CCM kubadili upepo wanapoelemewa nini maoni yako?

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,881
1,124
Wana jf nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za ccm toka mwaka 1985,ccm imekumbwa na misukosuko mingi kuanzia miaka hiyo mpaka leo hii .

Kuna kipindi walikuwa na mikakati mizuri sana ya kushughulikia matatizo na changamoto zao lakini kila miaka inavyoenda naona mambo kama yanabadilika,mwanzo waliweza kuwadhibiti makada wao mf abdul jumbe,maalim seif,malecela. Katikati wakabadili style ya udhibiti mf kolimba na wengineo.

Sasa naona mambo yanazidi kubadilika mapacha watatu,tukumbuke wakati hawa watu walipoanza kuitwa mafisadi na wanaharakati ccm waliwakingia kifua ila mambo yalivyowachachia na vijana wengi wasomi kuanza kukimbilia upinzani wakashtuka na kama kukurupuka hivi wakawaagiza wajitoe kwenye chama kwa sababu wanakichafua(kumbuka si utaratibu wa ccm wa kubembeleza makada)

Rostam kajitoa jimbo la igunga likabaki wazi wakajisifu falsafa yao imefanikiwa wakaingia igunga,hakuna anaeongelea ufisadi,chama kujivua gamba wala nini. Mbaya zaidi wamegeuza upepo na kuvamia viongozi wa dini ya kiislamu.

DC wa Igunga ni mwanasiasa aliyeteuliwa na rais ni kada wa CCM hilo halipingiki kwangu mimi ni shangazi yangu kwa wengine ni mama yao wengine ni jirani yao,ni mpwa wao, ni mwanamke mwenzao na bila kusahau ni muumini mwenzao.suala lililofanywa na chadema liwe halali liwe si halali ni suala la kisiasa na kisheria basi.

DC kalalamika kadhalilishwa kiutu na kwa cheo chake tupo tuliolaani na waliopongeza,kesi ipo mahakamani,baada ya mbunge wa igunga kupatikana kesi hutaisikia tena kila mtu atarudi kwenye utaratibu wake.tutasubiri jimbo jingine litakalo baki wazi labda arusha mjini au tandahimba fitna za arusha mjini hazitafananishwa na arusha wala igunga.

Viongozi wa kidini wakikubali kuingizwa kwenye fitna za kisiasa(ambazo huwa hazidumu)sijui hatma yake itakuwaje ccm wameshachoka hawana jeuri ya kuwakemea makada wake wanaokiuka maadili ya chama.

Najaribu kufikiria je? ccm wanaweza kuwaingiza mkenge viongozi wa kikristo kwenye masuala ya kisiasa yaliyo wazi kama la dc wa igunga? na ni kwa nini wamefanikiwa kwa bakwata na shura ya maimamu?je nini mustakabali wa taifa kwani kuna dini mbili mkristo akifanyiwa kitu kwenye siasa maaskofu watoe tamko,mwislamu akikosewa bakwata na shura ya maimamu watake waislamu waombwe radhi.

NAOMBA MICHANGO ISIKAE KIITIKADI AU KIDINI ILA IZINGATIE MAMBO YAFUATAYO.
1.UZALENDO.
2.MUSTAKABALI WA CHAMA CHETU(CCM)
3.KUDUMISHA UDUGU WETU WA KITAIFA.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom