PreGE2025 CCM kigambaoni yaonya kampeni za mapema

PreGE2025 CCM kigambaoni yaonya kampeni za mapema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,565
Reaction score
2,484
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kimekemea na kulaani vikali vitendo vya baadhi ya watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani kuanza kampeni kabla ya wakati pamoja na kutoa rushwa, kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Akitoa taarifa hiyo wakati wa uwasilishaji wa tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 katika Kata ya Kibada, ambapo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni, Yahya Sikunjema, amesema chama kwa kushirikiana na mamlaka za serikali hakitasita kuchukua hatua kali kwa wote watakaobainika kukiuka maadili ya uchaguzi kwa kutoa rushwa.

Amesema utekelezaji wa ilani hiyo umefikia asilimia 99, jambo linalodhihirisha dhamira ya chama hicho katika kutimiza ahadi kwa wananchi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kibada, Amini Sambo, amesema utekelezaji wa ilani umeendelea kuleta mafanikio makubwa kwa wananchi, ikiwemo kutatua changamoto zilizodumu kwa muda mrefu, kama vile ujenzi wa barabara ya Kibada hadi Mwasonga yenye urefu wa kilomita 45 kwa kiwango cha lami.

Pia soma Pre GE2025 - CCM Kuzuia Watia Nia Mapema: Kuminya Demokrasia au Kuthibiti Nidhamu ya Chama?

Katika tukio hilo pia alikuwepo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Kibada, Mboni Mbegu, ambaye alieleza namna wanawake wanavyoendelea kunufaika na utekelezaji wa ilani hiyo, hasa kupitia miradi ya maendeleo na uwezeshaji kiuchumi ambapo amewahasa wanawake kuchukua fursa za kuingia katika kugombea nafasi mbalimbali.
 
Hahaha mapema ya kigamboni ni lini?

Ni nzima ccm wanafanya kampeni miaka na siku zote bila kupumzika au ccm ya kigambini ni tofauti na hii huku Tanganyika?
 
Kuna diwani mmoja
Hahaha mapema ya kigamboni ni lini?

Ni nzima ccm wanafanya kampeni miaka na siky zote bila kupumzika au ccm ya kigambini ni tofauti na hii huku Tanganyika?
Aliyeshiriki kuuza na kuzulumu mashamba ya watu anahonga pesa kama hana akili vizuri
 
Kampeni gani hawa jamaa wanazizungumzia? Mbona kampeni zomekwishaanza mapema mpaka watu wamekwisha jinadi kwamba wao ni usalama wa taifa hawatishwi?
 
Back
Top Bottom