Mkuu Mzee wa Rula ya Lema inasikilizwa tarehe 20.09.2012....Kama wamekata rufaa watasaidia kupush nayo rufaa ya Lema itoke haraka maana haiwezekani iwahi kabla ya Lema halafu mambo itajulikana mbivu na mbichi, uchaguzi au arejeshewe ubunge wake Lema.
Naona leo mwenyekiti wangu anajaziba kweli.....Hiyo ni janja ya nyani ya CCM kula mahindi mabichi mwisho wa siku ni kufukuzwa na mwenye shamba!!!
Waliache jimbo la Igunga liende kwa mshindi halali.
Habari nilizozipata muda si mrefu zinaeleza kuwa uongozi wa juu CCM umeamua kukata rufaa kesi ya uchaguzi Igunga.
Lazima wafanye hivyo kama njia ya kupunguza aibu waliyovuna kutokana ubabe walioufanya kwa wapiga kura wa Jimbo la Igunga.Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya C.C.M-Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
imesema kuwa hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa hapo jana ya kumsimamisha ubunge mbunge wao Dr. Kafumu na hivyo watakata rufaa.
SOURCE: Michuzi Blog
Wanapoteza Muda Tu.!Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya C.C.M-Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
imesema kuwa hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa hapo jana ya kumsimamisha ubunge mbunge wao Dr. Kafumu na hivyo watakata rufaa.
Yawezekana hiyo hukumu ilikuwa kiini macho tu ili kuusafisha Mhimili huu wa dola ambao kwa hivi karibuni Unakumbwa na kashfa ya kubeba majaji vihiyo. Yawezekana baada ya kukata rufaa wakashinda na kurudishiwa kiti chao. Tunaweza tukaisifu sana mahakama lakini mwishoe ikala kwa sisi!
Haki ya CCM kukata rufaa kwenye kesi hii inatoka wapi? CCM si mmoja wa washtakiwa katika kesi ya msing, itakata rufaa kwa misingi gani kisheria? nadhani wenye haki ya kukata rufaa nui aidha Dalali, mwanasheria mkuu au msimamizi wa uchaguzi ambao ndio walioshtakiwa. inachoweza kufanya ccm ni kumshauri au kumwelekeza mgombea wake akate rufaaDemokrasia na utawala
wa sheria uheshimiwe. Rafani ni haki ya msingi ya kila mtu. CCM isibezwe
kwa kutumia haki yake ya msingi.