccm ni kuondoa mazingira ya kitu kinachoitwa KURA kwao.Na bado watakuja na proposal za ajabu kupita kiasi.Tusubili tuone,yetu macho na masikio.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo mkuu ni kwamba hawa jamaa wa CCM siku zote hufikiria irrationally wakidhania wao wataendelea kuwa majority!!!!! Ndiyo maana hata ishu ya katiba wanaifikiria ki-CCM CCM.
   
 13. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hilo la kuzuia chaguzi ndogo ni ubatili. Wanaogopa wapiga kura, wanajua wanayoyafanya yanawachukiza wapiga kura.

  Hilo la uteuzi wa wagombea kwa siku moja nalo ni ubatili. Hawataki kukubali uwepo wa kivuli chao wenyewe? Ukweli utabaki kuwa ccm haikubaliki, ile dhana ya kujiunga ccm ili ushinde uchaguzi imefika mwisho. Watu makini wanagombea kupitia upinzani wa leo.

  Mabadiliko ya katiba yangekuwa kwa manufaa ya wananchi, kuanzia kwenye mchakato, tungepata tume huru ya uchaguzi na fursa ya kuwa na wagombea binafsi. Kwa kuwa katiba haitakuwa ya wananchi bali ya watawala, kama itapatikana, basi fursa ya mabadiliko itafanywa na uongozi ujao kupitia chama mbadala. Hayo mawazo ya mukama na ccm yake yatakuwa yamezikwa.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Huyu Mukama asitudanganye hapa. Ni kweli Afrika ya kusini wan mfumo wa proportinal represantation, lakini mfumo wao ambao pia unatumika kwenye nchi kama Namibia hauchagui mtu bali ni chama. Kinachofanyika kila chama kinapendekeza majina ya wabunge wake kufuatana na idadi ya bunge zima (Kama ni bunge la watu 100, kila chama kinapendekeza majina 100). Kwa maana hiyo hakuna majimbo ya uchaguzi kama kwetu.

  Kwa ufumo anaousema wa RSA, kwa jinsi JK alivyoibuka na 60 % ina maana CCM walitakiwa wawe na 60% ya wabunge. Kitu ambacho najua CCM hawako kukifanya. Wanataka mfumo unaowafavor wao tu. Anyway, hilo ni swala la katiba mpya.
   
 15. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Je tutakapokuwa na mgombea huru asiye na chama na akafariki au akaugua kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu bungeni itakuwaje? CCM wasituletee janja yao hapa, wanataka kuzuia wagombea binafsi!

  Mfumo wa "representation" kama anaosema Mukama hafuai kwenye nchi yenye siasa za udini, ukabila na za hongo ya ngono kama TZ. Tumeona tu nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais na wabunge wa viti maalamu zilivyotumika vibaya. Au wakuu wa mikoa na wilaya! Leo badala ya rais kuteua "technocrats" watakaomsadia kuendesha nchi anateua "maswaiba" wake!

  CCM wameanza kuogopa uamuzi wa wananchi kupitia kura, kwa kuwa inaonekana hata tume ya uchaguzi itashindwa kuchakachua kuipa ushindi kwa jinsi wananchi wlivyopata mwanko wa kuwa na chaguzi huru na za haki! Kama wanadhani demokrasia ni ghali basi wajaribu "anarchy" utawala wa vurugu usiojali sheria "anarchism" ni ghali mara kumi ya demokrasia...
   
 16. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa sasa mwisho watapendekeza kuwe na mgombea mwenza ktk ubunge
   
 17. i

  ibange JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni upuuzi mtupu. Hata mfanyeje hamtaweza kuiokoa ccm
   
 18. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hamna mantiki labda tungekuwa tunachagua wabunge kwa propotional ya kura za kila chama kuliko ilivyo sasa.
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  haya mazee kweli yamefilisika maana yanaongea mautumbo ya bata tu hapa
   
 20. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mbona sioni tatizo kwa chaguzi ndogo ila angezungumzia tatizo la wabunge kutofautiana kimtazamo na vyama vyao kama akifukuzwa anaondoka na ubunge wake hapo ningemwelewa.. ccm kingekuwa na adabu kwa wabunge na wanachama wake.
   
Loading...