CCM kumekucha: Raila Odinga sasa amponza Magufuli!

CCM kumekucha: Raila Odinga sasa amponza Magufuli!

Kiukweli Dr.John Pombe katuangusha sana baadhi ya mashabiki wake tunaoguswa sana na uchapakazi wake.Ni kiongozi ambaye kwa kweli tulishaanza kumuona kama mmoja wa watanzania wanastahili kupewa dhamana ya kuliongoza taifa katika awamu ya tano ya utawala wa taifa letu.Sasa katika hili watu makini lazima tukiri kuwa ni mapungufu makubwa katika suala zima la diplomasia ya kimataifa.Vyovyote iwavyo,kauli inayotolewa na kiongozi mwenye dhamana huwa ina matokeo yake.Yawe mazuri au mabaya.,Kwa hiyo wadau tunapojadili jambo hili, hatumjadili Dr.Magufuli kama yeye.Kinachoangaliwa hapa ni dhamana alizonazo na kile alichokifanya.
Kwa hiyo,kama tunajadili suala hili kwa kuongozwa na miiko ya uongozi, bila shaka tutakubaliana kuwa mh.Waziri kimsingi aliteleza.Na hakuna dhambi katika hilo.Makosa hufanywa na binadamu.Muhimu kwa mh.Waziri kukubali kuwa ni jambo ambalo limeleta utata na mkanganyiko mkubwa si kwa watz tu,bali hata kwa wakenya wenyewe.Hivyo,basi ajitokeza hadharani,bila kumung'unya maneno kuomba radhi.Hoja kwamba alitoa kauli hiyo kama yeye binafsi haina mashiko kabisa ukizingatia kuwa katika mkutano ule hakutambulishwa kama Dr.Magufuli kutoka Tz,bali alitambulishwa kama waziri wa TZ.Hivyo alipokuwa akizungumza wakenya walikuwa wanamsikiliza kama waziri wa serikali ya TZ! Lazima busara imtawale katika hili! Na kwa kuomba radhi haitampuguzia kitu bali zaidi sana atajijengea heshima na kwamba amefanya jambo la kiungwana.
 
Hivi mnafikiri kuwa wote wenye PHD wana hekima pia. Huo ni ukosefu wa hekima na busara!
 
Kumbukeni wiki kadhaa zilizopita Uhuru Kenyatta na Ruto walifika Ikulu ya DAR na kuteta na JK. Vyombo vya habari viliripoti kiduchu. Lakini binafsi naamini walikuwa wanatafuta support ya TZ. Sasa Raila aliona si vizuri kutumia JK ila yeye apitie kwa MAGUFULI pengine si kwa sababu ya urafiki tu lakini vilevile jamaa aliona pengine Dkt. Magufuli anaheshimika hapa TZ, hivyo, akienda KENYA anawezabadilisha upepo wa siasa. Wakati huo huo, DKt. Magufuli alipaswa kumpa msimamo wake kuwa anakwenda lakini inaweza kutoa picha tofauti kwa serikali mbili hizo, kwamba CCM inamtaka RAILA na si wengine, na hapa ndipo alipaswa kutumia busara na si umaarufu! Hata hivyo, hakuomba ruhusa toka kwa MKUU wake wa kazi? Alieleza anakwenda kufanya nini? Je, Wakenya watapata picha gani kwa JK na CCM yake? Hapo hamna urafiki.

Mkuu Kitanga, taarifa zilizopo ni kuwa Mh.Magufuli alipata baraka zote kutoka kwa Waziri Mkuu ambaye ni kiranja wake ndo maana utaona hata hatokei kusema chochote - hapa kila mtu atakuja na lake mwisho wa siku hakuna cha maana!
 
Back
Top Bottom