CCM kumchukulia hatua makamu mwenyekiti CUF

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, 02 August 2011 19:48 newsroom
https://www.jamiiforums.com/index.p...hdGlkPTc3OnBlcnNvbmFsLXRlY2gmSXRlbWlkPTE3Ng==https://www.jamiiforums.com/index.p...hdGlkPTc3OnBlcnNvbmFsLXRlY2gmSXRlbWlkPTE3Ng==https://www.jamiiforums.com/index.p...t=default&page=&option=com_content&Itemid=176https://www.jamiiforums.com/index.p...t=default&page=&option=com_content&Itemid=176https://www.jamiiforums.com/index.p...-cuf&format=pdf&option=com_content&Itemid=176https://www.jamiiforums.com/index.p...-cuf&format=pdf&option=com_content&Itemid=176

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kitamfikisha mahakamani Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis Ali, kwa kauli chafu na za kebehi alizotoa dhidi ya serikali. Pamoja hilo, kimelaani matamshi ya kebehi yaliyotolewa na Ali kwa kuwaita viongozi wake wa Zanzibar ni watumwa wa utetezi wa muundo wa serikali mbili katika Muungano. CCM ilimtaka pia Machano kufuta kauli yake ndani ya siku saba na kuomba radhi huku ikitishia kukifikisha CUF mahakamani na kwenye jumuia ya kimataifa pamoja na washirika wengine wa maendeleo. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema matamshi hayo yana lengo la kuziamsha siasa chafu na kutaka kuisambaratisha serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar. "Kauli hii ya Machano si ya kiungwana, imekosa ustaarabu na haikufaa kutamkwa katika kipindi hiki cha mpito ambacho dunia nzima inaitazama Zanzibar kwa macho mawili ikielekea katika kufungua kurasa mpya za maelewano na kuzika uhasama," alisema Vuai. Alisema neno utumwa lilikataliwa na Wazanzibari tangu mwaka 1964 baada ya mapinduzi matukufu yaliyouondoa utawala wa kisultan na vibaraka wake.

Vuai alishangaa na kuhoji iweje ndani ya Zanzibar huru kutokee viongozi na wananchi kuwa watumwa. Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema chama chochote cha siasa hutokana na imani ya itikadi na muundo wa sera zake mbele ya jamii, hivyo CCM inapotetea muundo wa serikali mbili uendelee, inafanya hivyo kwa kutekeleza sera zake. Aliwaonya viongozi na wanaharakati wanaowapotosha wananchi, kuacha kufanya hivyo na badala yake wawe waungwana kwa kuelezea faida na tija zilizopatikana tangu kuwepo kwa muungano miaka 47 iliyopita.
 
Back
Top Bottom