jjimmy.jjose
Member
- Dec 12, 2012
- 35
- 4
Nimesoma gazeti la leo la Raia Mwema na kukuta kichwa cha habari "Raila Odinga sasa amponza Magufuli" naomba tujadili msitakabali wa Chama cha Mapinduzi. Habari kamili hii hapa:
Raila Odinga sasa amponza Magufuli
"Debe la Kampeni ya urais lazua jambo serikalini"
UAMUZI wa Waziri wa Ujenzi wa Tanzania,Dk.John Magufuli kuungana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai, Kumpigia debe mgombea wa urais wa Kenya, Raila Odinga katika kinyang'anyiro cha urais nchini humo, umezua mijadala ya chini kwa chini ndani ya chama tawala na kwa baadhi ya maofisa waandamizi wa serikali, Raia Mwema, limeelezwa.
Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari Kenya na hapa nchini Decemba 6, mwaka huu, akiwa jijini Nairobi, Waziri Magufuli,aliwaambia wa Kenya Raila anayegombea urais kupitia Chama cha Orange Democratic (ODM), anastahili kuwa Rais wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa Magufuli, Raila anazo sifa za uongozi kwa ngazi hiyo ya urais. Alitoa maelezo hayo katika Mkutano Mkuu wa ODM.
Ni kutokana na uamuzi huo wa Magufuli kumpigia debe la wazi Odinga licha ya kuwa kwamba yeye ni Waziri wa Serikali ya Tanzania ambayo haijatangaza msimano wake kuhusu mgombea wanayemuunga mkono Kenya, mijadala ya ukosoaji dhidi ya Magufuli imeanza kushika moto ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na maofisa waandamizi serikalini.
Kwa mujibu wa mijadala hiyo, kwa muda mrefu sasa haijawahi kutokea Waziri wa Serikali ya Tanzania kuweka wazi msimamo wa kumuunga mkono mgombea urais wa nchi nyingine dhidi ya wagombea wengine. Hata alipowahi kuulizwa na waandishi wa habari wa kimataifa katika Ikulu ya Dar es Salaam, wakati wa ziara ya aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush, Februari mwaka 2008, kwmba angependa nani awe Rais wa Marekani kati wagombea waliokua wakichuana, Barak Obama wa Democrat na John McCain wa Republican, Rais Jakaya Kikwete alijibu kidiplomasia ''Yeyote awaye, Tanzania ipo tayari kufanya kazi naye.''
Katika majibu hayo, Rais Kikwete alikwepa kuonyesha wazi msimamo wa Tanzania tofauti na kiu ya muuliza swali iliyotaka kuhusisha jibu hilo na asili ya Rais Obama kuwa ni Afrika, na hususan Afrika Mashariki. Lakini hali ni tofauti kwa Magufuli ambaye hata hivyo, alikwenda Kenya kwa mwaliko kama rafiki wa Odinga na si kiongozi wa serikali ya Tanzania.
Akiwa Kenya Magufuli alisema;''Nataka kuwaambia Wakenya kwamba Odinga ni mcha Mungu, mnatakiwa kujua hilo. Kama mimi ningekuwa Mkenya mingempigia huyu jamaa kura ili aongoze nchi. Lakini sasa kwa kuwa siruhusiwi hata kupiga kura, basi nawaambia msiache kumchagua huyu atawongozeni vizuri.''
Baadhi ya wakosoaji wa Magufuli wanasema Waziri huyo angeweza kuzungumza katika mkutano huo kwa lugha ya kidiplomasia zaidi kuliko lugha ya moja kwa moja kama alivyofanya. ‘Kuna makosa ya kidiplomasia. Unajua masuala ya kampeni mgombea anatumia kila mbinu kuhakikisha anaonyesha anaaminiwa zaidi ya wenzake hata na serikali za nchi jurani. Kuna uwezekano kampeni za Odinga zikaihusisha Tanzania kwamba inamuunga mkono dhidi ya wagombea wengine wakati si kweli kwamba Tanzania imetangaza msimamo wake.
''Ni makosa haya amefanya Magufuli . Ni kweli amepata mwaliko binafsi lakini haikuwa na ulazima wa kuweka msimamo ule wazi kiasi kile huku akitambua kwamba yeye ni Waziri kitoka Tanzania'' alieleza mmoja wa maofisa waandamizi serikalini.
Lakini mmoja wa viongozi wa CCM amweleza mwandishi wetu kwamba, Magufuli mi Waziri anayetokana na Serikali ya CCM na kwa hiyo, inawezekana baadhi ya Wakenya wakadhani huo pia ni msimamo wa CCM.
''Nadhani hata CCM inabidi watolee ufafanuzi kauli hii ya Waziri Magufuli kumpigia kampeni Raila Odinga. Viongozi wetu ni lazima wajue namna yakuzungumza kwa kuzingatia mahitaji ya wakati na hapa ndipo tunapoweza kupima uwezo wa viongozi wetu kuchambua madhara na faida za kauli zao,'' alisema kiongozi huyo kutoka CCM.
Lakini Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa msimamo wa chama chao kuhusu suala hilo alijibu "Kwa sababu Magufuli ni kiongozi kwa ngazi ya ubunge na Waziri, nadhani watu sahihi wa kuzungumzia hilo kabla ya chama ni Bunge na Serikali kwa maana ya Waziri Mkuu au yeye mwenyewe''
Juhudi za kumtafuta Magufuli kuzungumzia suala hili na hasa kujua kama alitamka kwa kudhamiria na kujua athari zake kwa upande wa serikali yake, hazikuzaa matunda. Hakuweza kupatikana hata kwenye simu yake.
Akiwa katika mkutano huo, Waziri Magufuli alikaririwa akisema kati ya wagombea wote waliojitokeza kuwania kiti cha urais nchini humo, hakuna anayemfikia Odinga na kwamba wakimchagua atawasaidia bila ubaguzi.
Alisema na hata Odinga ambaye ni Waziri Mkuu wa Kenya akiamua kugombea ubunge katika Jimbo lake la Chato (Jimbo la Magufuli), hawezi kumshinda.
"Kwa hiyo nasimama hapa ndugu zangu wana ODM kuwapa pongezi kubwa sana kwa sababu mmechagua jembe" anakaririwa kusema Magufuli.
Katika hali ya kuzuia utata zaidi, Magufuli aliwaambia watuwaliokuwapo katika mkutano huo kwamba baadhi ya wagombea wa urais Kenya hawawezi kufanya ziara nje ya nchi hiyo kutokana na kubanwa na sheria.
Ingawa Magufuli hakuwataja majina, wagombea hao ni pamoja na Uhuru Kenyatta ambaye majuzi ameungana na William Ruto . Wote wawili wanakabiliwa na mashitaka yanayohusishwa na vurugu za uchaguzi Mkuu uliopita nchini Kenya.
Mashitaka dhidi yao yamefunguliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Hague. Uchaguzi Mkuu nchini Kenya unatarajiwa kukfanyika Machi 4, mwakani.
Source: Raia Mwema (Desemba 12-Desemba 18, 2012)