PostGE2025 CCM kubalini yaishe, mtamponza Mama Samia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nani sasa wa ku-take blames kila raisi hataki jumba bovu limuangukie ataweka hata milingoti ili kumsukumia ajae and that is what they do
 
CCM ilishakufa kitambo tu. Kwa sasa kuna genge tu la wahuni wachache. Na hawa ndiyo wanaomuendesha huyo mama kama gari bovu.
Ni kweli kabisa na uzuri Watanzania wenye akili wameshaligundua. Hata wakati wa Chama kimoja Nyerere hakuwahi kufanya kufuru hii ya mauaji .Eti mtu akikosoa basi adhabu yake ni kifo? Haikubaliki kabisa😭😭😭
 
Mbona ccp yq china ipo mpaka leo
CCP ya China ni chama chenye maono na wanatumia Meritocracy yaani Uwezo wa Kiongozi unakuwa vetted na muendelezo wa matendo na akili yake kwa muda mrefu.
Wanapanga mipango yao mbele ya wakati.

CCM kwa upande wake ilikuwa wakati wa kuundwa kwake ikiwa na misingi ya kutetea Wakulima na Wafanyakazi na ikifuata falsafa ya Ujamaa. Lakini kwa Sasa imepoteza Dira, sio chama cha siasa, ni kikundi cha kutawala si kwa ushawishi bali mabavu. Viongozi wake hawana Falsafa na dira, wanalojua ni kuendeleea kushikilia dola. Njia hii inayokosa ridhaa ya Umma haiwezi kwenda umbali mrefu
 
Wengi wao si watu wakusoma nyakati, wamekariri kuongoza kwa vitisho
 
Nani sasa wa ku-take blames kila raisi hataki jumba bovu limuangukie ataweka hata milingoti ili kumsukumia ajae and that is what they do
Ilibaki kidogo limwangukie Kikwete, ila Kikwete ni mtoto wa mjini tofauti na huyu hana huo ujanja.
 
Poleni sana CCM tulikuwa nanyi siku za mateso lkn Mungu amewapenda zaidi.
 
Who are you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…