CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

Mwanakijiji mpe kubwa na huyu GT tujinafasi.
 

mwalimu.. ni kama umesoma makala yangu ya kesho!!!!! Watanzania watakisoma hicho unachokisema kesho kwenye Tanzania Daima!
 

Binafsi sijapendekeza "tusubiri" CCM isambaratike. Ninachosema ni kuwa tushiriki ili kuhakikisha inasambaratika. Sisi wananchi ndio tuwe sababu ya wao kumeguka. Mbegu hiyo ukifiria sana tumeshaipanda kwa takribani miaka miwili sasa na pole pole imeanza kuota ndani ya CCM. Haya ya kina Nnauye, Mwakyembe, mama Kilango na wengine hayakutokea hivi hivi.. Tunachotakiwa is to keep watering that "seed of discord".

Njia ya Pili ni hiyo ya Wananchi kuweza kuchukua hatamu wenyewe jambo ambalo sio lazima iwe mapinduzi ya kumwaga damu isipokuwa mapinduzi ya Kifikra..

Hii naamini siyo njia bali ni pre-qualification ya mtu anayetaka kuleta mabadiliko TAnzania. Hatuwezi kuibadili Tanzania kwa kubadili vyama! Tutaweza kuibadili TAnzania kwa kuchochea mabadiliko ya kifikra! Ndio maana nimejipachika ukamanda wa Mapambano ya Kifikra. Fikra duni lazima zioneshwe kuwa ni duni na lazima zishindwe.

Jioni ya leo nilipata nafasi ya kuzungumza na kada wa CCM Tambwe Hizza (kirafiki tu); kuna vitu alisema ambavyo vimenifanya niamini kuwa vile tunavyoandika na kusema si vyote vinaishia kwenye kufungia vitumbua na maandazi. Kuna mbegu inapandwa taratibu na pole pole inakua. Fikra za watu zimeanza kubadilika. Bado tuna safari ndefu hata hivyo ambayo ni lazima tujaribu kuifupisha.

Kama tulikuwa tunatumia punda kutaka kufika huko tunakokwenda, hatuna budi kufikiria kitu kama pikipiki hivi!

Mapinduzi ambayo tumeyaona Mbeya na Tarime, sasa chukulieni kuwa inawezekana Tanzania nzima...

Mkandara, don't be fooled with what happened in Mbeya na Tarime; yaliyotokea yametokana na frustrations and anger not out of an idea; a better idea. Wenzetu wa Marekani walichochagua ni a better idea! (fikra bora).

Jukumu letu kubwa ni kuweza kupandika hili wazo kuwa "we can do better, we have to do better, and yes we must do better"! This my friends is the battlefield.
 
ooh Boy!!!...


Hii mada ni ya 2008...
 
Naam! Huyu ndiye Mzee Mwanakijiji halisi.
 

JF Senior Expert MemberArray


Join Date : 10th March 2006
Location : Kijijini
Posts : 31,744
Rep Power : 87751404
Likes Received24300
Likes Given13220​


[h=2]
Magufuli na CCM Mpasukwa, Lowassa na Matumaini, na Nyota ya CHADEMA[/h]
Wazo: Kufikiria hata kwa mbali kuwa ati Magufuli analeta uongozi mpya toka CCM ni kujikunyata katika usahaulifu. Ni usahaulifu uliopitiliza kudhania kwamba ati kwa kumteua Magufuli CCM sasa imebadilika na kuzaliwa upya! Wengine wamefikia mahali wanaamini ati sasa Magufuli atapita kiulaini tu.


Magufuli kama ilivyokuwa kwa wagombea wengine ndani ya CCM wote wanawakilisha maslahi ya chama tawala. Wote wamekuja na watakuja na mwendelezo (rejea hotuba yake ya kuomba kura) wa dhana zile zile, sera zile zile na mwelekeo ule ule. Alishindwa Kikwete kukiunganisha chama Magufuli ataweza? Nitachambua hili zaidi siku chache zijazo baada ya vumbi walilolitifua Dodoma kutua.


…...
Endapo Lowassa ataenda ACT (kama wengi wetu tumekuwa tukifiria kwa muda sasa tulipozisoma alama za nyakati) CCM itapata shida na maumivu mengine ya kichwa na sidhani kama Magufuli ana dawa ya kuyaponya. Hili linafungua uwezekano mpya kabisa wa ushindi wa CDM na washirika wake katika UKAWA. Sioni ni namna gani watu waliounga mkono CDM miaka yote hii wataweza kumkumbatia Lowassa bila kuonekana ni wanafiki. Sitoshangaa kama Lowassa atapokelewa CDM wengine wanaweza kabisa kuamua kuunga mkono Magufuli ili kuendelea kumkataa Lowassa na mambo yake, ahadi zake na maono yake.


Vyovyote vile ilivyo, Magufuli hawezi kuiokoa CCM iliyogawanyika, iliyopoteza mwelekeo na ambayo ina majeruhi na wengine wanakuja yatakapoanza mambo ya Ubunge. Magufuli ataweza kuzungumza kwa kutaja namba mbalimbali na kA hisia na vichekesho lakini ukweli wa hali tete ya chama tawala umethibitishwa Dodoma. Kama Kikwete aliyesifiwa kwa sura yake nzuri, tabasamu lake, 'ujana' wake na ambaye amekuwa kwenye utumishi wa wizara nyingi muda mrefu amekifikisha chama chake hapa na Taifa ni vipi Magufuli anaweza kwenda zaidi wakati hata kama akishinda hatokuwa Mwenyekiti wa CCM hadi 2017 (kama Kikwete hatojiuzulu mapema)?


Kwa wale wanaotaka mabadiliko ya kweli CDM na washiriki wake wanatakiwa kujionesha wanaelewa kadi walizonazo mkononi na ni zamu yao kucheza kwani za CCM tumeziona zilivyochezwa na wamebaki na magarasa tu. Ni wakati wa CDM kuita "Last Card".


MMM​




 
Reactions: SMU
Kwa kifupi sisi wananchi ndio tunatakiwa kubadilika kwanza pamoja na jitihada zote za serikali kutupatia elimu ata kwa ku sacrifice baadhi ya raslimali(mali asili au madini),bado tumekuwa WAJINGA WA KUTUPWA!.. wasomi wakitafuna nchi(tamaa na ufisadi),wafanya biashara wakikwepa kodi,wakulima wakishindwa ubunifu,wanasiasa wakikosa sera na kuleta tafrani bungeni(wengi hawajui wafanye nini nchi iendelee)..mwisho tunategemea kusaidiwa na sisi sio watu wa industrial & technology, isipokuwa ni malimbukeni.HAKIKA HAYATI BABA WA TAIFA(KUPITIA HOTUBA ZAKE) NA SHAABAN ROBERT(KATIKA KITABU NCHI YA AHADI) waliyaona matatizo yetu!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…