CCM: Kiti cha Spika kimeinyima nafasi CCM!

CCM: Kiti cha Spika kimeinyima nafasi CCM!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kishindo cha mikutano ya Wabunge sita wa CHADEMA waliosimamishwa na Naibu Spika,Job Ndugai, kwa uamuzi uliungwa mkono na Spika Anne Semamba Makinda,kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti kwa siku tano,kimeitikisa CCM. Inasemwa kwamba Kiti cha Spika kimewapa CHADEMA nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara wasiyostahili na hivyo kuibana na kujibu mapigo ya mikutano ya Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abduralhman Kinana.

Inadaiwa kuwa Kiti cha Spika ni kama kilipanga kuendeleza mapambano ya kisiasa nje ya Bunge kwa kuwasimamisha Wabunge sita wa CHADEMA ambao wote ni wasemaji mahiri. Kimsingi,Kiti cha Spika sasa kinalaumiwa na CCM kwa kuwasimamisha Wabunge: Tundu Lissu,Joseph Mbilinyi,Mchungaji Peter Msigwa,Ezekiel Wenje,Highess Kiwia na Godbless Lema ambo sasa wanachanja mbuga mikoani kuwashtaki CCM na Serikali yao kwa wananchi.Tayari Wabunge hao,wakiongezewa nguvu na Mwenyekiti wao Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu Dr.Wilbrod Peter Slaa pamoja na viongozi wengine wa litaifa wa CHADEMA wameshafanya mikutano ya hadhara Mwanza,Dodoma na Iringa.

' Unamsimamisha Lissu,Lema na wenzao tena kwa siku tano unategemea nini?' aling'aka Waziri mmoja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. 'Muda huu wa Bunge la Bajeti ulikuwa muafaka kwetu(CCM) kufanya mikutano ya hadhara bila mawaa. Ndivyo ilivyopangwa na kukubaliwa na chama. Ndivyo afanyavyo Katibu Mkuu Kinana na Nape Nnauye. Sasa Kiti cha Spika kimeturudisha nyuma na kutuharibia mipango yetu' aliongeza.

Waziri mwingine ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa Kiti cha Spika kitashtakiwa kwenye vikao vya chama kwa kutoa nafasi kwa CHADEMA kujibu makombora ya CCM muda huu. ' Lazima tuwashtaki katika vikao. Laiti Wabunge hawa wangetingwa na vikao vya Bunge,wasingeweza kufanya kama wafanyavyo sasa. Hapa kuna harufu ya mpango maalum wa kuibeba CHADEMA. Bora hata Kiti cha Spika kiwaite haraka Wabunge hawa Bungeni ili kuwapunguza kasi' alisema Waziri huyo aliyeungwa mkono na Mawaziri wengine pamoja na Wabunge.

Ilikuwa ni katika Kikao kisicho rasmi cha kichama kilichofanyika hapa Dodoma baada ya kuwepo na uzushi kuwa eti CHADEMA imewachochea wananchi wa Liwale na wananchi hao wanajiandaa kuandamana na kufanya fujo.

Kizungumkuti kweli kweli!

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam ( sasa Dodoma)
 
mkuu nakuaminia sana, lakini ngoja vijana wa buku 7 7 wa lumumba wa kinana na nape waje, jiandae na mvua ya mawe,,

unajua mkuu sisiemu mnakosea sana, yaani nyinyi mngejikita katika sera zenu na kutatua matatizo ya wananchi, vyama pinzania kama CHADEMA vingekufa nataural death, unazani wangesema nini??/

sasa tatizo la chamachenu sijui halina washauri au ni ukaidi tu, au ni jadi nyinyi kudanganya, na matatizo haya ya ahadi hewa 68 mlizozitoa 2010 yatawasumbua sana 2015,

timizeni ahadi zenu mlizozitoa kwa wananchi tangu 1992 hiyo ndio njia pekee na salama ya kuzibiti upinzani, tofauti na hapo polisi watajisumbua bure kuzuia na kuua watu
 
CCM imeshakufa....na elewa kwamba
Penye msiba...kila mtu huonekana mchawi!
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.
 
sure vuta-nkuvute CCM makundi bado yapo tena yana nguvu kubwa sana na kinchoendelea ni kukomeshana chezea EL au watu mmesahau aliyemuweka Makinda kwenye kiti ni nani. wakitia jiwe wao wanaeka ugoko CHADEMA full kuchanja mbuga tu
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.

WEWE ENDELEZA DHARAU DOGO KUWAITA WATZ WAJINGA, NANI KAFANYA WAMEKUWA WAJINGA KAMA SIO MASHETANI NYINYI MNAONGOZA HII NCHI KWA MIAKA 51 SASA....MPUUZI MKUBWA WEWE, DOGO UNADHARAU SANA KWA KUWA WEWE UNAPATA BUKU SABA KUTOKA KWA MUME WAKO MWIGULU UNAJIONA UNAAKILI SANA, NANI KASABABISHA WATZ WASIPATE ELIMU BORA....ETI BINTI zile pesa mlizokuwa mkichangisha watu kwa mpesa za uchaguzi za 2010, zilipatikana sh ngapi?? au hata hukumbuki hivi ziliwahi kutolewa mrejesho wa matumizi. hivi uchaguzi mkuu mlitoa ahadi ngapi unazikumbuka....???

BINTI SUMU kwanini mliamua kufanya kampeni za uchaguzi wa urais zikawa za kifamilia.... naona unatafuta buku saba ya kula mchana.. utapakatwa sana binti

kamoniii....f... u
 
.....Waziri mwingine ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa Kiti cha Spika kitashtakiwa kwenye vikao vya chama kwa kutoa nafasi kwa CHADEMA kujibu makombora ya CCM muda huu. ' Lazima tuwashtaki katika vikao. Laiti Wabunge hawa wangetingwa na vikao vya Bunge,wasingeweza kufanya kama wafanyavyo sasa. Hapa kuna harufu ya mpango maalum wa kuibeba CHADEMA. Bora hata Kiti cha Spika kiwaite haraka Wabunge hawa Bungeni ili kuwapunguza kasi' alisema Waziri huyo aliyeungwa mkono na Mawaziri wengine pamoja na Wabunge..... ( sasa Dodoma)

Tafakari hapo kwenye red
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.

Kule hakuna walevi kama wale walio ibiwa kule hotelini Morogoro (Mzee wa Bunduki 2).
 
Kuna mdau mmoja aliandika hapa kuwa Ndugai ni CHADEMA. Pengine yuko sahihi maana hatua yake ya kuwafungia wabunge 6 wa CHADEMA kwa siku tano, imeleta hasara tupu kwa CCM.

Kwa muda wote huu waliokaa nje hawa wabunge, hakuna mwananchi anahangaika na kinachoendelea bungeni, na hivyo hoja za serikali ni kama wamezisomea gizani. Watu wako busy wanafuatilia mikutano ya wabunge wa CHADEMA, na sumu ambayo wamemwaga hawa wabunge haiwezi kutoka! CCM wanadhulumiwa na kiti cha Spika!
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.

Noma hakuna kama za Mafisadi walivyokusanya hela zetu na kwenda kuwapatia wa Uswiz wafanyie biashara... sie watanzania ni watu wakarimu... bora hawa wa CDM wanakunywa bia wanaongeza mapato TBL na kodi inapanda na CCM wanaipiga ili waendelee kutuibia...
 
Asante sana kaka kwa kutuhabarisha haya .Indeed Ma CCM jana yatakuwa yameumana maana najua Nape yuko hapo kwa kazi maalumu na vikao na wabunge
 
Sisi tuna mungu wao wana pesa

NGOJA WALIONGWA PESA WAJE KUWATETEA WAKUU WAO
 
yule spika bibi jana kawaburuza wabunge kukipitisha kifungu cha ruzuku ya mbolea,yani ni mwakilishi wa serikali bungeni!
 
Kilichobaki CCM ni kulaumiana tu mpaka watakapong`oka 2015, kila fitna wanazofanya zinawabeba CDM
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.

Kuna maali Biblia inasema '' husimfunge punda kinywa apulapo nafaka'' maana yake mwache avune nafaka ila akisikia njaa ale nafaka hizo hizo hisuifunge mdomo wake, Hacha CDM wakomboe Wa TZ na wale kwa jasho hilo hilo la Watz.

NYIE KULENI HELA ZA WAKULIMA WA KOROSHO LINDI!
 
Hawajua tatizo sio CDM bali ni kutodeal na matatizo ya wananchi.........wame loose focus kabisa.
 
Wabunge wa CHADEMA wameshakusanya hela za wajinga kwenye hiyo mikutano yao baada ya hapo wanaenda Bar kujipongeza.

13.+Kinana+akikabidhi+Mbuzi+kwa+nahodha+wa+timu+ya+Libenenga,++Steven+Maundu.+Kulia+ni++bdallah+Mazengo+wa+Nkongo+FC+iliyofungwa+2-0+Kinana+Cup,+Ulanga.jpg
 
Back
Top Bottom